Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,558
- 41,078
Nchi Yenye Matatizo makubwa ya umaskini, huduma na mifumo mbalimbali, kama ilivyo Tanzania, ili iweze kutoka ilipo, inahitaji viongozi wenye ubunifu zaidi, akili zaidi, uadilifu zaidi na uzalendo zaidi kuliko Nchi zilizoendelea.
Bahati mbaya, nchi hizi zenye matatizo kama Tanzania, ndiyo zinazoongoza kuwa na viongozi walio duni zaidi katika ubunifu, uadilifu, akili na uzalendo. Wengi wanatafuta uongozi ili waondokane na umaskini au ili wajitajirishe zaidi, na hivyo kuyaongeza matatizo zaidi kuliko kuyapunguza.
Ni vema tukawa na mfumo unaowachekecha wale wote wanaoutafuta uongozi ili kujitajirisha na kujineemesha.
Kwa kuanzia, tungeweka sheria ya kipindi cha mpito, angalao cha miaka 20, viongozi wa kisiasa, wale wanaochaguliwa na wananchi, wasiwe na mishahara. Badala yake walipiwe gharama kama vile malazi, usafiri, matibabu, na chakula tu, pale wanapokuwa mbali na makazi yao. Lengo iwe ni kuwaondoa wale wote wanaoutafuta uongozi kwa dhamira ya kujineemesha.
Kisha kuwe na sheria maalum kwaajili ya kuwadhibiti viongozi ambao watakuwa wamekosa uadilifu kama vile kupokea rushwa au malipo yoyote yanayohusiana na ufisadi. Viongozi hao baada ya kumaliza muda wao, kuwe na kamati maalum ya kufuatilia utendaji wao wakati wakiwa viongozi, na wale wote ambao watathibitika bila shaka kuwa walifanya kazi kwa weledi mkubwa, ujasiri, ubunifu, na kwa uadilifu mkubwa, watapewa vyeti maalum na kupewa malipo ya mara moja ya uongozi uliotukuka. Wale ambao watathibitika kutenda kinyume chake, watatangazwa majina yao kwa umma, na wasiruhusiwe kugombea nafasi yoyote ya uongozi kwa kipindi cha miaka 20.
Hii itawafanya wanaotafuta pesa kupitia uongozi kutogombea uongozi, na waliopo kwenye uongozi kufanya kila wawezalo kutenda vyema ili mwisho wa term yao wapate mafao mazuri, na kuruhusiwa kugombea uongozi.
Tukiwekwa sheria ya namna hii, hakika nami na wengine wengi wasiopenda kuchafuliwa na mifumo ya kifisadi iliyopo, tutagombea uongozi.
Kama kweli mtu unasema unataka kuwasaidia watu na Taifa kupitia uongozi, basi dhamira hiyo ionekane kwa vitendo. Isiwe kinyume chake. Unasema unataka kuwasaidia watu kupitia uongozi kumbe unataka kuwaibia watu na Taifa kupitia uongozi. Nchi inahitaji viongozi wanaoumizwa na matatizo ya Taifa, lakini siyo kuumizwa tu bali wenye uwezo na walio wabunifu wa kuyaondoa au kuyapunguza hayo matatizo yanayowaumiza.