Uchawa na ustawi wa taifa letu

Night Watch

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
2,014
1,973
Nawasalimu wana jukwaa.
Kwa siku za hivi karibuni hapa nchini Tanzania kumeshamiri au kuzuka mtindo maarufu wa watu kujiita machawa. Vijana hawa shughuli yao kubwa imekuwa kuwasifia watu wakubwa kwa lengo la kujipatia kipato na manufaa kadhaa,cha kusikitisha zaidi vyombo vya habari vimekuwa nyenzo kubwa ya kupalilia swala hili kwa kuwapa nafasi vijana hao kuonyesha uchawa,lakini pia mitandao ya kijamii pia imechangia kwa kiasi kikubwa mtu kujirekodi huku akimsifia mtu fulani kama chawa.
.
.
Swala hili la uchawa ukiliangalia kwa jicho pevu utaona au kugundua kwamba hali hii imepelekea hao wanaojiita machawa kupoteza uwezo wa kufikiri na kuchanganua mambo,jambo hili limekuwa hatari katika ustawi wa jamii yetu na makuzi ya kizazi kijacho.
.
.
Swali ni je sisi kama kizazi cha sasa ni hatua gani tunapaswa kuzifanya ili kizazi kijacho kisije kutumbukia katika hali hii ya uchawa.
 
Back
Top Bottom