Uchumba kuvunjika ...kisa HARUSI

Me naomba kama anampiga chini huyo mchumba wake basi aniachie tu namba yake. Labda na mimi nitakula tunda kimasihara ili nije nilete kisa changu kwenye ule uzi wetu pendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa ni shaidi wa yehova huyo atakuwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
100%kwa uyo mzee, ni kama mm kabisa sijawah kuwa mfuasi wa sherehe zisizo na tija ndoa ni agano kati ya muaji,muolewaji na Mungu wao safi[emoji1547].piga chini uyo binti
 
Huyo mzee kama mzee wangu aisee... Tushakubaliana future husband akikubali tunafunga ndoa kanisani tena ikiwezekana ofisini kwa mchungaji jioni dinner ya familia. Sipendi misherehe na kuingia gharama za kijinga
 
Housegirl kaingiaje? 🤣🤣🤣
 
Kuna binti alikua ni jirani yangu na tunaabudu sehemu moja .Basi bwana mi sina hili wala lile nikapewa taarifa/mualiko natakiwa kuwa mwanakamati kwa ajili ya hiyo send off ya huyo kigori .Changa mapesa kimbizana na michango bongeee la sherehe likafanyika.Nikaombwa tena kama kijana mwenye busara na heshima niongozane nao kwenye kufunga ndoa mji kasoro.Picha linaanza bwana harusi kasema yeye atahudumia watu wanne tu,mama wa biharusi kachukua ndugu ,majirani tumekaribia kujaza coaster 2 na nusu.Kufika kwenye eneo la tukio ,ndoa imefungwa kanisani tumerudi nyumbani tumekula ubwabwa pale zikapigwa picha mbili tatu Mc akatangaza jamani na huu ndio mwisho wa sherehe hakuna party hakuna nini.Wacha mama wa binti aanze kulia na kujigaragaza huku anamtaja jina bwana harusi kuwa kamdhalilisha,kamtia aibu kwa ndugu ,jamaa na marafiki.Nilichojifunza tunaongozwa sana na sifa kuliko uhalisia wa maisha.
 
Duuh kweli Wanasuaso Akili zinafanana.. hata Mimi huo ujinga wa harusi siukubali hata kidogo.
Subri nikifikia hiyo hatua Wachache tu ndo watanielewa Ila wengi watakuja kunishangaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia Tena kwa Akili zangu timamu Kufunga harusi na Mwanamke wa kizazi hiki Cha online Ni Ujinga wa kiwango Cha SGR.

Ninayo mifano mingi juu ya mbwembwe za harusi zilizofungika lkn leo ndo zinazidi kutuongezea Ma single mother na ma braza men mtaani kila kukichaa.

Pia Naunga jitihada na msimamo wa mzee wetu Mwenye Akili nyingi kwa asilimia zote.(He has motivated me to follow his action)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…