'Uchumi wa Kifisadi: Injini inayoendesha Nchi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Uchumi wa Kifisadi: Injini inayoendesha Nchi'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Nov 25, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kumbe ni hatari tena hatari sana kujaribu kuzuia ufisadi. Hatari hii wanaharakati na wapiganaji maarufu kama Mwanakijiji wameifumbia macho au hawajui kuwa ipo. Hii ni hatari ya kujaribu kuvuruga mfumo ambao kumbe ndio unaoendesha nchi. Huu ndio mfumo utupao nishati ya umeme, huduma za maji, elimu, afya na kadhalika. Kila kunapokuwa na jitihada za kuutibua mfumo huu basi nchi huingia gizani, kipindupindu huzuka na magonjwa lukuki hutuvamia. Heri tuuache mfumo wa zimwi likujualo uendeshe nchi yetu hivyo hivyo tu!

  Kwa ufupi huu ndio mfumo ambapo Mtanzania aliyeliona jua kuanzia 1985 na hasa 1995 huzaliwa, hulelewa, hukua na hata hufa. Kama anavyonena Mwana wa Ulimwengu katika Rai ya Jenerali, mtoto aliyezaliwa katika ufisadi (na naongezea, aliyezaliwa kifisadi), na kulelewa kifisadi basi huishia kuwa fisadi tu. Naam na kama unavyothibitisha Utafiti wa gazeti la The Citizen, Mtanzania kwa kawaida hupitia hatua elfu za ufisadi toka anapozaliwa hadi anapoingia kaburini. Kwa kawaida cheti chake cha kuzaliwa hupatikana kifisadi, hupata nafasi ya kujiandikisha darasa la kwanza kifisadi, hutumia desa au mafeki kufaulu mitihani ya taifa na ikibidi hufanya ufisadi ili afaulishwe. Safari hiyo ya kifisadi haishii hapo. Kama akiwa dereva basi kwa kawaida hupata leseni ya udereva kifisadi, akipata ajali basi husamehewa na matrafiki kifisadi. Siku akiamua kumiliki ardhi au nyumba basi hupata hatimiliki kifisadi. Na hata akitaka kuwa kiongozi basi hupata kura kifisadi na pia huweza hata kutumia cheti cha uprofesa wa kifisadi ili atinge mjengoni. Hata harakati na upiganaji hufanyika kifisadi pia, kama huamini waulize mashujaa wa vita dhidi ya ufisadi ni jinsi gani wanapata taarifa za ufisadi na huwa wanazipata kwa nani na wakati gani!

  Kwa ujumla hayo ni maisha ambayo yanaendeshwa kwa uchumi wa kifisadi. Huu ndio uchumi unaomfanya dereva wa taxi amuulize mteja wake aandike shilingi ngapi kwenye risiti kana kwamba hajui bei halali anayopaswa kuandika ni shilingi ngapi! Ni mfumo ambao umeufanya ufisadi ujikite katika nyoyo na fikra za wananchi na jamii kwa ujumla. Hakika kikulacho ki nguoni mwako, naam ufisadi u nguoni mwetu. Kumbe yule mtafiti tuliyetaka kumpiga mawe alikuwa sahihi aliposema kuwa uchumi wetu ni wa kujaliana, naam, kifisadi!
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Ukweli unauma! Lakini ndio ukweli wenyewe!! Tumejikita kwenye tatizo ambalo kujitoa kunataka uwendawazimu ambao Marehemu Thomas Sankara aliwahi kusema ili kuushinda sharti mtu uwe kama mwendawazimu vile.....

  "I would like to leave behind me the conviction that if we maintain a certain amount of caution and organization we deserve victory[....] You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness. In this case, it comes from nonconformity, the courage to turn your back on the old formulas, the courage to invent the future. It took the madmen of yesterday for us to be able to act with extreme clarity today. I want to be one of those madmen. [...] We must dare to invent the future."
  Thomas Sankara
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Sa mtu analipwa 150,000 kwa mwezi, how do you expect him/her kutoboza mwezi wa 13?

  Mambo haya yapo damuni, na yamepewa full-baraka indirectly na sirikali!
  Vinginevyo ingeshaunda tume kuchunguza hawa watu wanafanyafanya vp, huku wakiwa na familia ya watoto 6, na wategemezi wa kumwaga.
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Busara bandia, washauri bandia, maendeleo bandia

  Jenerali Ulimwengu

  Agosti 5, 2009

  TUMEONA katika makala ya wiki jana jinsi kitoto kilichozaliwa katika familia ya mafisadi kinavyolelewa kifisadi, kinavyosomeshwa kifisadi, kinavyofanywa 'kifaulu' kifisadi, kinavyoajiriwa kifisadi, kinavyoozeshwa kifisadi na kinavyokuwa kitu kingine cha ufisadi katika mwendelezo wa utamaduni wa ufisadi kilimozaliwa.

  Sidhani kwamba tunaweza kuwa na matumaini ya kupata lo lote la maana kutoka kitoto hicho kwa maana ya kuiendeleza nchi na kuwaendeleza watu wake. Watu wa aina ya kitoto hicho hawawezi kuijenga wala kuiongoza nchi, kwa sababu wao hawajajengwa wala kuongozwa katika misingi ya kujenga lo lote la maana isipokuwa kuendeleza utamaduni uliowazaa na kuwalea.

  http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1596
   
Loading...