Uchambuzi kitabu cha Mwinyi: Niliepuka kubishana, kumkosoa Nyerere hadharani

Tumbiliwaulaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2020
276
500
mwinyi aly.jpg

RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Nwinyi, amebainisha kuwa wakati wa uongozi wake, aliepuka kubishana hadharani
na mtangulizi wake, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, akiwaonya viongozi wa sasa kujaribu kupata uhalali wa wanayoyafanya
kwa kutupia lawama viongozi waliopita.

Katika kitabu chake cha 'Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu', Mwinyi anasema aliona ilikuwa muhimu kwake kuepuka kubishana na Mwalimu Nyerere hadharani wala kukosoa uamuzi na yote yaliyofanyika wakati wa uongozi wake. "Ipo hulka ya kibinadamu ya viongozi wapya kujaribu kupata uhalali wa wanayoyafanya kwa kutupa kila aina ya lawama kwa viongozi waliopita.

Hayo, kwa maoni yangu ni makosa makubwa. "Hakuna kitu rahisi kama kukosoa wengine, lakini wananchi hawachagui kiongozi ili akaorodheshe lawama. Ukichaguliwa na wenzako kuwaongoza unakuwa umepewa dhamana kubwa kupeleka taifa mbele. "Wananchi wanataka kuona matokeo chanya ya unachokifanya wewe uliye na serikali kwa wakati huo, wakitambua kuwa kila awamu ya uongozi ina nafasi yake na inachokifanya ni sehemu ya mradi usioisha wa ujenzi wa nchi na kutumikia wananchi," anasihi.

Mwinyi anafafanua kuwa mageuzi mengi yaliyofanyika wakati wa awamu yake hayakuwa ya kutafuta umaarufu, bali kuwaondolea wananchi adha mbalimbali. "Hatukuandika waraka, hatukubuni itikadi mpya na wala hatukutumia majukwaa kujinasibu. Mengi tuliyafanya kimya kimya, kwa ujasiri lakini na hekima pia. "Na siku zote nilijitahidi kupata maoni na baraka za chama na kusikiliza
na kupokea ushauri kwa dhati kabisa na kuuzingatia, si kutimiza wajibu tu.

"Kutoka kwa Mwalimu niliimarishwa hulka yangu ya kusikiliza kwa makini maoni na ushauri wa wengine kabla ya kufanya uamuzi na kuutekeleza. Na baada ya kuelewana na wenzangu tulisambaa nchi nzima kuwafahamisha wananchi," anasema. Mwinyi anabainisha kikwazo kikubwa kilichomkumba wakati wa kufanya mageuzi hayo kilitokana na kundi analiloliita la uhafidhina ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wenzake walioona vigumu kukubali haja na hoja ya mabadiliko, hasa pale ambapo hawakuwa na
uhakika na msimamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu mageuzi.

Katika kitabu chake hicho, Mwinyi pia anabainisha namna hali ya uchumi wa nchi ilivyokuwa mbaya wakati anakadhibiwa kijiti huku akisifu mchango wa Mwalimu Nyerere katika kurekebisha hali hiyo. Mwinyi anaweka wazi kuwa hata shinikizo IMF na Benki ya Dunia (WB) kwa Tanzania kukubaliana na masharti yao kama nchi inataka fedha (misaada na mikopo) kutoka kwao na wahisani wengine kutoka nchi za Magharibi, lilitatuliwa kwa ushauri wa Mwalimu Nyerere.

Anafafanua kuwa Mwalimu Nyerere hakukubaliana na baadhi ya masharti hayo na aliweka msimamo mkali na hivyo makubaliano hayakufikiwa mpaka anaondoka madarakani. Katika kutatua suala hilo, Mwinyi anarejea ushauri wa Mwalimu Nyerere akimnukuu: "Tazameni, pesa bado tunazihitaji ili tukwamue uchumi wetu uende mbele. Hali ni mbaya kweli. Maadamu mimi nimeng'atuka, sikserikalini, huu ndiyo wakati mzuri wewe Sheikh Ali na timu yako mkamilishe mazungumzo hayo na ninaamini yatakwenda vizuri maana
wakubwa hao wanajua kuwa yule mkorofi keshaondoka".

Mwinyi anasema ataendelea kumshukuru Mwalimu kwa uamuzi wake wa kuitisha kikao cha Kamati Kuu ya CCM (kilifanyika Zanzibar) na kutoa kauli ile mbele ya Kamati Kuu na hivyo kumpa rukhsa ya kuendelea na kazi hiyo ya kuimarisha uchumi wa nchi.

