adriz
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 15,479
- 33,507
Moja kwa moja..
Kumekuwa na hoja miongoni mwa watu kuwa viongozi wa dini wa Kiislamu hawatetei haki wapo nyuma katika yale yanayoendelea nchini au wamepewa posho . Sasa nataka nichambue na tujadiliane wote kistaarabu kutokana na uelewa wangu wa kidini na kiulimwengu kutoka na hoja hizo.
Kwanza kabisa dini ya Uislamu inapinga mauji ya watu wasio na hatia , na dhuluma juu ya kiumbe chochote awe Muislamu, mkiristo , Yahudi hata adui yako nk haitakiwi kumfanyi dhuluma , kama aya inavyoeleza 👇👇
" ...Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni audilifu . Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamungu.." {5 : 8}
Na Uislamu unapinga mauji yeyote ya dhuluma na adhabu yake ni Kali mno kama kama inavyosema Aya hapo ,👇👇
"...kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.." {5 : 32 }
📝 MIONGONI MWA SABABU ZA KISHERIA ZINAZOFANYA MASHEIK NA WAISLAMU KUKAA MBALI NA MAANDAMANO.
NB : Kuna watu wanasema Masheik wanaona kiongozi ni Muislamu mwenzao ndio maana hawaonyeshi kuunga mkono maandamano, hoja hizo hazina nguvu sababu zinazofanya wasiunge mkono maandamano sio aliyopo ni Muislamu bali hata wakati wa Magu hali haikuwa tofauti walikuwa watii kwa Mamlaka.
1. Hakuna maelekekezo kutoka kwenye maandiko yanayotaka kuandamana katika kudai haki .
Masheik wanasimamia dini na dini ya Uislamu imetoa muongozo katika kila majambo hata jinsi ya kuyaendea .
Muongozo wa Uislamu umeelekeza kwanza kutii Mtawala hata akiwa sio Muislamu maadamu hakuamrishi katika maasi , na ikiwa atakuamrisha maasi hautomtii kwenye huo uasi anaokuamarisha bali utamtii kwenye majambo mengine. Kama inavyoeleza katika Aya hii 👇👇
" Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi " { 4 : 59 }
Je , kiongozi akizidi ujeuri na dhuluma hatuna nafasi ya kujinasua ?
Kiongozi ni product ya jamii , Jamii ikiwa ya hovyo lazima watapatikana viongozi wa hovyo hakuna namna ndio maana sisi kwa sisi tunafanyiana dhuluma sana mtu hata apewe kitengo kidogo cha kukusanya pesa ya rambirambi unakuta huko mtu anachukichia sasa mtu kama huyo akija kupata madaraka atakuwa fisadi zaidi.
Katika Uislamu kutengeneza Jamii lazima utengeneze watu na kutengeneza watu ni lazima kuanzie katika Misingi ya chini kwenye Familia , malezi na Elimu na wao wenyewe kuwa waadilifu na wachamungu kabla ya kutaka viongozi wao wawe waadilifu. 👇👇
" ..Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo nafsini mwao.. " { 13 : 11 }
Je , hatuwezi kutoka kupigana na kufanya Uasi katika kujinasua ?
Kabla ya kutaka kupigana au kufanya Uasi kwanza anagalia haya ;👇
a) Uwezo wa kupigana unao yaani umejipanga ?
Kama mnakumbukumbu siku za mwanzo wa shambulio la October 7 Waislamu baadhi waliwashangilia Hamas na kuona vidume wanapigania haki hawataki uonevu lakini Mimi nikisikitika na kuonya kuwa wamefanya upuuzi na utawaponza mno sababu .
i)Hamas walikuwa kama wamekurupuka hawakujipanga kivita bali ni kufanya ambush na ufedhuli .
ii) Hamas hawezi KuBattle na so called Israel state sababu ukiCompare uwezo wa kijeshi na allies Hamas wameachwa mbali mno.
iii) Retaliation ya Netanyahu itakuwa haina huruma kabisa jamaa ni mwendawazimu.
Usipokuwa na uwezo wa KuBattle na mpinzani wako Wala kujipanga kisasawa ni sawa na kujiua kizembe Kwa sababu hizo MaSheikh hawawezi kuwaambia waumini wao watoke wakati ;
i) Polisi ana Gun na mabomu , halafu raia wana mawe na fimbo .
ii) Ukichaa wa Polisi na ukatili wao unafahamika ukikutana nao katika mazingira hayo hakuna chance ya kuBattle wakati raia mpo peke yenu bare hands hata kama mpo wengi.
Msingi huu upo hata katika Jihad za kisheria kiongozi wa Dola ya Kiislamu katika nchi ya Kiislamu haurusiwi kutoa jeshi ukiwa disorganized na uwezo wako ni mdogo kuBatte na mpinzani .Inachotakiwa ni kujipanga kwanza kikamilifu Kisha kujiingiza vitani. Ndio maana hata vita ikawekewa nidhamu na watu kiasi gani mpambane na watu kiasi gani na sio kwenda kizembe mkafyekwa wote 👇👇
" Kwa hivyo wakiwa wapo watu mia moja kati yenu wenye kusubiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ( 8 : 66 )
Vilevile kukawekwa nidhamu ya kujiandaa kwa uwezo wote dhidi ya adui na sio kwenda kizembe au kukaa kizembe bila maandalizi , isiwe adui ana Hypersonic ballistic missile na Nyuklia wewe vibomu vya kawaida , adui yako ana Gun wewe una panga na fimbo . Muislamu hatakiwi kwenda front vita kama hiyo 👇👇
b) Kupima madhara yake kabla ya uasi na vita.
Kanuni ya msingi katika Uislamu likiwa jambo lina Faida na madhara , basi unaangalia kipi kitazidi mizani kati ya Faida na madhara au Faida zitakuwa chache lakini madhara makubwa ? Kama jambo lina Faida lakini madhara ni makubwa basi tunaacha kwani kuondosha madhara makubwa ndio kunapaswa.
kutangulizwa kwanza kuliko kuangalia Faida zitakazopatikana .
Ndio maana niliwasikitia WaPalestina since day one kabla ya kilicho wakuta sababu nilijua jinsi hali Yao ilivyo na adui wao alivyo katili...
NB : Episode ya kwanza imeisha uzi utaendelee na episode ya pili ambayo panapo majaliwa utaeleza sababu nyingine na kuchambua ;
1. Je , inaruhusiwa kukalia maovu kimya bila kukemea ?
2. Je , Kuna njia ngapi za kukema maovu na ipi Bora kutumika kwa wakati upi ?
3. Uchambuzi wa kuhusu kipi Cha kufanya juu mtawala muovu kwa mujibu wa mafundisho sahihi ya Uislamu.
Huu Uzi nimeuketa sababu Kuna Waislamu waliniomba hapa jukwaani live na wengine kunifuata PM kutaka nifafanulie kwa mujibu wa Uislamu niweke na dalili kuhusu wajibu wetu sisi Waislamu kwa yanayoendelea tukiwa kama sehemu ya nchi na Jamii kwa ujumla.