Uchawi haupo, ni imani tu

Sasa unatumia Mbinu gani? Mana Mimi naamini uchawi upo Sasa Nataka niitoe iyo mind set, hafu nione matokeo yake.
Yaani mkuu,utafanikiwa sana kwasababu hutaogopa chochote wala yeyote,isipokuwa Mungu,watu utawaheshimu na siyo kuwaogopa,ktk maamuzi hutatetereka,utafanya tu kwa kujiamini bila kuogopa yeyote ili mradi upo ktk Haki na usawa na busara ikitumika.Kuhusu mbinu Sali sana,Sana maandiko matakatifu,izoeze akili yako kufikiri positive juu ya mambo mbalimbali.
 
kwanini uchawi usiwepo halafu imani iwepo ?

kwanini tena useme uchawi ni imani?
Namaanisha kuwa Uchawi km Uchawi kwa wenyewe haupo,isipokuwa akili za watu zinazowaza uchawi hupelekea kitu hicho kuaminika kuwa kipo kumbe si kweli,ni mambo ya kufikirika tu!,hamna lolote.
 
Namaanisha kuwa Uchawi km Uchawi kwa wenyewe haupo,isipokuwa akili za watu zinazowaza uchawi hupelekea kitu hicho kuaminika kuwa kipo kumbe si kweli,ni mambo ya kufikirika tu!,hamna lolote.
na kwanini ukatae imani za watu wengine?
acha wafu wazikane mkuu
 
Uchawi ni jambo lenye utata sana
 
Unasema uchawi haupo halafu unapeleka mbegu kwa padre......we ungejilimia tu freestyle
Baraka ya watu,vitu,n.k.ni kawaida kwa Imani yangu km Mkristo Mkatoliki,nafanya hivyo km ishara ya kumkabidhi Mungu jitihada zangu ili kupitia maombi ya Mtumishi wake niweze kufanikiwa.
 
Unasema uchawi haupo halafu unapeleka mbegu kwa padre......we ungejilimia tu freestyle
Kwa hiyo unataka kusema nini?

Wewe mama yako au babayo hajawahi kukupa 'baraka' unapotaka kufanya Jambo la kukunufaisha?
 
Mkuu,nimesema Uchawi km uchawi haupo,kilichopo ni ile hali ya watu kuamini kuhusu uchawi,namna walivyoziseti akili zao.Uchawi ni kitu cha kufikirika tu ukikiwazia sana lazima kikupelekeshe mpeta mpeta,lkn km huna mawazo kuhusu huo uchawi mbona utapeta sana.
 
Sasa Wachawi mbona huyu Jamaa anawaaibisha namna hii..? Si mumfanyie Jambo huyu ili aje kuwa shuhuda kwa wote!.. fanyeni fanyeni Basi tuone mpo au hampo..[emoji28]
Nawakaribisha sana.
 
Amen.Asante mkuu kwa mchango wako.
 
Sadaka tunatuma wapi? Au comments zitahesabika kama sadaka
Mkuu mimi sipokei sadaka,ninachoweza kukuambia km umewiwa kutoa sadaka,basi chukua sadaka yako wapelekee wahitaji,naamini Mungu atapendezwa na jambo hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…