ichumu lya
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 2,605
- 2,729
Mimepitia na kufanya uchambuzi katika rasimu ya mtaala wa elimu iliyotangazwa na Waziri wa Elimu inahitaji marekebisho kabla ya kupitishwa rasmi na kuwa mtaala unaofaa. Ni muhimu kuondoa kabisa mambo ya dini yanayoweza kusababisha machafuko. Nakumbuka mwaka 2014 tulipopendekeza kuondolewa kwa mambo ya dini, lakini sasa wamerudisha kijanja. Nani yuko nyuma ya dini?
Kuna vitu vingi tulivyokataa, lakini wanavilazimisha:
1. Kuwekwa kwa swala la dini kwenye mtaala huu litasababisha malumbano au hata vurugu. Nchi hii haiongozwi kwa misingi ya dini, ingawa watu wake wana dini na wengine hawana. Ukisoma kwa makini rasimu hii, unaona kuwa nchi inaingia mkenge wa dini: Elimu ya biashara wameipa umuhimu wa kitaalamu, elimu ya dini ya Kiislamu, lakini wakristo na wasio na dini wameachwa wapi? Je, mtaala huu umechukuliwa kutoka Zanzibar na kuhamishiwa Tanganyika? Kuna maswali mengi sana bado tunajiuliza, je, lengo lao ni kuleta mfarakano na watafika wapi na ligi wanayotaka kuanzisha?
2. Mtaala huu unakinzana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 🙄.
13.-(1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
(2) Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake.
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka.
Usawa wa binadamu Sheria ya 1984 na. 15 ib. 6 Usawa mbele ya Sheria Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6 Sheria Na. 4 ya 1992 ib. 8 Sheria ya 2000 na. 3 ib. 5 Sheria ya 1994 na. 7. Fungu la 8[1], [k].
Ukisoma vifungu hivi unaona Waziri anavyoingiza nchi kwenye mgogoro wa kikatiba na mimi kutokea hapo niko tayari kupinga vifungu hivi mahakamani kuzuia Mtaala huu wenye ubaguzi kupishwa. Tayari nimemwandikia Waziri e-mail nikimkumbusha kwenye maoni tulivyopinga mambo ya dini kuingizwa kwenye mtaala wa Elimu, na hii ndiyo sababu kuu iliyomfanya Rais Magufuli kuukataa. Najua kuna lengo ovu, ila tutashughulika nalo kisheria.
2. CHAKULA mashuleni tulisema jukumu la chakula ni jukumu la serikali, sio jukumu la wazazi. Kwakuwa Elimu bure ni pamoja na chakula, lakini wao wameliacha hewani bila kuonyesha mwenye wajibu. Hili tukiliacha hivi, litafungua mlango kwa serikali kuwalazimisha wazazi kupeleka chakula shuleni kama ilivyo leo. Tunataka swala la Elimu libaki mikononi mwa Serikali, maana wakati wanaomba kura walinadi elimu bure, na hawawezi kulikwepa. Na kwakuwa sera ya CCM ndiyo inayotekelezwa, ni vyema wakahakikisha watoto wetu wanapata chakula shuleni, ama watwambie kwamba wameshindwa. Tufanye maamuzi kama wenye nchi, apo nasimama na kifungu hiki 🙄.
(a) Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii.
(b) Lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi
(C) Serikali itawajibika kwa wananchi;
Niwakumbushe kwamba serikali inawajibika kwa wananchi sio wananchi kuwajibika kwa serikali kama ilivyo sasa.
3. Tulipendekeza elimu ya ufundi aina zote ifundishwe kuanzia darasa la tatu ili kupata utaalamu wakiwa na uwezo mzuri wa kufundishika na apo ndipo tunaweza kupata matokeo mazuri ya watoto wetu kujua nini wanataka kufanya mbeleni, tutapata mafundi wa vyombo mbalimbali tutapata wataalamu na wahandisi lakini pia tutaondoa utegemezi wa ajira unaoitesa dunia.