Uchambuzi: Nia ya msajili wa vyama vya siasa kufuta usajili wa kudumu wa ACT - Wazalendo

Makombeni10

Member
Jul 29, 2015
34
64
*KUFUTIWA USAJILI WA KUDUMU ACT- WAZALENDO*

SEHEMU YA KWANZA

NIA YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUFUTA USAJILI WA KUDUMU WA ACT-WAZALENDO (UCHAMBUZI)
1. Utangulizi
Kabla ya kutoa uchambuzi juu ya nia ya msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama cha ACT-Wazalendo, akizingatia sheria ya vyama vya siasa iliyofanyiwa marekebisho (The Political Parties Act Cap 258 RE 2019), muhimu kutoa maelezo mafupi kuhusu mchakato wa marekebisho hayo yaliyofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 29 Januari, 2019, kuwa sheria baada ya kutiwa saini na Rais John Pombe Joseph Magufuli tarehe 13 Februari, 2019 na kuanza kutumika baada ya kutangazwa katika Gazette la serikali Na. 8 Vol. 100 la tarehe 22 Februari, 2019.

Kabla ya serikali ya awamu ya tano kupeleka muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa mwezi Oktoba, 2018, kulikuwa na hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania (Mihayo, J) iliyoweka bayana mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa. Hukumu hiyo katika shauri la Emmanuel Nyenyemela and Another versus Registrar of Political Parties, Civil Case No.6 of 2003 iliweka bayana kuwa sheria ya vyama vya siasa (The Political Parties Act Cap 258 RE 2002) ilikuwa haimpi mamlaka msajili wa vyama vya siasa kubariki au kubatilisha maaamuzi ya vikao vya vyama vya siasa. Kwa tafsiri nyingine, msajili chini ya sheria hiyo hakuwa na mamlaka kuingilia mambo ya ndani ya kiutawala ya vyama vya siasa. Hukumu ilisema;

“In the same vein, I do not see anywhere in the Political Parties Act where the Registrar has power to bless or condemn meetings of political parties or decisions that they make.”

Kwa tafsiri isiyo rasmi Mahakama Kuu (kupitia Jaji Mihayo) ilisema;
“Katika maana ile ile, sioni mahali popote katika sheria ya Vyama vya siasa, ambapo Msajili ana mamlaka ya kubariki au kubatilisha mikutano ya vyama vya siasa au maamuzi wayafanyayo.”

Kwa ujeuri na bila kujali tafsiri hiyo ya mahakama kuu, msajili wa vyama vya siasa aliendelea kufanya maamuzi tata yanayokinzana na hukumu hiyo; hususan pale alipobatilisha maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CUF-Chama cha Wananchi na kumtambua Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kuwa mwenyekiti wa Taifa wakati akifahamu fika kuwa alikwisha jiuzulu, kuthibitishwa na mkutano mkuu wa chama hicho na hatimaye kufukuzwa uanachama. Jambo hilo lilisababisha kesi nyingi mahakamani dhidi ya msajili wa vyama vya siasa, miongoni mwake kesi Na. 23 ya mwaka 2016 iliyohoji mamlaka ya msajili kuingilia maamuzi ya vikao vya Chama. Aidha mwishoni mwa mwaka 2018, msajili wa vyama vya siasa alisimamia mkutano mkuu feki wilayani Mvomero, uliofanya mapinduzi ya uongozi halali wa chama cha Democratic Party (DP) na kufunguliwa kesi mahakama kuu ya Tanzania. Ili kuthibiti hali hiyo na kutekeleza azma ya Rais wa serikali ya awamu ya tano ya kudhibiti na kuua vyama vya upinzani; kwa mujibu wa hotuba yake kwa wana CCM mkoani Singida tarehe 5 Februari, 2016, ndipo serikali ikaja na marekebisho hayo ya sheria. Marekebisho yalilenga kumpa mamlaka ya udhibiti msajili wa vyama vya siasa na kimsingi kujinaisha siasa nchini. Waziri mwenye dhamana ya Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa; ambaye ni ndiye Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, aliliambia Bunge kuwa lengo la Muswada ni “kutatua changamoto mbali mbali zilizojitokeza katika utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa.” Kwa lugha ya Kiingereza Waziri Mkuu alisema “with the aim of removing legal challenges under the Act for better implementation of the Act.”

