Uchaguzi wa Meya Dar Waota Mbawa

Uchaguzi wa Meya Dar Waota Mbawa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
UCHAGUZI wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam bado ni kitendawili licha ya Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kuwa na idadi kubwa ya wajumbe kuliko Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini bado hawaishi vikwazo, anaandika Happyness Lidwino.

Wajumbe halali walioshiriki katika uchaguzi wa mameya wa Halmashauri za Manispaa Jijini ni 163 huku CCM wakiwa 76 na Ukawa 87, kwa hivyo Ukawa kuwazidi CCM wajumbe 11.

Akizungumza na waandishi leo Jijini Mwita Waitara Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam Kuu ‘’The Great Dar’’ amesema wanashangazwa na mbinu zinazotumiwa na CCM kwa kuwashirikisha watumishi wa serikali katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema CCM wanafanya kila mbinu ili kulipoka Jiji licha ya kuwa na idadi ndogo ya wapiga kura. Mbinu hizo pia wamemshirikisha Willson Kabwe Mkurugenzi wa Jiji kuvunja sheria katika majukumu yake.

Mbinu nyingine waliyoitumia ni kuwaandaa wanachama feki wa CCM wakiongozwa na wakili Elias Nawela kufungua kesi ya madai huku wakitaka wajumbe 9 toka Zanzibar na 11 kutoka mikoa mingine kushiriki uchaguzi wa meya.

Waitara amesema, kesi hiyo yenye jarada namba 39 ya mwaka 2016 wameshaomba kujiunga na kesi hiyo huku wakiwa na mawakili wa kutosha ambapo inatarajiwa kusomwa Machi 21 mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu.

‘’CCM haina ujanja kwa sasa kwani tunapambana nao, na hatutakubali wajumbe wasiohusika kupiga kura wakati ni kinyume cha sheria ya Serikali za Mitaa za mwaka 1982 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2006,’’ amesema Waitara.

‘’Juzi tumepokea barua kutoka kwa Mkurugenzi ya mwaliko wa ushiriki katika uchaguzi wa meya wa Jiji lakini ndani ya barua hiyo kuna kitu hatujakubaliana nacho. Barua inaeleza uchaguzi utafanyika Machi 22 mwaka huu ukumbi wa Kareemjee lakini wanaotakiwa kuingia ni wajumbe tu,.

Wananchi na wafuasi wa vyama hawataruhusiwa kushuhudia ucha guzi huo. Tunajua hizo ni mbinu za CCM kwa kuwa kuna uovu umepagwa kufanyika siku hiyo.
Kufuatia hali hiyo Waitara amesema Ukawa umemwandikia barua Mkurugenzi huyo ya kutokubaliana na matakwa yake ya kuzuia wafuasi wa vyama kuingia ukumbini wakati wa uchaguzi kwani ni uvunjifu wa sheria na kwamba hawatakubali, bali watawapigania na kuhakikisha wananchi wanaingia ukumbini.

Aidha, kuhusu kesi iliyopo mahakamani watahakikisha sheria inafutwa hata kama uchaguzi utapelekwa mbele lakini hawatakubali kuruhusu mamluki wa CCM kuingia ukumbini kwani wao hawatashiriki uchaguzi huo.
 
Ngoja niendelee kuwa mwalimu maana huu unafiki wa wanasiasa wa ccm unakatisha tamaa...hivi waliruhusu vyama vingi vya nini kama hawakuwa tayari kupokea matunda ya vyama vingi...
 
Kauli ambayo miaka yote CCM imekuwa ikiitoa ni kwamba "msichague upinzani, wataleta vita!" Tangu nikiwa O-Level enzi zile; pamoja na uelewa wangu mdogo; bado sikuacha kujiuliza "sasa mtu umeshamchagua na yupo madarakani; aanzishe vita kwa maslahi ya nani?" Tayari nilishakuwa na ulewa kwamba aanzishae vita ni yule anayeshindwa uchaguzi na hapo kupata jibu kwamba kumbe CCM wanachowaambia wananchi ni kwamba, wakichagua upinzani, wao CCM wataingia msituni!!

Nakiri kwa nafsi huku Mungu akiniona na anipe adhabu yoyote ikiwa nitakuwa naongea uongo! Hapo zamani, niliamini CCM wasingeweza kufanya hivyo hata kama kweli wanashindwa uchaguzi! Kinyume chake hivi sasa; kila ninapoangalia wanavyong'aninia umeya Dar es salaam... ikiwa na maana kwamba hawakubali kuiacha Dar es salaam; ndipo hivi sasa najiuliza ikiwa kuiacha Dar es salaam tu ni kwa mbinde namna hii; je ni kweli hawa watu wanaweza kuwa tayari kuiacha nchi nzima?! Nikachanganya na yale ya Zanzibar shaka yangu inaongezeka maradufu.
  • CCM mnanitisha
  • CCM mnanitia hofu
  • CCM mnanifanya nifikirie ni-conclude kwamba amani tuliyonayo nchi mwetu haitokani na CCM bali inatokana na upinzani kukubali kushindwa bila kujali ikiwa ni kushindwa huko ni kwa halali au hapana!
  • Ikiwa kuachia mkoa mmoja wa Dar es salaam mnaona taabu hadi mnafikia hatua ya kufoji hadi hati za mahakama; hivi kweli mtakuwa tayari kuachia mikoa yote 26 nyinyi?!
 
