Uchumi wetu kumbe.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchumi wetu kumbe..............

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Columbus, Oct 27, 2012.

 1. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Katika siku nilizowahi kusononeshwa ni jana, nilibahatika kusikia mjadala fulani redioni nikasikia uchumi wa Tanzania hautokani na kilimo wala viwanda bali tanzania limekuwa taifa la kichuuzi. Inakuwaje watanzania tunapanua masoko ya bidhaa kutoka China na India badala ya hayo masoko kubaki kwao, kwa maana nyingine nchi hizi zimekuwa kubwa kuliko tunavyozijua katika ramani.

  Hizi nyumba zinazorekebishwa mitaani karibu kila kukicha ni kwa ajili ya kuuza bidhaa mbofu mbofu za kichuuzi kutoka China na India, hivi hawa viongozi wetu wanalijua hili? na kama wanalijua wanalifurahia au linawakera kama mimi.

  Nchi yenye rasilimali lukuki kama madini ya aina nyingi,mbuga za wanyama wa kila aina,maziwa yenye samaki wa kila aina,misitu yenye uoto wa asili,mabonde yenye rutuba inayostawi mazao ya kila aina, watu walio na utulivu,nguvu na ari ya kujikwamua isipokuwa wamekosa wa kuwaongoza.

  Sasa hivi inaonyesha hatuna sera yoyote, upepo unakoelekea ndio huko huko. Shime shime watanzania wenzangu tunaachwa nyuma katika ulimwengu huu tuamke tuseme sasa basi inatosha.
   
Loading...