Uchaguzi wa uliorudiwa Kenya una kila harufu ya kurudiwa tena!

Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,099
Likes
6,264
Points
280
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,099 6,264 280
Nadhani Uhuru Kenyatta na Wafuasi wake wa Jubilee wanajifariji tu na ushindi huu mkubwa wanaoupata katika uchaguzi huu wa kurudiwa. Nimetafakari sana, na kuona kuwa kuna uwezekano mkubwa sana wa uchaguzi huu kurudiwa tena (re-run of the re-run election).

Ninahisi hapa, ni kwamba Uhuru Kenyatta alishinikiza huu uchaguzi wa marudio ufanyike ili kukwepa kipengele kinachomtaka aachie uraisi na kukabidhi uraisi kwa spika ikiwa uchaguzi wa marudio hautafanyika katika siku 60 toka ubatilishwe. Uchaguzi huu wa marudio ukibatilishwa, Uhuru ataendelea kuwa raisi chini ya sheria hiyohiyo ya siku 60 kwa kuwa uchaguzi wa marudio utakuwa umempa tena mamlaka uraisi na kuhitimisha zile siku 60 za ubatilishwaji wa uchaguzi wa kwanza. Ni kama Uhuru amepania kwamba uchaguzi wowote wa uraisi lazima ufanyike yeye akiwa raisi, sio akiwa amekabidhi uraisi kwa spika.

Sababu za kubwa za kufanya uchaguzi wa marudio urudiwe tena, ikiwa utapingwa mahakamani, ni kama zifuatazo;
  1. Kuna baadhi ya vipengele vilivyoamriwa virekebishwe na Mahakama Kuu iliyobatilisha havikurekebishwa
  2. Tayari kulikuwa na shauri la kuomba kuahirishwa kwa uchaguzi ambayo haikusikilizwa kutokana na kutotimia quorum ya majaji - lakini kwa kanuni ya sheria kutosikilizwa kwa shauri hilo ni justice denied, kitu ambacho hakikubaliki kisheria
  3. Siku chache kabla ya uchaguzi kuna kesi dhidi ya maofisa wa uchaguzi (returning officers) ambapo mahakama ilitoa hukumu kwamba kuteuliwa kwao kulikuwa batili, na bado hawa maofisa walitumika katika uchaguzi wa marudio kwa kuwa hakukuwa na muda wa kuwateua kivingine ili wawe halali
  4. Uchaguzi umefanyika katika mazingira hatarishi na inawezekana kabisa zaidi ya 50% ya watu waliojiandikisha wameshindwa kupiga kura (takwimu zimeonyesha waliopiga kura ni 33% tu ya waliojiandikisha)
  5. Tume ya uchaguzi ilishatoa tamko kwamba haiwezi kutoa hakikisho kwamba ingesiamamia uchaguzi wa marudio ili uwe wa uhuru na haki
  6. Kuna sehemu za Kenya ambako watu walishindwa kabisa kupiga kura kutokana na sababu mbalimbali na hivyo kuwanyima haki yao ya kupiga kura
 
Shana Chuma

Shana Chuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Messages
2,118
Likes
2,054
Points
280
Shana Chuma

Shana Chuma

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2016
2,118 2,054 280
Jifunze kwanza matumizi ya "ra" na "la" ndipo uanzishe thread zako za kubashiri.
 
pingli-nywee

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Messages
6,861
Likes
5,496
Points
280
pingli-nywee

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2015
6,861 5,496 280
Maelezo yake yoote umeona hilo tu!
Naona unatetea hiyo lafudhi yenu ya kinkurunzinza. Big up, we jamaa huwa mzalendo sana kwa nchi yako Burundi.
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,099
Likes
6,264
Points
280
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,099 6,264 280
Jifunze kwanza matumizi ya "ra" na "la" ndipo uanzishe thread zako za kubashiri.
Seriously Mkuu, niambie ni wapi na nitafurahi kurekebisha. La sivyo ushauri wako na ukurudie mwenyewe, maana mie sijaona ninapohitaji kurekebisha.

NB: Hatimae nimeona - kwenye title nimesema "kira" badala ya "kila". That was a typo, sio suala la mie kujifunza matumizi ya "ra" na "la". Tatizo sijui namna ya ku-edit thread title. Huwa naomba Moderators wanisaidie kurekebisha kosa kwenye title.

Hata hivyo, you should be intelligent enough kuona kipi ni typo na kipi ni mapungufu katika kujua lugha.
 
M

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Messages
501
Likes
625
Points
180
M

MAGALLAH R

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2014
501 625 180
Naona Uhuru anataka kuingia ikulu by any means necessary
 
S

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Messages
4,494
Likes
7,422
Points
280
S

Sexless

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2017
4,494 7,422 280
The fact that Maraga has voted isn't the move to justify the good preparations of re- run election?

The Kshs:1bn deposited in the bank account of Maraga, are its source (from who) and motive known?
But all in all, nullifying the election for the second time it will kill the economy of Kenya.
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Messages
12,386
Likes
12,169
Points
280
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2014
12,386 12,169 280
Mbona wa Zanzibar haukurudiwa tena pamoja na Maalim kususa?
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,099
Likes
6,264
Points
280
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,099 6,264 280
The fact that Maraga has voted isn't the move to justify the good preparations of re- run election?

