Kauli ambayo miaka yote CCM imekuwa ikiitoa ni kwamba "msichague upinzani, wataleta vita!" Tangu nikiwa O-Level enzi zile; pamoja na uelewa wangu mdogo; bado sikuacha kujiuliza "sasa mtu umeshamchagua na yupo madarakani; aanzishe vita kwa maslahi ya nani?" Tayari nilishakuwa na ulewa kwamba aanzishae vita ni yule anayeshindwa uchaguzi na hapo kupata jibu kwamba kumbe CCM wanachowaambia wananchi ni kwamba, wakichagua upinzani, wao CCM wataingia msituni!!
Nakiri kwa nafsi huku Mungu akiniona na anipe adhabu yoyote ikiwa nitakuwa naongea uongo! Hapo zamani, niliamini CCM wasingeweza kufanya hivyo hata kama kweli wanashindwa uchaguzi! Kinyume chake hivi sasa; kila ninapoangalia wanavyong'aninia umeya Dar es salaam... ikiwa na maana kwamba hawakubali kuiacha Dar es salaam; ndipo hivi sasa najiuliza ikiwa kuiacha Dar es salaam tu ni kwa mbinde namna hii; je ni kweli hawa watu wanaweza kuwa tayari kuiacha nchi nzima?! Nikachanganya na yale ya Zanzibar shaka yangu inaongezeka maradufu.
- CCM mnanitisha
- CCM mnanitia hofu
- CCM mnanifanya nifikirie ni-conclude kwamba amani tuliyonayo nchi mwetu haitokani na CCM bali inatokana na upinzani kukubali kushindwa bila kujali ikiwa ni kushindwa huko ni kwa halali au hapana!
- Ikiwa kuachia mkoa mmoja wa Dar es salaam mnaona taabu hadi mnafikia hatua ya kufoji hadi hati za mahakama; hivi kweli mtakuwa tayari kuachia mikoa yote 26 nyinyi?!