Uchawi wa kulogewa kibyongo, busha

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,826
730,266
Ukifuatilia kwa karibu haya mambo kuna mahali inafika unabaki na mshangao
Mtu anaanza kuugua from no where..!anajikunja kama ana kibyongo au kabeba kitu kizito hasa au anatembea utadhani ana busha na kuna wakati amevimba kabisa sehemu husika

Kwa usomi wa kimagharibi na kushika dini za kuletewa mnakuwa hamuamini katika nguvu za giza hivyo mnampeleka mgonjwa hospitali....anafanyiwa vipimo vyote kule lakini hakutwi na ugonjwa wowote, japo anaumwa kweli
Kwa shida sana mwisho wa siku mbakubaliana na ushauri wa baadhi ya ndugu au marafiki, wengine wanasema maombi na wengine wanasema kwa waganga wa kienyeji

Hawa wa mwisho wanashinda na mgonjwa kupelekwa huko kwa mganga husika , mnapokelewa na matibabu yanaanza

Mara mgonjwa anapewa dawa na kuanza kutapika vitu vya ajabu mara nyingi zikiwemo nywele kipande cha kaniki nk nk...mnatajiwa mbaya wenu mnapewa dawa ya kinga mnalipia matibabu na kuondoka

Wengi wamepigwa kwa namna hii...hawa watu waitwao waganga wa kienyeji wengi si waganga hasa bali ni matapeli wanaojua mazingaombwe, na wengi huwa na uwezo wa kumtengenezea mtu ugonjwa ili baadae aje amtibu na kupata sifa na kipato

Waathirika wengi kwenye hili ni wale wapendao sana kwenda kwa waganga kwa ajili ya kupata bahati ngekewa na kupendwa..ukifika pale atakusoma na kukufahamu mtazamo wako hivyo atakutengenezea phantom la kuja kukudhuru mbeleni
 
Lakini pia watu wa pwani ni hatari sana hasa linapokuja swala la mke wa mtu....kaa mbali mno na huyo binadamu
Mabusha ni aina fulani ya ugonjwa wa matendo unaoambukizwa na aina fulani ya mbu, lakini kule pwani unaweza kulipata busha overnight ukijifanya inasimama sana...mitaa ya kule kushushwa mshipa ni kitu cha dakika
 
Lakini pia watu wa pwani ni hatari sana hasa linapokuja swala la mke wa mtu....kaa mbali mno na huyo binadamu
Mabusha ni aina fulani ya ugonjwa wa matendo unaoambukizwa na aina fulani ya mbu, lakini kule pwani unaweza kulipata busha overnight ukijifanya inasimama sana...mitaa ya kule kushushwa mshipa ni kitu cha dakika
Kuna watu flan flan hawajaamka, wakiamka wataamka Na wewe, maana wanataka kukupangia cha kupost huku
 
Back
Top Bottom