Tumbiliwaulaya
JF-Expert Member
- Nov 22, 2020
- 280
- 435
Kitabu cha Mkapa kinaeleza mambo mengi sana ikiwemo jinsi CCM inachota pesa za umma kufanyia shughuri za chama, mwenda zake ndio alikizindua unakumbuka?Hii inafanana sana na report ya CAG kwa Samia,
Hii chapter imeandikwa lini? Je angeisema iwapo Mwendazake angekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa hicho kitabu?
NAUUUUMIIIA SANA Nikiona watu waliofanya vitu vikubwa nchi hii kimya kimya wakiongelewa vibaya just because they didn't SHOUT SHOUT IN THE PUBLIC OR USE THE MEDIA OR UNNECESSARY PRESS CONFERENCE NATAMANI NINGELAANI WOTE WANAOWAONGELEA VIONGOZI FLANI FLANI VIBAYA WAKATI MAMBO YALIKUWA YAKIENDA VIZURI AAAAAAH.Una lako lingine linalokufanya umtukane lakini si kwa uongozi wake,mzee mwinyi amepokea nchi hii ikiwa kwenye hali mbaya sana lakini kwa jitihada zake alifanya maisha ya watu wengi kuwa na unafuu japo kulikuwa na kasoro hizi na zile ambazo zilikuja kurekebishwa na waliomfuata kwa kiasi walichoweza.
Yeye ndiye aliyefanya na EPA yakeKitabu cha Mkapa kinaeleza mambo mengi sana ikiwemo jinsi CCM inachota pesa za umma kufanyia shughuri za chama, mwenda zake ndio alikizindua unakumbuka?
🤣 aliyemnanga hapo ni yuleyule aliyemsifia sana kuwa amefanya makubwa sana ambayo yeye hakuweza kuyafanya kwa miaka 10Mzee asingeila Idi ya Mwaka huu
Mnaokisoma mniangalizie kama Mzee Ruksa amegusia chavda maana Kwa wale wahenga wenzangu Kwa wakati huo ukimtaja Mzee ungedhani ni replica ya chavda .Hiki kitabu naona kimejaa malalamiko tupu na mipasho
Kama lile lisukuma lililojenga uwanja wa ndege kwao, hivi sasa unatumika kuanika nafakaNAUUUUMIIIA SANA Nikiona watu waliofanya vitu vikubwa nchi hii kimya kimya wakiongelewa vibaya just because they didn't SHOUT SHOUT IN THE PUBLIC OR USE THE MEDIA OR UNNECESSARY PRESS CONFERENCE NATAMANI NINGELAANI WOTE WANAOWAONGELEA VIONGOZI FLANI FLANI VIBAYA WAKATI MAMBO YALIKUWA YAKIENDA VIZURI AAAAAAH.
Hii sehemu ilichomekewa baada ya mwendazake kuzikwaHii inafanana sana na report ya CAG kwa Samia.
Hii chapter imeandikwa lini? Je, angeisema iwapo Mwendazake angekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa hicho kitabu?
Hivi vitabu kumbe vina madiniKitabu cha Mkapa kinaeleza mambo mengi sana ikiwemo jinsi CCM inachota pesa za umma kufanyia shughuri za chama, mwenda zake ndio alikizindua unakumbuka?
Huyu mwendazake alikuwa anawananga watangulizi wake mpaka akasema watulie,wasiwashwewashweUtabishana vipi na mtu aliyekushika mkono na kukupa Urais mbele ya Wababe wengi kama akina Msuya
Hii sehemu ilichomekewa baada ya mwendazake kuzikwa
Sasa kwa nini hakumshauri mwendazake jiwe kuacha kuwasema vibaya majikwaani viongozi waliostaafu na kila siku kazi yake ilikuwa kusema nchi imeliwa sana wengine hawajafanya anayofanya yeye?
RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Nwinyi, amebainisha kuwa wakati wa uongozi wake, aliepuka kubishana hadharani
na mtangulizi wake, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, akiwaonya viongozi wa sasa kujaribu kupata uhalali wa wanayoyafanya
kwa kutupia lawama viongozi waliopita.
Katika kitabu chake cha 'Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu', Mwinyi anasema aliona ilikuwa muhimu kwake kuepuka kubishana na Mwalimu Nyerere hadharani wala kukosoa uamuzi na yote yaliyofanyika wakati wa uongozi wake. "Ipo hulka ya kibinadamu ya viongozi wapya kujaribu kupata uhalali wa wanayoyafanya kwa kutupa kila aina ya lawama kwa viongozi waliopita.
