Naomba ushauri jamani ndugu zangu nilipendana na binti mmoja kwa kipindi cha muda wa miaka minne hadi sasa lakini ikafikia muda yeye baada ya kumaliza chuo tukaamua kuwajulisha wazazi ili taratibu zingine zifuate barua, washenga na nyinginezo lakini sasa mahari iliyotajwa milioni tano mimi sina hata baiskeli na binti tunapendana hatari sasa anaujauzito wangu na wazazi hawajajua hili sasa nifanyeje ili nipeleke mahali kwao maana binti anataka nimuoe na wazazi washasema kumtoa pale kwao mpaka pesa yote itimie mil.5 sasa nipo njia panda nifanyeje hapa wadau maana nataka nimuoe huyu.