Chanzo: Nipashe
 
Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,797
2,000
Ujumbe mzuri huo kutoka kwa Mzee Mwinyi. Kuna haja ya kukisoma hicho kitabu ili kupata muktadha wa baadhi ya maamuzi yaliyofanyika kipindi chake ikiwa ni pamoja na Azimio la Zanzibar lililoondoa lile la Arusha bila mkakati wowote mbadala wa kusimamia miiko ya uongozi.
 
Tumbiliwaulaya

JF-Expert Member
Nov 22, 2020
276
500
Hii inafanana sana na report ya CAG kwa Samia,

Hii chapter imeandikwa lini? Je angeisema iwapo Mwendazake angekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa hicho kitabu?
Kitabu cha Mkapa kinaeleza mambo mengi sana ikiwemo jinsi CCM inachota pesa za umma kufanyia shughuri za chama, mwenda zake ndio alikizindua unakumbuka?
 
vexozanzhu

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
459
1,000
Una lako lingine linalokufanya umtukane lakini si kwa uongozi wake,mzee mwinyi amepokea nchi hii ikiwa kwenye hali mbaya sana lakini kwa jitihada zake alifanya maisha ya watu wengi kuwa na unafuu japo kulikuwa na kasoro hizi na zile ambazo zilikuja kurekebishwa na waliomfuata kwa kiasi walichoweza.
NAUUUUMIIIA SANA Nikiona watu waliofanya vitu vikubwa nchi hii kimya kimya wakiongelewa vibaya just because they didn't SHOUT SHOUT IN THE PUBLIC OR USE THE MEDIA OR UNNECESSARY PRESS CONFERENCE NATAMANI NINGELAANI WOTE WANAOWAONGELEA VIONGOZI FLANI FLANI VIBAYA WAKATI MAMBO YALIKUWA YAKIENDA VIZURI AAAAAAH.
 
FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
8,221
2,000
Utabishana vipi na mtu aliyekushika mkono na kukupa Urais mbele ya Wababe wengi kama akina Msuya
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,657
2,000
Mzee asingeila Idi ya Mwaka huu
🤣 aliyemnanga hapo ni yuleyule aliyemsifia sana kuwa amefanya makubwa sana ambayo yeye hakuweza kuyafanya kwa miaka 10
😅 na ni huyohuyo aliyempandisha chati mwanaye kule kiembembuzi

Mwaka huu siasa itafichua mengi sana ambayo hatukuyajua kabla
 
Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
773
1,000
Mzee Mwinyi ana hekima sana! Tatizo vijana na hasa walioko kwenye siasa kwa muda huu wengi ni vi.laza ,wahuni ,hawana muda wa kujisomea na kujua mambo kwa undani lakini pia ni wapenda sifa wasiojitambua wanaodhani siasa ni kutafuta maisha ya haraka haraka kupitia kiki za kijinga basi!
 
Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
2,540
2,000
Hiki kitabu naona kimejaa malalamiko tupu na mipasho
Mnaokisoma mniangalizie kama Mzee Ruksa amegusia chavda maana Kwa wale wahenga wenzangu Kwa wakati huo ukimtaja Mzee ungedhani ni replica ya chavda .
 
Asprin

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
63,859
2,000
NAUUUUMIIIA SANA Nikiona watu waliofanya vitu vikubwa nchi hii kimya kimya wakiongelewa vibaya just because they didn't SHOUT SHOUT IN THE PUBLIC OR USE THE MEDIA OR UNNECESSARY PRESS CONFERENCE NATAMANI NINGELAANI WOTE WANAOWAONGELEA VIONGOZI FLANI FLANI VIBAYA WAKATI MAMBO YALIKUWA YAKIENDA VIZURI AAAAAAH.
Kama lile lisukuma lililojenga uwanja wa ndege kwao, hivi sasa unatumika kuanika nafaka
 
Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,018
2,000

RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Nwinyi, amebainisha kuwa wakati wa uongozi wake, aliepuka kubishana hadharani
na mtangulizi wake, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, akiwaonya viongozi wa sasa kujaribu kupata uhalali wa wanayoyafanya
kwa kutupia lawama viongozi waliopita.

Katika kitabu chake cha 'Mzee Rukhsa, Safari ya Maisha Yangu', Mwinyi anasema aliona ilikuwa muhimu kwake kuepuka kubishana na Mwalimu Nyerere hadharani wala kukosoa uamuzi na yote yaliyofanyika wakati wa uongozi wake. "Ipo hulka ya kibinadamu ya viongozi wapya kujaribu kupata uhalali wa wanayoyafanya kwa kutupa kila aina ya lawama kwa viongozi waliopita.