Marekebisho yaliyopelekwa Bungeni kutatua changamoto, yalipendekeza vifungu vipya kumi na nane (18) vya adhabu; zikiwemo za faini hadi milioni hamsini (50) na vifungo vya hadi miaka ishirini (20) jela; ambapo, vifungu sita (6) vilitoa adhabu ya kufuta usajili wa kudumu wa vyama vya siasa. Haiyukimniki kuwa changamoto katika sheria ya vyama vya siasa ilikuwa ni adhabu. Pamoja na kupunguza vifungu kadhaa vya adhabu baada ya malalamiko na upinzani mkubwa kutoka kwa vyama vya upinzani na wadau kadhaa wa haki za binadamu, bado sheria imebaki na vifungu vitatu vyenye adhabu ya kufuta chama cha siasa chenye usajili wa kudumu [vifungu vya 8E(3), 19(1) na 21D(2)].

Kifungu cha 8E(3) kinampa mamlaka msajili kukifuta chama cha siasa kilichoanzisha kikundi cha ulinzi;

8E. Political parties not to form security group
“(3) A political party which contravenes the requirement of this section, shall be deregistered and every leader or member of the party concerned shall be liable on conviction imprisonment for a term not less than five years but not exceeding twenty years or both.”

Kifungu cha 19(1) kinampa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama kilichokiuka matakwa ya sheria au kilichopoteza sifa za usajili chini ya sheria ya vyama vya siasa;

19. Power of Registrar to suspend or cancel registration
“(1) Subject to subsection (2) the Registrar may suspend or cancel the registration of any political party which has contravened any of the provisions of this Act or which has otherwise ceased to qualify for registration under this Act.”

Kifungu cha 21D(2) kinampa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama cha siasa kilichokiuka takwa lolote la sheria ya vyama vya siasa ambalo halikuwekewa adhabu makhsusi;

21D. Offences and penalties
“(2) Any political party which contravenes any Provision of this Act to which no specific penalty is prescribed, shall be liable to a fine of not less than ten million shillings and not exceeding fifty million shillings or to suspension or to deregistration.”

Hata hivyo serikali ilijisahaulisha kuwa licha ya vifungu hivyo kumpa mamlaka msajili ya kutekeleza azma hiyo ya Rais wa serikali ya awamu ya tano ya kuuwa upinzani nchini na kumpa kinga msajili wa vyama ya kutoshitakiwa, bado kuna suala la haki ya kikatiba ya kushiriki katika shughuli za kisiasa (freedom of association) ambayo Mahakama Kuu ilikwisha litolea maamuzi kupitia hukumu katika shauri la Chama cha Democratic Party (DP); The Chairman of Democratic Party versus The Registrar of Political Parties and The Attorney General, Miscellaneous Civil Application No. 42 of 1993. Hukumu hiyo (Samatta, JK kama alivyokuwa) iliweka wazi kuwa mamlaka ya chombo chochote kilichoanzishwa kwa sheria lazima yatokane na sheria iliyokianzisha na zaidi sana katiba ya nchi. [msisitizo umewekwa]

“It is a well established principal of law that a statute must be construed in the light of the general law of the land, and in particular in the light of the Constitution of the country. Section 20(1) of the Constitution of the United Republic guarantees the right of the freedom of association. This is very important right under the kind of political system which this country has now adopted. Any curtailment of the enjoyment of that right must be reasonable and necessary.”[msisitizo umewekwa]

Hukumu hiyo ni msingi na sababu tosha ya wadau kuipeleka sheria ya vyama vya siasa iliyorekebishwa (The Political Parties Act Cap 258 RE 2019) mahakamani ili kulinda haki ya kikatiba ya uhuru wa wananchi kushiriki katika shughuli za kisiasa iliyomo kwenye ibara ya 20(1).
Iko dhana potofu miongoni mwa wahafidhina na viongozi wa serikali kuwa mambo ya kisiasa yaamuliwe kisiasa. Dhana hii inalenga kuwezesha maamuzi ya ovyo ovyo kwa misingi ya kiitikadi na hususan pale kunapokuwepo na kile kinachoitwa “amri kutoka juu.” Dhana hii inaweza kuangaliwa kwa kujifunza na kukopa uzoefu wa nchi nyingine barani Afrika. Mahakama Kuu ya Namibia (Parker, AJ) katika shauri la Amupanda versus Swapo Party of Namibia (A 215/2015)[2016] NAHCMD 126 (22 April, 2016) ilibainsha wazi kuwa katika suala la haki na usawa hakuna siasa. Mahakama ilisema ifuatavyo;
“In Namibia no person is entitled to “disregard with impunity” an order of the court. In our system every order must be obeyed unless it has been set aside by a competent court. And more important; in Namibia issues concerning justice and fairness are not seen as “political matters”. As I have said more than once, the applicants in the instant case have approached the seat of judgement of the court in order to enforce their contractual right on the basis of natural justice, including fairness and justice. There is nothing political about that.”[msisitizo umewekwa]
 
Back
Top Bottom