Hawa watoto wanasumbua sana mkuu hapa jukwaani ,wanafikiri wote tupo rika moja sijui.Li story la uongo et ulipomuangalia kwenye macho ukajua kua ni mchawi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] halafu ukaendelea kukkaa nae et akufundishe uchaw. Sasa ulimjuaje kua i mchaw kama ww sio mchaw. Halafu unafundishwa uchaw na mtu anaejifunza. Mbaya zaid ulikua na fisi wako kabla hujawa mchaw. Shkamoo
Huo sio mchawi na nina uhakika hana anachokijua kuhusu uchawiRais2020 mm naomba nikuulize kuna manufaa gani mnayapata kwenye shughuli zenu za uchawi?
Je,nyinyi wachawi kiboko yenu ni nani kwamaana mkisikia jina au ukui wake kazi zenu zinashindwa
Tafadhali naomba jibu
amekusoma nadhaniWashirikina watakaa Motoni milele,,,ila hujachelewa kumrejea Mola wako..yan wew unahitaji ruqya moja matata sana,kwanza hayo mazimwi yte ulionayo inabdi yaunguzwe na Quran..
Tubu kwa Mola wako toba ya kweli na uache kuwanga..
Afu wachawi mnachelewagwa kufa kama nn...
Mkuu kuna sehemu ulisema mwaka 2008 ulikuwa upo chuo sasa ukipiga mahesabu kutoka 2008 mpaka sasa umri wako upo kati ya 31_35 sasa kwa nini nisikuite mtoto?Mimi ni sawa na umri wa baba yako mkuu. Hebu tujaribu tu kuheshimiana
Unatumia nguvu kubwa kujiteteaJe,hujajiuliza kama nilikuwa chuo kama in service?
Jamaa kakupatia nn hahahaaHa ha ha ha ha ha ha ha
Hii ndio JF!!!
Mbona huuu ni mchezo wa kawaida tu,.. Hayo mbona wanaya fanyaga katika mchezo
Kuwa seriaz bhana!!!Habari za mida hii wakubwa na wadogo zangu,
Ni miaka takribani 8 sasa toka linitokee hili swala. Ilikuwa ni majira ya jioni siku ya Jumamosi. Nikitoka kimatembezi na rafiki yangu ili kunyoosha miguu na kuangalia mazingira. Kumbe rafiki yangu alikuwa ni mchawi anayechipukia na alikuwa ana miezi mitatu toka aanze kujifunza uchawi. Bahati nzuri wakati nimemuangalia macho yake niliona kila kitu juu ya kile alichokuwa anakifanya nyakati za usiku. Nilipomgundua tabia yake nilianza kukaa naye karibu ili anipe ujuzi wake wa kichawi. Kwa kuwa nilikuwa najua tu ulozi wa kutumia radi na usafiri wa fisi basi ilikuwa faraja sana kumpata huyu rafiki yangu. Hakika huyu jamaa alijifunza uchawi adimu sana wa kutumia usafiri wa mkuki na ulozi wa kutumia joka lenye vichwa vitatu.
Jamaa hakuwa mchoyo maana nilikuwa tayari nimevutiwa naye sana. Kuna siku jamaa tulisafiri naye kutoka Misungwi kuelekea Sengerema kwa ajili ya shughuli maalamu ambapo tulitumia usafiri wangu wa fisi ambao ulituchukua dk 10 kufika eneo la tukio. Wakati tunarudi kutoka sengerema kuelekea misungwi jamaa waliamu kunipitisha njia isiyo rasmi hali ambayo ilipelekea kupoteza mwelekeo ambapo nilijikuta nipo pekee yangu na fisi wangu.
Nikiwa nimepoteza mwelekeo ilinibidi kuchukua uamuzi wa kutoka kivyangu ili nifike kwangu kwa njia yoyote ile. Lakini gafla nikiwa safari nilipata ajali baada ya wachawi wenye asili ya Kigoma na Kikongo kunigonga. Kiukweli ilinichuka muda sana kupata fahamu na baada ya fahamu kunijia usafiri wangu haukuonekana. Hali hii ilinifanya kukamatwa na hawa wachawi wa Kigoma walionizidi uwezo.
Hawa wachawi wa kigoma walinipeleka kwenye kambi yao kwa ajili ya kunitoa sadaka. Walinipeleka kwa Kiongozi wao mnywa damu. Nilipofikishwa tu mizimu ya babu yangu ilinijia kwa nguvu sana na kuwashinda wote na wachache walipoteza maisha.
Nikiwa kwenye kambi yao niliweza kumchukua mmoja ya wafuasi wao na kumtoa damu zote mpaka kifo. Nilichomoa mfupa wake wa kidole GUMBA. Huu mfupa ndiyo ulinifikisha mahala pangu.
Nilipofika tu mahala pangu niliishiwa nguvu na kujikuta misukule na fisi waliokuwa kwenye ghala langu wanakimbia wote. Baada week Moja nilijiwa na nguvu za ajabu sana ambazo zinanitesa mpaka Leo. Hizi nguvu zinanifanya kutamani nyama za fisi na kunipa uwezo wa kuota dawa mbaya za kienyeji zenye uwezo wa kutoa uhai wa kiumbe chochote na kumalizana na wabaya wangu.
Naomba mwenye kujua jinsi ya kuondoa uchawi wa mtu tuwasiliane au anipe ushauri ili niondokane na hii Hali.
UCHAWI UNANIPONZA. NIMECHOKA NA UCHAWI.
Ni mimi Rais2020.