The Kshs:1bn deposited in the bank account of Maraga, are its source (from who) and motive known?
But all in all, nullifying the election for the second time it will kill the economy of Kenya.
If Maraga hadn't voted, people would have said he was biased against the rerun election. So it was very wise of him to go and vote.

As for the deposited funds into his account, he issued a statement that he had no idea where the money came from, and the bank should remove it immediately. The bank issued a statement that it was a deposit/transfer error. NO big deal about that. Remember something similar happened to a a student in South Africa, millions of Rands were transferred into her account by mistake (in her case she happily went on a spending spree and when the error was discovered she was ordered to pay what she had spent by then. I am told she committed suicide - not sure if it is true).
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,099
Likes
6,264
Points
280
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,099 6,264 280
aingie mara ngapi wakati hadi sasa yuko ndan ya ikulu
Hata kama akibaki Ikulu, sasa issue ni kwa kiasi gani turn out ya 33% ya watu waliopiga kura wanampa legitimacy ya kuwa raisi wa Kenya.

Tatizo viongozi wa Afrika huwa hawana aibu. Hata turnout ikiwa 10% ya wapiga kura, sidhani kuna kiongozi Mwafrica ataona si vema akaapishwa kuwa raisi wa nchi, sembuse 33%!
 
Sexer

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Messages
4,249
Likes
2,554
Points
280
Sexer

Sexer

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2014
4,249 2,554 280

mtu alazimishwi kupiga kura, na rais ni rais tu kuwe na turn out ya 100% ama 30% haijalishi. madaraka ya rais yapo kikatiba haijalishi turn out kwenye election ilikuwaje. na kumpenda rais hulazimishwi wajibu wako ni kutii sheria za nchi
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,099
Likes
6,264
Points
280
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,099 6,264 280
mtu alazimishwi kupiga kura, na rais ni rais tu kuwe na turn out ya 100% ama 30% haijalishi. madaraka ya rais yapo kikatiba haijalishi turn out kwenye election ilikuwaje. na kumpenda rais hulazimishwi wajibu wako ni kutii sheria za nchi
Ingekuwa hivyo Mkuu, Kenya sasa hivi wasingekuwa wanajadili kutunga sheria ya kulazimisha watu kupiga kura (mandatory voting law). Wameona kuwa na preseident aliyechaguliwa kwa turn out ya 33% ni issue!
 
Sexer

Sexer

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Messages
4,249
Likes
2,554
Points
280
Sexer

Sexer

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2014
4,249 2,554 280
Ingekuwa hivyo Mkuu, Kenya sasa hivi wasingekuwa wanajadili kutunga sheria ya kulazimisha watu kupiga kura (mandatory voting law). Wameona kuwa na preseident aliyechaguliwa kwa turn out ya 33% ni issue!
kwa hiyo unataka kusema iko hivyo?! bas kama iko hivyo wasingejadili kutunga hiyo sheria, so kwa mazingira ya sasa mtu halazimishwi kupiga kura ndo maana wanajadili huko baadae labda waanze kulazimishwa. afu nakushangaa unavyoshangaa suala la turn out, inafahamika hiyo ni kwa sababu ya kujitoa mshindani mkuu mmoja hali iliyopelekea wafuasi wake kwa wingi kutopiga kura, na pia baadhi wafuasi wa mshindani mkuu aliyebaki uchaguzini kuacha kupiga kura wakijua mgombea wao atashinda hivyo hakuna haja ya kuhangaika kupiga kura watakaopiga inatosha.
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
6,099
Likes
6,264
Points
280
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
6,099 6,264 280
kwa hiyo unataka kusema iko hivyo?! bas kama iko hivyo wasingejadili kutunga hiyo sheria, so kwa mazingira ya sasa mtu halazimishwi kupiga kura ndo maana wanajadili huko baadae labda waanze kulazimishwa. afu nakushangaa unavyoshangaa suala la turn out, inafahamika hiyo ni kwa sababu ya kujitoa mshindani mkuu mmoja hali iliyopelekea wafuasi wake kwa wingi kutopiga kura, na pia baadhi wafuasi wa mshindani mkuu aliyebaki uchaguzini kuacha kupiga kura wakijua mgombea wao atashinda hivyo hakuna haja ya kuhangaika kupiga kura watakaopiga inatosha.
Hapana Mkuu, haiko hivyo kwa sasa. Ninachomaanisha ni kwamba hata wao wanaona haiko sawa Raisi kuchaguliwa kwa 33% turn out. Ndio maana wanataka kuwa na sheria inayofanya iwe lazima kwa watu kwenda kupiga kura, ili iwe ni kosa la jinao kwa mfano Odinga kushawishi watu wasipige kura siku zijazo, na kuondokana na aibu ya kuwa na raisi alieyechaguliwa kwa 33% turn out.

Na ni wazi Odinga alijitoa na ku-campaign watu wasijitokeze ili ku undermine credibility ya ushindi wa Uhuru kwenye rerun election.

Hata hivyo it is too soon kusema ushindi wa Uhuru wa hii rerun vote hautapingwa mahakamani na kubatilishwa. Binafsi nadhani kuna zaidi ya 60% probability ya uchaguzi kurudiwa tena! Kumbuka katika mambo haya election cost will never override an election constitutional right.
 
Forum statistics

Threads 1,250,458
Members 481,354
Posts 29,733,803