Hayo, kwa maoni yangu ni makosa makubwa. "Hakuna kitu rahisi kama kukosoa wengine, lakini wananchi hawachagui kiongozi ili akaorodheshe lawama. Ukichaguliwa na wenzako kuwaongoza unakuwa umepewa dhamana kubwa kupeleka taifa mbele. "Wananchi wanataka kuona matokeo chanya ya unachokifanya wewe uliye na serikali kwa wakati huo, wakitambua kuwa kila awamu ya uongozi ina nafasi yake na inachokifanya ni sehemu ya mradi usioisha wa ujenzi wa nchi na kutumikia wananchi," anasihi.

Mwinyi anafafanua kuwa mageuzi mengi yaliyofanyika wakati wa awamu yake hayakuwa ya kutafuta umaarufu, bali kuwaondolea wananchi adha mbalimbali. "Hatukuandika waraka, hatukubuni itikadi mpya na wala hatukutumia majukwaa kujinasibu. Mengi tuliyafanya kimya kimya, kwa ujasiri lakini na hekima pia. "Na siku zote nilijitahidi kupata maoni na baraka za chama na kusikiliza
na kupokea ushauri kwa dhati kabisa na kuuzingatia, si kutimiza wajibu tu.

"Kutoka kwa Mwalimu niliimarishwa hulka yangu ya kusikiliza kwa makini maoni na ushauri wa wengine kabla ya kufanya uamuzi na kuutekeleza. Na baada ya kuelewana na wenzangu tulisambaa nchi nzima kuwafahamisha wananchi," anasema. Mwinyi anabainisha kikwazo kikubwa kilichomkumba wakati wa kufanya mageuzi hayo kilitokana na kundi analiloliita la uhafidhina ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), viongozi wenzake walioona vigumu kukubali haja na hoja ya mabadiliko, hasa pale ambapo hawakuwa na
uhakika na msimamo wa Mwalimu Nyerere kuhusu mageuzi.

Katika kitabu chake hicho, Mwinyi pia anabainisha namna hali ya uchumi wa nchi ilivyokuwa mbaya wakati anakadhibiwa kijiti huku akisifu mchango wa Mwalimu Nyerere katika kurekebisha hali hiyo. Mwinyi anaweka wazi kuwa hata shinikizo IMF na Benki ya Dunia (WB) kwa Tanzania kukubaliana na masharti yao kama nchi inataka fedha (misaada na mikopo) kutoka kwao na wahisani wengine kutoka nchi za Magharibi, lilitatuliwa kwa ushauri wa Mwalimu Nyerere.

Anafafanua kuwa Mwalimu Nyerere hakukubaliana na baadhi ya masharti hayo na aliweka msimamo mkali na hivyo makubaliano hayakufikiwa mpaka anaondoka madarakani. Katika kutatua suala hilo, Mwinyi anarejea ushauri wa Mwalimu Nyerere akimnukuu: "Tazameni, pesa bado tunazihitaji ili tukwamue uchumi wetu uende mbele. Hali ni mbaya kweli. Maadamu mimi nimeng'atuka, sikserikalini, huu ndiyo wakati mzuri wewe Sheikh Ali na timu yako mkamilishe mazungumzo hayo na ninaamini yatakwenda vizuri maana
wakubwa hao wanajua kuwa yule mkorofi keshaondoka".

Mwinyi anasema ataendelea kumshukuru Mwalimu kwa uamuzi wake wa kuitisha kikao cha Kamati Kuu ya CCM (kilifanyika Zanzibar) na kutoa kauli ile mbele ya Kamati Kuu na hivyo kumpa rukhsa ya kuendelea na kazi hiyo ya kuimarisha uchumi wa nchi.

Chanzo: Nipashe
Sasa kwa nini hakumshauri mwendazake jiwe kuacha kuwasema vibaya majikwaani viongozi waliostaafu na kila siku kazi yake ilikuwa kusema nchi imeliwa sana wengine hawajafanya anayofanya yeye?

Instead aliishia kusema aongezewe muda, hiki kizee bado kinanichefua sana
 
The Eye

Member
Oct 29, 2020
64
125
Hii inafanana sana na report ya CAG kwa Samia.

Hii chapter imeandikwa lini? Je, angeisema iwapo Mwendazake angekuwa Mgeni Rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa hicho kitabu?
Samia unamsingizia....report ya CAG haikumtaja kiongozi aliyepita.

Ila 'kiongozi aliyepita* ndo alikuwa anawasimanga sana wenzie.
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,657
2,000
Samia unamsingizia....report ya CAG haikumtaja kiongozi aliyepita.
Labda hujaelewa. report ya CAG kwa Mwendazake ilikuwa na para zingine mfukoni mwa CAG ndiyo hiyo ikasomwa kwa Samia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom