Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nadhani Uhuru Kenyatta na Wafuasi wake wa Jubilee wanajifariji tu na ushindi huu mkubwa wanaoupata katika uchaguzi huu wa kurudiwa. Nimetafakari sana, na kuona kuwa kuna uwezekano mkubwa sana wa uchaguzi huu kurudiwa tena (re-run of the re-run election).
Ninahisi hapa, ni kwamba Uhuru Kenyatta alishinikiza huu uchaguzi wa marudio ufanyike ili kukwepa kipengele kinachomtaka aachie uraisi na kukabidhi uraisi kwa spika ikiwa uchaguzi wa marudio hautafanyika katika siku 60 toka ubatilishwe. Uchaguzi huu wa marudio ukibatilishwa, Uhuru ataendelea kuwa raisi chini ya sheria hiyohiyo ya siku 60 kwa kuwa uchaguzi wa marudio utakuwa umempa tena mamlaka uraisi na kuhitimisha zile siku 60 za ubatilishwaji wa uchaguzi wa kwanza. Ni kama Uhuru amepania kwamba uchaguzi wowote wa uraisi lazima ufanyike yeye akiwa raisi, sio akiwa amekabidhi uraisi kwa spika.
Sababu za kubwa za kufanya uchaguzi wa marudio urudiwe tena, ikiwa utapingwa mahakamani, ni kama zifuatazo;

- Kuna baadhi ya vipengele vilivyoamriwa virekebishwe na Mahakama Kuu iliyobatilisha havikurekebishwa
- Tayari kulikuwa na shauri la kuomba kuahirishwa kwa uchaguzi ambayo haikusikilizwa kutokana na kutotimia quorum ya majaji - lakini kwa kanuni ya sheria kutosikilizwa kwa shauri hilo ni justice denied, kitu ambacho hakikubaliki kisheria
- Siku chache kabla ya uchaguzi kuna kesi dhidi ya maofisa wa uchaguzi (returning officers) ambapo mahakama ilitoa hukumu kwamba kuteuliwa kwao kulikuwa batili, na bado hawa maofisa walitumika katika uchaguzi wa marudio kwa kuwa hakukuwa na muda wa kuwateua kivingine ili wawe halali
- Uchaguzi umefanyika katika mazingira hatarishi na inawezekana kabisa zaidi ya 50% ya watu waliojiandikisha wameshindwa kupiga kura (takwimu zimeonyesha waliopiga kura ni 33% tu ya waliojiandikisha)
- Tume ya uchaguzi ilishatoa tamko kwamba haiwezi kutoa hakikisho kwamba ingesiamamia uchaguzi wa marudio ili uwe wa uhuru na haki
- Kuna sehemu za Kenya ambako watu walishindwa kabisa kupiga kura kutokana na sababu mbalimbali na hivyo kuwanyima haki yao ya kupiga kura