Uchawi upo, usidanganywe

Wengine tunaamini uchawi wa mabarabara, mifereji iliyofunikwa, treni zinazoenda sambamba na UDA, huduma za afya bora, ustawi wa jamii kwa yatima, wazee na watoto, elimu bora, kazi na uchumi bora, huu ndio uchawi..
Ni rahisi sana kusema hivyo lakini ukiombwa uonyeshe huo uchawi wako kwenye ugunduzi wa hata plastic fetoscope kwenye mambo ya afya utashindwa. Na inawezekana hata kwenye ustawi wa jamii hata mwanao nyumbani hata siku moja haujawahi kumwogesha. Binafsi kama isingekuwa hayo niliyowahi kuyashuhudia na ambayo nimeyaelezea vizuri hapo nyuma yamkini ningekuwa mmoja wa wale wanaopinga kuwepo uchawi.

By the way if you're a christian, muslim or pagan how can you negate the existence of witchcraft whilst it has frequently been mentioned in our holy books?
 
Sijaona uchawi hapo, nilichoona ni Jamaa kwenda kujisaidia kisha kuvamiwa na tembo na mauti yakamkuta
 
Kuna jamaa m1 mid 90 alikuwa kamaliza chuo sasa kila akipata kazi anaacha baada ya kuifanya kwa muda mfupi. Baada ya kuangaika sana bila mafanikio mzee m1 wa makoamo akasema huyu atakuwa kalogwa. Basi wakaenda kwa wataalam walichoambiwa na dawa yake ni vigumu kuamini.

Aliambiwa kalogwa na dawa yake ni lazima aende kwenye msitu maeneo ya huko upareni. Alitajiwa eneo na aliambiwa atakuta nyuki wametulia juu ya mti. Basi awafukuze kwa aidha kuwapiga kwa mawe au kupanda na kuwaondoa kwa mkono. Vyovyote vile ilimradi watoke pale.

Watu wakatili. Jamaa akaongozana na yule mzee na ndugu yake m1. Walipofika maeneo hayo wakakuta nyuki kweli, walishahakikishiwa kuwa kutakuwa hamna hatari yoyote yaani nyuki watakuwa wapole kama inzi. Ila atagongwa na wawili au watatu. Wakaingia mzigoni wakafurumusha nyuki ambao waliondoka eneo lile. Kweli kuna nyuki kadhaa waliwagonga.

Waliporejea nyumbani wakakuta wale nyuki wapo kwenye moja ya banda la kuku pale home kwao. Wakarudi kwa bingwa na kumweleza. Akawaambia kuwa wale watakaa pale kwa muda wa siku sita na siku ya saba awafukuze tena kama alivyofanya kule msituni. Siku zikaenda muda ukawadia. Akawafukuza kama mwanzo ingawa siku hiyo alitolewa manundu ya kutosha. Baada ya kupita kama mwezi hivi jamaa akachukua ajira na sasa ni moja ya mabosi huko mkoani tabora. Hakuwahi kuacha kazi tena.
 
Ngoja waje mwenyewe, watakwambia ni coincidence. Vinginevyo uwathibitishie...
 
naona unatangaza biashara kiaina...
atuendi nyamongo
By the way yule mganga alishakufa mkuu. Afu mimi ni mkristo mwaminifu kabisa. Nakushirikisha tu mambo yaliyowahi kutokea zilipendwa
 
Hahaha! Wanajua mkuu, lile tukio halikuwa la kawaida.. So walijua kabisa. Baada ya lile tukio kulikuwa na mtafutano usiokuwa wa kawaida. Bifu bifu
Yaani pole sana. Ndiyo maana wengine kwenda huko tunaogopa. Waweza ondoka hivi hivi kwa sababu za kijinga kabisa.
 
Siyo Rsee Muaniri kweli? Jokes.
 
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji1] [emoji1] Frusa hii
 

Uchawi upo wasioamini ni wale waliozoea kukaririshwa mambo.
 
Sasa hapo mganga anahusika nini?simlizi ni nzuri sana lakini mganga hahusiki kabisa hapo poleni kwa kutapeliwa.shida hapo ni uelewa shida hapo ni akili ndogo kutawala akili kubwa utafiti unaonyesha uganga ni taaluma lakini pia waganga hutumia akili nyingi kulaghai watu mbinu wanazo tumia mi2 nitaziita 4+4 uganga unapgred kila mara ndio maana hata wao huzidiana mganga wa naijeria tofauti na tz unadhani kwa nin?ok mganga wa naijeria ni msomi na kwa kua hakuna ajira akajiajiri hivyo anaweza kukuletea hata simba nyumbani kwako na ukachanganyikiwa na uganga ni netwek kubwa siyo ya kitoto uganga una mbinu nyingi sio za kitoto.nikupe mfano huu we2 una ndugu yupo jela unaenda kwa mganga akupe dawa ili uchanganye kwenye chakula ukampe ndugu yako jela akila tu atatoka na kweli unafanya hivo ok tayari umesha mpa dawa wiki ya 3 toka umpe mara msamaha wa rahisi unatoka kwale walio tumikia kifungo chao nusu na ndugu yako ni mmoja wapo hivyo pengine katika gereza la ukonga wanatoka watu 500 na segelea 300 na kote nchini watu wanatoka magerezani sasa tumia akili yako je ndugu yako ametoka kwa msamha wa raisi au kwa dawa za mganga?0756805540 tuendelee kubadilishana uzoefu
 
Hahahhahahaahahaha hapa nimecheka kinoma

Kama unaaminishwa na sayansi kuwa uchawi sio real, endelea tu mpaka utakapopigiwa show kali ya kibabe na wazee wa kilingeni..
 
Japo umeandika bila vituo wala nukta ila sijaelewa point yako. Mchawi/mganga wa Nigeria anamzidi vipi mganga/mchawi wa Tanzania kama hakuna uchawi... Umetoa namba tubadilishane uzoefu wa kitu ambacho hakipo?
 
Hahahhahahaahahaha hapa nimecheka kinoma

Kama unaaminishwa na sayansi kuwa uchawi sio real, endelea tu mpaka utakapopigiwa show kali ya kibabe na wazee wa kilingeni..
Hahahah! Kweli tena mkuu.
 
Wachawi wamenitesa sana ila na wao nimewatesa sana maana walikuwa kila wakija iwe mchana au usiku Mie nawaona kuna kipindi nilikaa wiki mbili bila kulala tunasumbuana mwisho wakamtuma mwenzao akaja live na kuniambia Kumbe Mie mtoto lakini ni mkubwa
Ukiona mchawi huwezi kuishi kwa zaidi ya mwaka mkuu..otherwise na wewe ni mwenzao..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…