UCHOKOZI WA EDO: Pambano la Waraka na ‘Clip’ limeisha sare?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,014
UCHOKOZI WA EDO: Pambano la Waraka na ‘Clip’ limeisha sare?

Thursday August 8 2019

Edo+Kumwembe.jpg

By Edo Kumwembe

Tumeachwa katika mataa. Kule katika soka kuna mechi zinamalizika kwa matokeo ya sare. Kuna mechi haiwezekani kumalizika kwa sare. Lazima mshindi apatikane, hata kwa mikwaju ya penalti. Tulidhani katika siasa lazima mshindi apatikane.

Kwa mfano, tumeona Mzee Mamvi amerudi kundini. Ni ishara kwamba pambano limemalizika kwa ushindi wa upande wa Namba Moja. Tumepiga makofi, tumeondoka uwanjani kurudi majumbani mwetu huku tukitabasamu. Tumeuona mwisho.

Lakini hapa majuzi kulikuwa na mechi kali kidogo ya kusisimua. Pambano la Waraka vs Clip za maongezi. Mbona inaonekana kama vile lile pambano la timu ya waraka dhidi ya timu ya ‘Clip za maongezi’ linaelekea kumalizika kwa
sare?. Bado tupo mbele ya televisheni zetu na rimoti zetu hatuoni kinachoendelea na umeme haujakatika?

Wale wazee wangu walikuja na waraka. Ulikuwa mrefu. Uliandikwa kwa umaridadi mkubwa. Baadaye upande wa pili ukaja na clip za maongezi. Hatujapata majibu halisi kuhusu waraka. Yalikuja majibu makali makali kutoka kwa Katibu, basi.

Hata hivyo bado tunajiuliza. Clip zililetwa kwetu kama majibu ya waraka au mashtaka ya kesi nyingine tofauti?

Vyovyote ilivyo waraka umepita na clip zimepita. Tunaona kimya kimetanda. Mechi inaendelea au imeisha? Nani mshindi? Ina maana clip zilikuwa ni majibu ya waraka?

Sisi wambea wa siasa holela tusingependa pambano liishe kwa sare. Lazima mshindi apatikane. Majuzi nikampigia rafiki yangu mmoja (Sina uhakika kama na mimi nimerekodiwa) akaniambia anadhani pambano lipo muda wa mapumziko.

Akaniambia mpaka kufikia uchaguzi mkuu wa mwakani tutajua nani alishinda katika mechi ile. Huyu rafiki yangu sikupenda alichoniambia kwa sababu sisi wengine tuna hamu mechi imalizike ndani ya muda mfupi. Kuna mambo mengi yanafanyika ndani ya muda mchache.

Uzinduzi wa uwanja wa kisasa wa ndege. Mkutano wa Sadc, hata hivyo nchi huwa inasisimua zaidi yakija mambo kama yale ya Waraka na Clip za maongezi. Wakati mwingine lazima tukiri kwamba tumerithishwa kupenda habari za siasa kuliko habari za maendeleo.
 
Hata mi wameniacha kwanye mataa, nilitaka hili pambano liendelee, lakini timu moja haikujibu hoja badala yake ikaja na clip, pamabano halitakiwi kwisha hivi hivi
 
Uchochezi huo
 
Hivi Kibajaji bado hajarudi kutoka china?
Maana alituaga kuwa anakwenda, siku akirudi tu 'atamchafua' Membe.
 
Hata mimi naona tuko half time tuendelee kuongeza korosho na Pepsi baridi ili wachezaji wanaporudi ulingoni tuwe na nguvu za kushangilia vizuri mtanange
 
Mhudumu naomba heineken mbili za bariiidiii......wakati nasubiria kipindi cha pili cha mtanange tafadhali.
 
Back
Top Bottom