Uchi mbele ya obama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchi mbele ya obama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Miranda, Oct 13, 2010.

 1. M

  Miranda Member

  #1
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ajitokeza Uchi Mbele ya Obama, Ashinda Dola Milioni 1
  [​IMG]
  Juan James Rodriguez alipotiwa mbaroni na polisi baada ya kujitokeza mbele ya rais Obama akiwa uchi wa mnyamaWednesday, October 13, 2010 3:54 AM
  Mwanaume ambaye alijitokeza mbele ya rais wa Marekani, Barack Obama akiwa uchi wa mnyama huku akiwa na maandishi ya kutangaza tovuti ya bilionea Alki David, amejishindia zawadi ya dola milioni 1 toka kwa bilionea huyo.Juan James Rodriguez, 24, alitiwa mbaroni na polisi baada ya kujitokeza mbele ya rais wa Marekani, Barack Obama akiwa uchi wa mnyama huku akiwa na maandishi makubwa kifuani na tumboni ya kutangaza tovuti ya bilionea Alki David.

  Rais Obama alikuwa Philadelphia akikipigia kampeni chama chake wakati Juan alipojitokeza mbele yake ghafla akiwa uchi wa mnyama.

  Bilionea Alki, Mgiriki aliyezaliwa Lagos, Nigeria alitangaza zawadi ya dola milioni moja kwa mtu yoyote atakayejitokeza uchi wa mnyama mbele ya rais Obama huku akiwa na maandishi ya kutangaza tovuti ya bilionea huyo inayoitwa “BATTLECAM”.

  Akiongea na waandishi wa habari, bilionea huyo alisema kuwa atatimiza ahadi yake kwa kumzawadia dola milioni 1, Juan ingawa kwa sasa wanaangalia video za tukio hilo ili kujua kama masharti yote ya zawadi hiyo yalifuatwa.

  Sharti la kushinda kitita hicho kinono lilikuwa ni kujitokeza mbele ya rais Obama na kuhakikisha Obama amekuona na pia kutamka kwa sauti kubwa “Battlecam.com” mara sita.

  Ingawa Juan huenda akashinda dola hizo milioni 1, alikamatwa polisi na kufunguliwa mashtka ya kujianika hadharani kinyume cha maadili ya jamii
   
Loading...