Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,851
- 7,764
Siku chache zilizopita nilikuja na Uzi, Fomu za matokeo ya uchaguzi Congo bado hazijaandaliwa na huenda uchaguzi huo usifanyike tarehe23/12/2018.
Jana tume ya uchaguzi nchini humo CENI imesogeza uchaguzi huo mbele kwa siku saba hadi 30/12/2018. Sababu ilitajwa kuwa Fomu za matokeo zitakamilika 25/12/2018 na hivyo uchaguzi hauna budi kucheleweshwa. Sababu nyingine ni kuungua kwa ghala la vifaa vya uchaguzi huko Kinshasa na hivyo ipo haja ya kuagiza vifaa vingine. Mlipuko wa Ebola pia umetajwa kuwa ni sababu ya kuahirishwa huko kwa uchaguzi japo wachambuzi wanadai sababu hii ya tatu ina ukakasi.
Wagombea 21 wanachuana ktk uchaguzi huo ila ni watatu tu wanapewa nafasi kubwa. Hao ni Martini Fayulu, Emmanuel Shadari na Felix Tshekedi. Uchaguzi mkuu ktk taifa hilo maskini duniani lenye rasilimali nyingi na udongo mzuri kwa kilimo umeahirishwa zaidi ya Mara tatu sasa.
Rais Kabila aliyechukua urais akiwa na umri wa miaka 30, ameliongoza taifa hilo kwa miaka 17 na analiacha likiwa maskini kabisa huku akiwa ni moja wa viongozi wanaongoza duniani kwa kuchukiwa na wananchi wake.
Kuahirishwa kwa uchaguzi huo kumeibua taharuki na wasiwasi miongoni mwa wananchi wa taifa hilo kubwa barani Africa.