Habarini wakuu,
Ni muda sasa nipo kwenye mgogoro na mpangaji mwenzangu, tumefikia hatua mpaka hatusalimiani!
Siku za hivi karibuni nilikuwa npo kibaruani ,jion nilpo rudi nyumbani, nikapewa taarifa na bint wangu wa kazi alimuona huyo mpangaji mwenzangu akichukua dekio la ndan kwangu na kuchana kipande kidogo kisha kutokomea ndani kwake na kipande hcho!
Sasa wasi wasi wangu upo juu ya hilo tukio,maana huwa nasikia kua namna wachawi huwa wanatumia nguo au kpande cha dekio katka kumfanyia shikri mbaya wake!
Naomba mwenye kujua zaidi na namna ya kuepukana na haya mambo!