Wanasema ukitaka kuona nyeti za kuku wee kaa upande upepo unapotoka utaziona pasina shida.

Iweje kila siku kuku anywe maji tu na asiende haja ndogo, safari hii lazma aende haja ndogo ameshakunywa sana maji kwa kweli.
 
Kama kweli Mh Magufuli amedhamiria kutumbua majipu basi anatakiwa aukubali ushindi halali wa ukawa kwenye umeya wa dar.manake ukawa watamsaidia sana kutumbua majipu yaliyoko dar..mirija yote ya unyonyaji waliyoiweka wenzake wa ccm itakatwa tu..ila kwa wao kuendelea kuzuia ushindi wa ukawa dar inatufanya sisi wananchitujiulize mara mbilimbili ukweli wa dhana yake ya kutumbua majipu..kama ni kweli aliimanisha alichokisema au zilikuwa ni sanaa za zekomedi?
 
Yan hapa ndo hawa jamaa huwa wanajidhalilisha sana, sehemu zote na miaka yote waliyowahi kuwa wao wengi, uchaguzi ulienda vizuri na hakukuwa na matatizo, ila leo wameshindwa, yan figisu figisu haziishi, mara hiki mara kile. Kama hiyo ofisi ina madudu mengi si wayatatue tu hayo. Yan mtu mweusi alilaaniwa kwa kweli.
 
UKAWA iteni mwanasheria Muapisheni wagombea wenu muanze kazi , nilikwisha sema humu kama meya atatoka UKAWA ( kama dunia inavyotarajia ) mabasi ya mwendo kasi yatatoweka , hii ndio shida kubwa , simbachawene anaburuzwa na kutumwa tu , katika hili hana uwezo wa kulimaliza , siasa za kishamba za akina juma simba hazitatupeleka popote , naishukuru timu yangu ya simba kwa kumtimua kwa ubadhilifu .
 
Kama wajumbe ni walewale 163 sioni shida na kama kuna wengine ambao sio, basi na wao waongeze idadi ya wajumbe, make CCM wanaweza wakaongeza wajumbe siyo ili wakapige kura bali kuvuruga uchaguzi, maana yake ni kwamba wanaingia wajumbe ambao hawausiki lakini mkurugenzi anawakubalia kwa kisingizio kuwa ni viongozi wa serikali, na UKAWA watakapo anza kuhoji polisi watakuja kuwakamata kwa kisingizio cha kuvuruga amani kwenye uchaguzi, watakamatwa hata watu kumi na mbili ili mradi wa hakikishe mmepungua na uchaguzi utaendelea, kwa kuwa mtakua pungufu watashinda uchaguzi. Kwa kuwa UKAWA wamewazidi CCM na wajumbe 11 bac watakamatwa 12 na tayari CCM itakua na zaidi ya mjumbe mmoja.
 
Kama kweli Mh Magufuli amedhamiria kutumbua majipu basi anatakiwa aukubali ushindi halali wa ukawa kwenye umeya wa dar.manake ukawa watamsaidia sana kutumbua majipu yaliyoko dar..mirija yote ya unyonyaji waliyoiweka wenzake wa ccm itakatwa tu..ila kwa wao kuendelea kuzuia ushindi wa ukawa dar inatufanya sisi wananchitujiulize mara mbilimbili ukweli wa dhana yake ya kutumbua majipu..kama ni kweli aliimanisha alichokisema au zilikuwa ni sanaa za zekomedi?
Ni ndoto kuendelea kufikiria kuwa ili nchi hii iendelee basi lazima mawazo ya kuisukuma mbele yatokane tu na CCM kisa eti wao ndio chama kilicholeta uhuru/ukombozi.Kama kuna watu hawakupaswa hata kusimama tena mbele ya watanzania na kuongelea habari ya mipango ya kuendeleza nchi basi ni CCM na washirika wake.
 
Na-declare interest kwanza kuwa miye siyo mwanachama wala mfuasi na shabiki wa chama chochote cha siasa hapa nchini. Hili la ccm kutaka kila kitu kiwe upande wao ni tatizo litakalokuja tuingiza kwenye machafuko siku za usoni. Wao wana rais ambaye akiamua hata kesho kuvifuta vyama vya siasa anaweza. Ni kwanini wauhadae ulimwengu kuwa nchi hii kuna demokrasia wakati sivyo? Hebu wajitafari tena na kuacha chaguzi ziwe huru na haki. Waache kupoteza muda wa wengine.
 
Elias Nawera anatumia taaluma yake vibaya. I know him since utawala wa kikwete hata harakati zake za ubunge ziligubikwa na Rushwa tupu.
 
Kuna barua ya CUF ya tarehe 17th March 2016, kwa Spika wa bunge kuhusu kujiuzuru nafasi zao zote za ubunge wa Zanzibar na Tanzania Bara je ni kweli? si deep green watapenyea hapo....
 
Back
Top Bottom