Uchakachuaji barabara za ndani Arusha, Waziri unalijua hili?

mshana org

JF-Expert Member
Jan 28, 2012
2,091
618
Nimepita maeneo ya Makao mapya mjini hapa Arusha, nimejionea barabara za ndani ya mji zinazojengwa kwa kiwango cha lami na wakandarasi wa kichina.

Lami inayowekwa haina kina hata 3cm wakishaweka moram na kokoto wanaweka lami nyembamba sana baada ya hapo barabara inafungwa kwa karibu siku 3 kabla ya kuanza kutumika.

Swali: Barabara hizi zitadumu kwa muda gani kabla ya kuanza repea ya kujaza viraka?

Je, huu sio uchakachuaji wa kodi zetu? Je, hiki ndicho kiwango stahiki?
 
Attachments

  • Lami 2.jpg
    Lami 2.jpg
    642.4 KB · Views: 72
  • Lami.jpg
    Lami.jpg
    793.2 KB · Views: 64
yani pamoja nakuzifunga kwa mawe lakini wapita kwa miguu wakikanyaga lamiyote inabanduka.pia hao wahsani wanaotoa fedha zakujengea barabara za kiwangohicho?kesho tutaambiwa ujenzi huo umegarimu mabilion ya shiling.
 
Nimeona road za kaloleni duh bora wangeweka changarawe moja kwa moja..ela zimepigwa..tizama gari binafsi la meya wa beijing mr Lymo
 
Natoka porini usiku huu ili niende Arusha nihakikishe kwa macho yangu. Ahsante kwa taarifa
 
nimepita kaloleni hii ya kutokea roundabout ya florida kuna mahali pameshabanduka
 
wenyewe wanasema sio kodi zetu ni wahisani wa world bank!

W/B ni bank na huwa haitoei vitu bure kirahisi.Hata Ads hawafanyi katika hayo maeneo labda kama ni njia ya kwenda ktik utajiri ambao kawekeza bepari waliomkopesha.Huo utakuw amkopo wenye riba nafuu.(isiyokuwa na unafuu hivyo)

Hayo ndio matokeo ya Utalii uliorudi katik ule mkutano CCM na presidaa walisema kuwa maandamano yalipositishwa mikutano imenza kuja.Wale ni ADB na W/B na sijui bank ya waarabu, sijui na bank gani huwa wanafanya kazi kwa faida, na wao ndio wanasaka wateja.Sasa kama sisi tuliandaa mkutano mkubwa ili mabenki waje tuuzia sera na mikopo kwa masharti yao imekula kwetu.Hao jamaa wa ADB na W/B wangeweza kuja fanya mkutano hata kama kungekuwa na mabomu achilia mbali maandamano ya CDM abayo hata hayana time na raia wala wageni.W/B wanafanya mikutano tena kwa hela na ulinzi wao Afghanistani,pakistani, somalia, na Iraq ndio bongo.Kweli tumechoka.Tuna uwezo mkubwa wa kujitete ili tuwahi kuibia na kuuwawa na si kujiokoa.
 
Nimepita maeneo ya Makao mapya mjini hapa Arusha, nimejionea barabara za ndani ya mji zinazojengwa kwa kiwango cha lami na wakandarasi wa kichina.

Lami inayowekwa haina kina hata 3cm wakishaweka moram na kokoto wanaweka lami nyembamba sana baada ya hapo barabara inafungwa kwa karibu siku 3 kabla ya kuanza kutumika.

Swali: Barabara hizi zitadumu kwa muda gani kabla ya kuanza repea ya kujaza viraka?

Je, huu sio uchakachuaji wa kodi zetu? Je, hiki ndicho kiwango stahiki?

tusiseme sana maana inawezekana ndio quotation alizopewa mkandarasi, mind you kila mradi lazima uwe na project engeneer kutoka upande wa client(jiji), kwa hiyo inawezekana hicho ndicho alichoambiwa afanye na client wake, labda tumuulize meya wa jiji au mkurugenzi ama mhandisi wa jiji watujuze ukweli.
 
bwana Mkiva nadhani wewe ni mvivu wa kufikiri. nimekuwa Arusha for some years, sijawahi kuona barabara iliyo jengwa kwa viwango kama hizi zinavyojegwa sasa, wewe unachosema na ulichoona ni hatua za awali kabisa za kuweka lami, hicho ulichokiona ukapiga picha na kutuwekea hapa siyo lami hiyo. Siku nyingine ukiona jambo hulielewi uliza, usikurupuke tu.
 
Ngojeni lami iwekwe siasa mmeanza mapema, hizo picha hazionyeshi lami.
 
i
bwana Mkiva nadhani wewe ni mvivu wa kufikiri. nimekuwa Arusha for some years, sijawahi kuona barabara iliyo jengwa kwa viwango kama hizi zinavyojegwa sasa, wewe unachosema na ulichoona ni hatua za awali kabisa za kuweka lami, hicho ulichokiona ukapiga picha na kutuwekea hapa siyo lami hiyo. Siku nyingine ukiona jambo hulielewi uliza, usikurupuke tu.

MKuu jamaa kapiga picha primer anasema ni lami! teh teh teh. JF ni jukwaa mwanana kweli.
 
Aisee mkuu siyo kwamba natetea wala nini ila mimi naishi maeneo haya naona ujenzi mzima unavyoendelea,,hizo picha ulizopiga ni barabara ya kwendea kaloleni kwa kupitia florida round about ambayo bado haijamaliziwa kabisa ndo wapo hatua za mwanzo kuweka lami lakini barabara wanaijenga kwa kiwango kizuri kama ungetaka kuona pita njia ya hapo seliani hospita mpaka kule NHC buildings utaona ubora wa hizo barabara baada ya kukamilika alaf utatoa marks wewe mwenyewe
 
bwana Mkiva nadhani wewe ni mvivu wa kufikiri. nimekuwa Arusha for some years, sijawahi kuona barabara iliyo jengwa kwa viwango kama hizi zinavyojegwa sasa, wewe unachosema na ulichoona ni hatua za awali kabisa za kuweka lami, hicho ulichokiona ukapiga picha na kutuwekea hapa siyo lami hiyo. Siku nyingine ukiona jambo hulielewi uliza, usikurupuke tu.

Mkuu nimeuliza hata wakazi wa hapo wakaniambia ndio mpango mzima mkuu
 
Back
Top Bottom