Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Katika taifa ambalo linahitaji kufanya maamuzi magumu na sahihi kuhusu mustakabali wake, hakuna eneo nyeti kama elimu. Elimu ni injini, ni mapafu, ni moyo unaosukuma damu ya maendeleo. Taifa lisilo na mfumo madhubuti wa elimu ni sawa na kutembea gizani bila dira.
Ndiyo maana uteuzi wa viongozi wa wizara hii unapaswa kuwa wa makini kupita maamuzi mengine yote ya kisiasa. Lakini uteuzi wa Wanu Hafidh Ameir kuwa Naibu Waziri wa Elimu umeibua maswali mazito—maswali ambayo hatuwezi kuyakwepa kama kweli tunataka kujenga Tanzania inayojitegemea.
Kwanza kabisa, mjadala huu si wa chuki binafsi, si wa kubeza mtu kama mtu. Ni mjadala wa uwezo, misuli ya kitaaluma, rekodi ya kazi, na uhalisia wa kile ambacho wizara ya elimu inahitaji katika karne hii ya sayansi na teknolojia. Wasifu wa Wanu ni mwepesi sana na hauoneshi uzito unaohitajika kuongoza sekta inayopaswa kubeba ndoto za vijana milioni kadhaa wanaoamini kuwa elimu ndiyo tiketi yao ya kutoka kwenye umasikini na kufika walipo Wachina, Wajapan au hata jirani zetu wanaosonga mbele kwa kasi.
Uteuzi wake unaonekana kama ishara nyingine kuwa Tanzania bado haijaamua kuwa serious kuhusu elimu. Ni kama tunacheza na maisha ya vizazi vijavyo. Ni kama tunasema: "haituhusu, muda utapita tu, nchi itaendelea tu kupumua kwa mazoea". Lakini ukweli ni kwamba nchi haiendelei kwa mazoea; inaendelea kwa maamuzi sahihi.
Mwaka 1956, miaka zaidi ya 70 iliyopita, Uchina ilifanya uamuzi mkubwa wa kitaifa—kuiweka elimu ya sayansi na teknolojia kuwa kipaumbele cha taifa. Haikuwa nchi tajiri kivile, haikuwa na miundombinu mikubwa, haikuwa na viwanda vya kuvutia. Lakini viongozi wao walijua kuwa maendeleo hayaji kwa bahati, bali kwa kupanda mbegu sahihi—na mbegu hiyo ilikuwa elimu. Leo, tunawaona Wachina wakitamba duniani katika uhandisi, teknolojia, nishati, viwanda, na hata katika uchumi wa kimataifa. Siyo kwa sababu “wamejaliwa”, bali kwa sababu waliamua kuwa serious.
Tanzania, leo, mwaka 2025, bado tunapamba moto. Bado tunafanya utani na mizaha huku kina Lucas Mwashambwa wakipiga makofi. Na tunaonesha utani huo waziwazi pale tunapowakabidhi wasio na uzito mkubwa majukumu ya kujenga kizazi cha kesho.
Wizara hii leo inahitaji mtu mwenye dira ya kitaaluma, aliyelelewa katika mazingira ya kitaaluma, aliyeishi na kufikiri kama msomi, aliyeelewa mfumo wa elimu si kihisia, bali kiuchambuzi na kiutafiti. Elimu sio nafasi ya mazoea, sio sehemu ya kujaribia majina mapya, sio sehemu ya kuficha udhaifu wa kisiasa au kulipa fadhila. Kama kuna wizara inayopaswa kuongozwa na watu wenye CV zenye mizizi mikubwa, ni wizara ya elimu.
Lakini CV ya Wanu—pamoja na kwamba inaonesha safari ya kisiasa—haioneshi uwezo, rekodi, au mchango wa kitaalam unaolingana na ukubwa wa jukumu la elimu ya taifa. Hili ndilo linaloumiza wengi. Ni kama tunafanya mzaha na mustakabali wa Taifa.
Tatizo si kwamba Wanu ni mtoto wa nani au kuwa ni mtoto wa Rais. Tatizo ni kwamba hatuoni uwezo unaolingana na nafasi. Hofu sio kwamba ametoka familia fulani. Hofu ni kwamba CV yake haiakisi mtu anayeweza kubadili mwelekeo wa elimu Tanzania; mtu anayeweza kusimama kwenye majukwaa ya kimataifa na kutetea mageuzi ya elimu; mtu anayeweza kuongoza mjadala wa kitaaluma bila kuyumba; mtu anayeweza kufikiria mbali.
Hii ndiyo sababu uteuzi wake unawasukuma Watanzania wengi kuamini: labda hatujui tunachotaka kama Taifa.
Je, tuna mpango wa kwenda sambamba na mapinduzi ya AI, Roboti, uchumi wa kidigitali, na ulimwengu wa sayansi?
Je, tunataka kuwa sehemu ya mataifa yanayounda teknolojia au tunataka kubaki mashabiki wa teknolojia ya wengine?
Haiwezekani tukafikia hayo ikiwa tunawapa watu wasio na rekodi za kitaaluma nafasi ya kusimamia sekta muhimu kama elimu.
China ilipiga hatua kwa sababu walijua wanachotaka. Walisema: “Elimu kwanza.”
Tanzania leo inasema nini?
Kwa uteuzi kama huu, inaonekana tunaendelea kusema: “Tutakuja baadaye. Kwa sasa tusubiri bahati.”
Lakini dunia ya leo haina nafasi kwa nchi za kusubiri bahati. Bahati wanayo watu serious.
Na kama hatutaamua leo, basi tutaendelea tu kuwa watazamaji—wabeba uchungu—mashabiki wa mafanikio ya wengine.
Kwa kifupi, uteuzi wa Wanu Hafidh Ameir kama Naibu Waziri wa Elimu sio tu kosa la kimkakati, bali ni dalili ya ugonjwa mkubwa: kukosa dira, kukosa uamuzi mgumu, na kukosa seriousness katika eneo ambalo ndilo ufunguo wa maendeleo ya nchi.
Kama taifa, tunastahili zaidi. Na watoto wetu wanastahili zaidi. Mama ni Rais, Mtoto ni waziri na Mkwe ni waziri bado Baba naye atapewa uwaziri mwisho wa siku bunge lote linakuwa ni ukoo.