Prof. Joyce Ndalichako atoa onyo kwa Maafisa Elimu wanaoshiriki katika wizi wa mitihani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,031
2,000
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Joyce Ndalichako amewaonya baadhi ya Maafisa elimu wasio waminifu ambao hushiriki vitendo vya wizi wa mitihani ili kuonekana katika maeneo yao ufaulu upo juu na pindi inapogundulika kuwasingizia wakuu wa shule.

Prof. Ndalichako ametoa onyo hilo Jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa 15 wa wakuu wa shule za Sekondari uliofanyika Jijini hapo kwa siku tatu kwa lengo la kutathmimni changamoto na mafanikio waliyoyapata kwa mwaka mzima katika maeneo yao ya kazi.

Amesema wapo baadhi ya maafisa elimu hushiriki mitendo hivyo viovu kwa lengo la kujionyesha kuwa wanafanya kazi nzuri katika maeneo yao wasijue kwamba wanaliangamiza taifa kwa kuzalisha wataalamu wasiokuwa na uwezo kuwa kutumia elimu yao kwa sababu hawakutumia akili zao kufaulu mitihani.

“Hili swala naona linazidi kuota mizizi kila matokeo yakitangazwa utasikia NECTA imewafutia mitihani wanafunzi sababu wa udanganyifu katika mitihani halafu kuna baadhi ya maeneo hadi maafisa elimu wanahusika halafu wakigundulika wanawaangushia jumba bovu wakuu wa shule hii haikubaliki” amesema Prof. Ndalichako.

Amesema kuna baadhi ya maafisa elimu huwatisha wakuu wa shule ambao hawataki kushiriki katika vitendo hivyo viovu na kuwataka wakuu wa shule ambao waliwahi kutishwa na maafisa elimu wao kwenda kutoa taarifa katika mamlaka husika ili watu hao wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Amesikitishwa na kuona vitendo hivyo vimevuka mipaka na kwenda katika vyuo vya kati akitolea mfano chuo cha VETA mkoani Kagera ambapo taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wanawashikilia mkuu wa chuo na baadhi ya wakufunzi kwa kushiriki vitendo hivyo vya wizi wa mitihani.

“ Vitendo hivi sasa vimevuka hadi kufika vyuo vya kati kule Kagera mkuu wa chuo na walimu wenzake wamekamatwa hivi vitendo havikubaliki kabisa na watu kama hawa hatuwataki katika sekta ya elimu waondoke” amesema.

Aidha ameonya tabia ya baadhi ya maafisa elimu kutotii maagizo ya Wizara ya elimu wakidai kuwa wao wapo chini ya TAMISEMI amesema watu kama hao watachukuliwa hatua kama kawaida kwa sababu yeye ndioi msimamizi wa elimu hapa nchini vinginevyo wakatafute elimu nyingine sio wizara yae.

Mbali na hilo amezitaka shule binafsi kuacha tabia ya kuwanyanyapaa wanafunzi wanaposhuka ufaulu na kuwataka kuhama shule hizo na kutafuta shule nyingine wakati wamekula ada ya wazazi wao na wanafunzi hao hao wanapokwenda shule nyingine hufaulu.

Pia amezitaka shule binafsi kuacha tabia ya kuajili walimu na wafanyakazi wakigeni katika shule zao bila kufuata utaratibu za kupata vibali na kubainisha kuwa watakwenda kufanya uhakiki katika shule hizo na watakao wabaini watachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri Prof. Ndalichako amewataka wakuu hao wa Shule kwenda kusimamia ulinzi na usalama wa maeneo ya shule ikiwamo kudhibiti majanga ya moto ambayo yameibuka kwa wingi katika siku za hivi karibuni kwa mabweni ya wanafunzi kuungua.

“Wakuu wa shule ndio wasimamizi wa kila kitu katika maeneo ya shule siku za hivi karibuni yameibuka maswala ya moto katika mabweni ya wanafunzi kuungua mkasimamie hayo kwa ukaribu sana majanga kama hayo yasijirudie tena” amesema

Awali rais wa chama cha wakuu wa shule za sekondari hapa nchini TAHOSSA mwalimu Frank Mahenge amesema katika mkutano huo wametumia kutathmini utendaji wao wa kazi kwa mwaka unaoisha na wameshirikisha changamoto wanazokutana nazo katika maeneo yao ya kazi sambamba na kuweka mikakati mipya ya kwenda kutekeleza kwa mwaka ujao.
 
LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,355
2,000
kuna shule moja walimu wake hawana mpango mpango kufanya udanganyifu ili waonekane shule yao inafaulisha sana,wao akifaulu hata mmoja kwa akili zake inatosha,hawajali masimango toka ngazo za juu kwa nini hawafanyi udanganyifu wafaulishe wengi wakati shule yao ipo ndani porini kijijini hakuna wa kuwaona 'wakiwasolvia pepa 'wanafunzi
 
LOTH HEMA

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
5,355
2,000
acha tuseme ukweli bila kupepesa macho,mkuu wa shule anafanya mchongo na msimamizi wa mtihani asaidie wanafunzi maswali kadhaa ya kutosha kupata maksi za ufaulu,shule zina siri kuu za kufaulisha
 
kson m

JF-Expert Member
Jan 24, 2014
5,987
2,000
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Joyce Ndalichako amewaonya baadhi ya Maafisa elimu wasio waminifu ambao hushiriki vitendo vya wizi wa mitihani ili kuonekana katika maeneo yao ufaulu upo juu na pindi inapogundulika kuwasingizia wakuu wa shule.

Prof. Ndalichako ametoa onyo hilo Jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa 15 wa wakuu wa shule za Sekondari uliofanyika Jijini hapo kwa siku tatu kwa lengo la kutathmimni changamoto na mafanikio waliyoyapata kwa mwaka mzima katika maeneo yao ya kazi.

Amesema wapo baadhi ya maafisa elimu hushiriki mitendo hivyo viovu kwa lengo la kujionyesha kuwa wanafanya kazi nzuri katika maeneo yao wasijue kwamba wanaliangamiza taifa kwa kuzalisha wataalamu wasiokuwa na uwezo kuwa kutumia elimu yao kwa sababu hawakutumia akili zao kufaulu mitihani.

“Hili swala naona linazidi kuota mizizi kila matokeo yakitangazwa utasikia NECTA imewafutia mitihani wanafunzi sababu wa udanganyifu katika mitihani halafu kuna baadhi ya maeneo hadi maafisa elimu wanahusika halafu wakigundulika wanawaangushia jumba bovu wakuu wa shule hii haikubaliki” amesema Prof. Ndalichako.

Amesema kuna baadhi ya maafisa elimu huwatisha wakuu wa shule ambao hawataki kushiriki katika vitendo hivyo viovu na kuwataka wakuu wa shule ambao waliwahi kutishwa na maafisa elimu wao kwenda kutoa taarifa katika mamlaka husika ili watu hao wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Amesikitishwa na kuona vitendo hivyo vimevuka mipaka na kwenda katika vyuo vya kati akitolea mfano chuo cha VETA mkoani Kagera ambapo taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wanawashikilia mkuu wa chuo na baadhi ya wakufunzi kwa kushiriki vitendo hivyo vya wizi wa mitihani.

“ Vitendo hivi sasa vimevuka hadi kufika vyuo vya kati kule Kagera mkuu wa chuo na walimu wenzake wamekamatwa hivi vitendo havikubaliki kabisa na watu kama hawa hatuwataki katika sekta ya elimu waondoke” amesema.

Aidha ameonya tabia ya baadhi ya maafisa elimu kutotii maagizo ya Wizara ya elimu wakidai kuwa wao wapo chini ya TAMISEMI amesema watu kama hao watachukuliwa hatua kama kawaida kwa sababu yeye ndioi msimamizi wa elimu hapa nchini vinginevyo wakatafute elimu nyingine sio wizara yae.

Mbali na hilo amezitaka shule binafsi kuacha tabia ya kuwanyanyapaa wanafunzi wanaposhuka ufaulu na kuwataka kuhama shule hizo na kutafuta shule nyingine wakati wamekula ada ya wazazi wao na wanafunzi hao hao wanapokwenda shule nyingine hufaulu.

Pia amezitaka shule binafsi kuacha tabia ya kuajili walimu na wafanyakazi wakigeni katika shule zao bila kufuata utaratibu za kupata vibali na kubainisha kuwa watakwenda kufanya uhakiki katika shule hizo na watakao wabaini watachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri Prof. Ndalichako amewataka wakuu hao wa Shule kwenda kusimamia ulinzi na usalama wa maeneo ya shule ikiwamo kudhibiti majanga ya moto ambayo yameibuka kwa wingi katika siku za hivi karibuni kwa mabweni ya wanafunzi kuungua.

“Wakuu wa shule ndio wasimamizi wa kila kitu katika maeneo ya shule siku za hivi karibuni yameibuka maswala ya moto katika mabweni ya wanafunzi kuungua mkasimamie hayo kwa ukaribu sana majanga kama hayo yasijirudie tena” amesema

Awali rais wa chama cha wakuu wa shule za sekondari hapa nchini TAHOSSA mwalimu Frank Mahenge amesema katika mkutano huo wametumia kutathmini utendaji wao wa kazi kwa mwaka unaoisha na wameshirikisha changamoto wanazokutana nazo katika maeneo yao ya kazi sambamba na kuweka mikakati mipya ya kwenda kutekeleza kwa mwaka ujao.
Aanze na matokeo ya darasa la saba 2020 aone wanaoingia kidato cha kwanza kama walifaulu au la ndipo atakapolia kilio kikuuuu !!!!!
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,604
2,000
Usitoe onyo, chukua hatua kwani kuna kipi wasichokijua hao wavujisha Mitihani ? Fanya kazi Muheshimiwa Waziri na siyo blah blah, binafsi ningependa kusikia mtu xyz kakamtwa na kushitakiwa kwa kosa la kuvujisha Mitihani, ...
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,709
2,000
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof. Joyce Ndalichako amewaonya baadhi ya Maafisa elimu wasio waminifu ambao hushiriki vitendo vya wizi wa mitihani ili kuonekana katika maeneo yao ufaulu upo juu na pindi inapogundulika kuwasingizia wakuu wa shule.

