Udafisi: Mbinguni ni wapi endapo binadamu tukifa tunazikwa Ardhini?

Udafisi: Mbinguni ni wapi endapo binadamu tukifa tunazikwa Ardhini?

Hakuna sehemu panaitwa mbinguni ni kauli tu za kwenye maandiko yaliyo andikwa na binadamu kama wewe ndio yanadai Kuna mbingu
ila unaamini wewe ulitokana na manii ya baba yako na yai la mama yako,?
 
kabla ya kuuliza kuhusu mbinguni. tujiulize sisi tumetoka wapi
Yaani hapo ndi shida inapo anzia. Kwa akiri za kidunia labda kina viumbe vimetutengeneza na vina tu control kama tunavyo control computer zetu.
 
Ufahamu wako hapo ndo ulikofika! Maana nikikuuliza Mungu anaishi wapi utaniambia ni mbinguni, nikikwambia mbinguni umewahi kufika utaniambia hapana! Nikikuuliza shetani yupo utaniambia ndio nikikuuliza anaishi wapi utaniambia ni kuzimu je kuzimu ni wapi???? Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa ukomo wa kufikiri na kuwaza, ndo maana mambo ukianza kujiuliza hayana majibu! Kwa hiyo amini kwamba Mungu yupo na kama Mungu yupo amini kwamba mbingu ni halisi na kuzimu ni halisi, kinachobaki ishi kwa imani ndipo utakapompendeza Mungu! Siri zote za wapi mwanadamu anaenda baada ya kifo zimeandikwa kwenye biblia, na kinachozikwa ni mwili tu lakini roho ambayo ndio uhalisi wa mtu huwa haipo toka huyo mtu alipokata pumzi siku ya kwanza! Na kwa nini mwili unaenda mavumbini biblia imeeleza!! Tatizo binadamu ni wabishi sana hamtaki kusoma biblia, hamtaki kuokoka na kumwamini Yesu!
Note: bila kumwamini Yesu amini kwamba utatupwa motoni na baada ya kifo unaenda kuzimu! Kuzimu na mbinguni ni sehemu ambazo zinafikika kupitia kifo tu! Bila kufa hizi sehemu huwezi kufika! Maana zinatambulikana kwa jinsi ya Rohoni!!
Asante Kwa ufafanuzi
 
Back
Top Bottom