Hayo, kwa maoni yangu ni makosa makubwa. "Hakuna kitu rahisi kama kukosoa wengine, lakini wananchi hawachagui kiongozi ili akaorodheshe lawama. Ukichaguliwa na wenzako kuwaongoza unakuwa umepewa dhamana kubwa kupeleka taifa mbele. "Wananchi wanataka kuona matokeo chanya ya unachokifanya wewe uliye na serikali kwa wakati huo, wakitambua kuwa kila awamu ya uongozi ina nafasi yake na inachokifanya ni sehemu ya mradi usioisha wa ujenzi wa nchi na kutumikia wananchi," anasihi.
Mwinyi anafafanua kuwa mageuzi mengi yaliyofanyika wakati wa awamu yake hayakuwa ya kutafuta umaarufu, bali kuwaondolea wananchi adha mbalimbali. "Hatukuandika waraka, hatukubuni itikadi mpya na wala hatukutumia majukwaa kujinasibu. Mengi tuliyafanya kimya kimya, kwa ujasiri lakini na hekima pia. "Na siku zote nilijitahidi kupata maoni na baraka za chama na kusikiliza
na kupokea ushauri kwa dhati kabisa na kuuzingatia, si kutimiza wajibu tu.
"Kutoka kwa Mwalimu niliimarishwa hulka yangu ya kusikiliza kwa makini maoni na ushauri wa wengine kabla ya kufanya uamuzi na kuutekeleza. Na baada ya kuelewana na wenzangu tulisambaa nchi nzima kuwafahamisha wananchi," anasema. Mwinyi anabainisha kikwazo kikubwa kilichomkumba wakati wa kufanya mageuzi hayo kilitokana na kundi analiloliita la uhafidhina ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wenzake walioona vigumu kukubali haja na hoja ya mabadiliko, hasa pale ambapo hawakuwa na
uhakika na msimamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu mageuzi.
Katika kitabu chake hicho, Mwinyi pia anabainisha namna hali ya uchumi wa nchi ilivyokuwa mbaya wakati anakadhibiwa kijiti huku akisifu mchango wa Mwalimu Nyerere katika kurekebisha hali hiyo. Mwinyi anaweka wazi kuwa hata shinikizo IMF na Benki ya Dunia (WB) kwa Tanzania kukubaliana na masharti yao kama nchi inataka fedha (misaada na mikopo) kutoka kwao na wahisani wengine kutoka nchi za Magharibi, lilitatuliwa kwa ushauri wa Mwalimu Nyerere.
Anafafanua kuwa Mwalimu Nyerere hakukubaliana na baadhi ya masharti hayo na aliweka msimamo mkali na hivyo makubaliano hayakufikiwa mpaka anaondoka madarakani. Katika kutatua suala hilo, Mwinyi anarejea ushauri wa Mwalimu Nyerere akimnukuu: "Tazameni, pesa bado tunazihitaji ili tukwamue uchumi wetu uende mbele. Hali ni mbaya kweli. Maadamu mimi nimeng'atuka, sikserikalini, huu ndiyo wakati mzuri wewe Sheikh Ali na timu yako mkamilishe mazungumzo hayo na ninaamini yatakwenda vizuri maana
wakubwa hao wanajua kuwa yule mkorofi keshaondoka".
Mwinyi anasema ataendelea kumshukuru Mwalimu kwa uamuzi wake wa kuitisha kikao cha Kamati Kuu ya CCM (kilifanyika Zanzibar) na kutoa kauli ile mbele ya Kamati Kuu na hivyo kumpa rukhsa ya kuendelea na kazi hiyo ya kuimarisha uchumi wa nchi.
Chanzo: Nipashe
Samia unamsingizia....report ya CAG haikumtaja kiongozi aliyepita.Hii inafanana sana na report ya CAG kwa Samia.
Hii chapter imeandikwa lini? Je, angeisema iwapo Mwendazake angekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa hicho kitabu?
Labda hujaelewa. report ya CAG kwa Mwendazake ilikuwa na para zingine mfukoni mwa CAG ndiyo hiyo ikasomwa kwa SamiaSamia unamsingizia....report ya CAG haikumtaja kiongozi aliyepita.
Nimekuelewa mkuu.Tatizo npo pub😂Labda hujaelewa. report ya CAG kwa Mwendazake ilikuwa na para zingine mfukoni mwa CAG ndiyo hiyo ikasomwa kwa Samia