Uchapishaji na usambazaji wa vitabu vyenye makosa, Ndalichako asimamisha maafisa wawili

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Joyce Ndalichako amesema hawezi kuomba msamaha kwa vitabu kukosewa ila atawawajibisha waliokosewa, na hapo akawasimamisha mara moja kaimu mkurugenzi wa taasisi ya elimu na kaimu kamishna wa elimu kufuatia uchapishaji na usambazaji wa vitabu vyenye makosa
Ndalichako amesema alipokea taarifa kuhusu vitabu na kitabu cha darasa la 3 cha kiingereza watu waliondika ni aibu na kama watu zaidi ya 9,000 wameondoka kwa kughushi vyeti na hao pia itabidi waondoke

upload_2017-5-16_9-8-44-png.509881
 
Waziri ndio anyethibitisha machapicsho ya vitabu hivyo huu msala haukwepeki lazima awajibike kisheria lakini kabla ya hatua hiyo lazima machapisho hayo yalitoka kwa idhini yake au waziri alimtangulia.
 
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Joyce Ndalichako amesema hawezi kuomba msamaha kwa vitabu kukosewa ila atawawajibisha waliokosewa, na hapo akawasimamisha mara moja kaimu mkurugenzi wa taasisi ya elimu na kaimu kamishna wa elimu kufuatia uchapishaji na usambazaji wa vitabu vyenye makosa
Ndalichako amesema alipokea taarifa kuhusu vitabu na kitabu cha darasa la 3 cha kiingereza watu waliondika ni aibu na kama watu zaidi ya 9,000 wameondoka kwa kughushi vyeti na hao pia itabidi waondoke

Profesa mzima anaonekana kutoelewa maana halisi ya uwajibikaji (accountability).

Kama yaye alitimiza wajibu wake ipasavyo wala asingefikia kupata shinikizo la bunge juu ya utendaji kwenye wizara yake!
 
Vitabu vyenye makosa vipo ving sana siyo shule ya msingi hata sekondary. Kuna vitabu ukivingalia vimekaa kibiashara.
Ndalichako mzembe sana. Miaka yote yupo hapo. Alishindwa kubainisha matatizo mpaka wabainishe wengine?
Hii nchi hata sielewi tunaenda wapi?
 
Hapa Ndalichako namvua vyeo vyote!! Sheria hiyo hapo juu inasema yeye ndiye atakaye idhinisha matumizi ya vitabu vinavyotungwa na kuhakikiwa na TIE, sasa unawezaje kuidhinisha kitu ambacho hujakipitia kujiridhisha na ubora wake!! Hapa housegirl kapika, kaandaa meza na kufunika hotpot mezani halafu mama kamkaribisha mmewe chakula kwa mbwe mbwe zote bila kujiridhisha na chakula kilichotengwa mezani, hotpot zilipofunuliwa kilichokutwa ni aibu tupu kwani tayari housegirl alishapanga kumkomoa mke wa Boss kwa uzembe wa kutomjali mmewe! Nani alaumiwe: Mke wa Boss au Housgirl!?
 
Back
Top Bottom