Prof. Ndalichako ametoa onyo hilo Jijini Dodoma wakati akifunga mkutano wa 15 wa wakuu wa shule za Sekondari uliofanyika Jijini hapo kwa siku tatu kwa lengo la kutathmimni changamoto na mafanikio waliyoyapata kwa mwaka mzima katika maeneo yao ya kazi.

Amesema wapo baadhi ya maafisa elimu hushiriki mitendo hivyo viovu kwa lengo la kujionyesha kuwa wanafanya kazi nzuri katika maeneo yao wasijue kwamba wanaliangamiza taifa kwa kuzalisha wataalamu wasiokuwa na uwezo kuwa kutumia elimu yao kwa sababu hawakutumia akili zao kufaulu mitihani.

“Hili swala naona linazidi kuota mizizi kila matokeo yakitangazwa utasikia NECTA imewafutia mitihani wanafunzi sababu wa udanganyifu katika mitihani halafu kuna baadhi ya maeneo hadi maafisa elimu wanahusika halafu wakigundulika wanawaangushia jumba bovu wakuu wa shule hii haikubaliki” amesema Prof. Ndalichako.

Amesema kuna baadhi ya maafisa elimu huwatisha wakuu wa shule ambao hawataki kushiriki katika vitendo hivyo viovu na kuwataka wakuu wa shule ambao waliwahi kutishwa na maafisa elimu wao kwenda kutoa taarifa katika mamlaka husika ili watu hao wachukuliwe hatua kali za kinidhamu.

Amesikitishwa na kuona vitendo hivyo vimevuka mipaka na kwenda katika vyuo vya kati akitolea mfano chuo cha VETA mkoani Kagera ambapo taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wanawashikilia mkuu wa chuo na baadhi ya wakufunzi kwa kushiriki vitendo hivyo vya wizi wa mitihani.

“ Vitendo hivi sasa vimevuka hadi kufika vyuo vya kati kule Kagera mkuu wa chuo na walimu wenzake wamekamatwa hivi vitendo havikubaliki kabisa na watu kama hawa hatuwataki katika sekta ya elimu waondoke” amesema.

Aidha ameonya tabia ya baadhi ya maafisa elimu kutotii maagizo ya Wizara ya elimu wakidai kuwa wao wapo chini ya TAMISEMI amesema watu kama hao watachukuliwa hatua kama kawaida kwa sababu yeye ndioi msimamizi wa elimu hapa nchini vinginevyo wakatafute elimu nyingine sio wizara yae.

Mbali na hilo amezitaka shule binafsi kuacha tabia ya kuwanyanyapaa wanafunzi wanaposhuka ufaulu na kuwataka kuhama shule hizo na kutafuta shule nyingine wakati wamekula ada ya wazazi wao na wanafunzi hao hao wanapokwenda shule nyingine hufaulu.

Pia amezitaka shule binafsi kuacha tabia ya kuajili walimu na wafanyakazi wakigeni katika shule zao bila kufuata utaratibu za kupata vibali na kubainisha kuwa watakwenda kufanya uhakiki katika shule hizo na watakao wabaini watachukuliwa hatua za kisheria.

Waziri Prof. Ndalichako amewataka wakuu hao wa Shule kwenda kusimamia ulinzi na usalama wa maeneo ya shule ikiwamo kudhibiti majanga ya moto ambayo yameibuka kwa wingi katika siku za hivi karibuni kwa mabweni ya wanafunzi kuungua.

“Wakuu wa shule ndio wasimamizi wa kila kitu katika maeneo ya shule siku za hivi karibuni yameibuka maswala ya moto katika mabweni ya wanafunzi kuungua mkasimamie hayo kwa ukaribu sana majanga kama hayo yasijirudie tena” amesema

Awali rais wa chama cha wakuu wa shule za sekondari hapa nchini TAHOSSA mwalimu Frank Mahenge amesema katika mkutano huo wametumia kutathmini utendaji wao wa kazi kwa mwaka unaoisha na wameshirikisha changamoto wanazokutana nazo katika maeneo yao ya kazi sambamba na kuweka mikakati mipya ya kwenda kutekeleza kwa mwaka ujao.
Ukiwa Baraza la mitihani ukumbuki yaliyokukuta huko?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom