Uchaguzi wa Marekani: Namwunga mkono Ron Paul

Uchaguzi wa Marekani: Namwunga mkono Ron Paul

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,700
Reaction score
1,857
Nakumbuka, nilishabikia sana uchaguzi wa Marekani uliopita. Nilikuwa nalala usiku wa manane kufuatilia maendeleo ya kijana wetu, Barak Obama. Ila hivi sasa sitaki kusikia hata jina lake. Huyu jamaa- kama Mk...re- amewakatisha tamaa sana watu waliokuwa wakimsapoti. Sijui hakufahamu kuwa watu wengi walimwunga mkono kwa sababu ya kutarajia hataendeleza au kuanzisha vita duniani. Yote hayo yamekuwa matarajio hewa, hasa wakati huu mazungumzo ya kuishambulia Iran yakikoa moto.
Kwa upande wa pili, ameshindwa kabisa kugeuza dira ya Marekani, na kwa kweli haidhuru ameukuta uchumi wa Marekani katika hali mbaya, si makosa kusema yeye ameongezea kudidimia kwake.
Akichaguliwa tena, si tu kwamba twaweza kushuhudia vita ya III ya dunia, bali Marekani itakoma kuwa kiongozi wa kiuchumi duniani. Itabaki kuwa dola kubwa kwa miaka 10-15 ijayo kwa sababu tu ina silaha kali, kama vile ilivyokuwa Soviet Union, lakini si kwa kitu kingine.
Laiti kama Uchina ingekuwa na idadi ndogo ya watu, basi ingeipiku Marekani kwa pato la mtu na hata la taifa kwa muda mfupi sana.
Kwa vile nilikuwa nikimsapoti kwa kutarajia atatoa picha nzuri ya watu weusi, na angalau atawasaidia watu weusi wa nchini kwake ambao wanazidi kunyanyaswa na kuonewa (Zaidi ya Wamarekani milioni 2 wako jela, wengi wakiwa weusi), na kwa vile hakufanya lolote .......mimi naona RON PAUL ndiye kiongotzi mwenye dira nzuri ya kuikwamua Marekani kutokana na matatizo yake. Ni dhahiri kuwa bajeti ya Ulinzi, security nk na misaada isiyo mpaka kwa Israel (political, financial and military) ndiyo mambo mawili makubwa yanayoikausha (draining) Marekani. RON PAUL anaahidi kuondoa vituo vyote vya Majeshi ya Marekani nje ya nchi (takriban 180) na ku deal na Israel kama nchi nyinginezo duniani, ingawaje ataisapoti katika kuilinda. Aidha, hataanzisha vita nyingine isipokuwa kama nchi ya Marekani itashambuliwa.
Naona huyu ndiye anayetufaa kwa amani ya dunia, na pia kwa uchumi wa Marekani. Kwani kutetereka kwa uchumi wa Marekani kunatudhuru sote.
 
Hiki kibabu japokuwa napenda jinsi anavyojenga hoja na kwa jinsi misimamo yake isivyobadilika (toka miaka ya sabini) lakini kwa jinsi watu wa stormfront wanavyompenda sana inanifanya wakati mwingine nijiulize maswali mengi.
 
Hongera kwa kukifanyia endorsement hicho kibabu; labda utakiongezea kura 2,3, ila ujue hakitashinda kamwe. Sera zake ni kama za mwota ndoto...haziko practical kabisa.
 
Nyie ngojeni huyo OMERA atakavyowabamiza hao jamaa mpaka NN atakimbia janvi hili!!
 
Cjaona wa kupambana na mjaruo hapo?
 
Mie namuunga mkono Newt Gingrich kwa sababu ni msema kweli.
 
..i like Ron Paul's foreign policy.

..ila mtizamo wake wa kutaka ku-abolish Federal Reserve sikubaliani nao.

..vilevile rekodi na mtizamo wake kuhusu race unatia mashaka.
 
Hongera kwa kukifanyia endorsement hicho kibabu; labda utakiongezea kura 2,3, ila ujue hakitashinda kamwe. Sera zake ni kama za mwota ndoto...haziko practical kabisa.
Kitu gani si praactical katika sera za Ron Paul? Si ukiseme tukijadili? Nahofi wewe ni katika wale wanaosikiliza FOX NEWS na kumeza ndoano, kibua na mshipi.
Nakuomba utumie uelewa wako na ufanye tathmini yako mwenyewe ukinyambua hotuba zake taangu miaka ya sabini.
 
..i like Ron Paul's foreign policy.

..ila mtizamo wake wa kutaka ku-abolish Federal Reserve sikubaliani nao.

..vilevile rekodi na mtizamo wake kuhusu race unatia mashaka.

Kama unafahmu Federl Reserve ni nini, na nani wanaimiliki, nipe sababu moj tu kw nini unaisapoti.
Juu ya race......yaonesha wazi umeathiriwa na negative media. Kwa ushauri wangu: unapoona media ya Marekani inamwandama mwanasiasa hicho ni kigezo kizuri cha kumsapoti. Kwani inamanisha hayuko mifukoni mwa........
 
Mimi michango yangu ya hela natoa kwa Obama na nitaendelea kutoa katika kampeni za mwaka huu. Ninyi wengine jiliwazeni na vizee vyenu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nilidhani waTanzania wanamuunga mkono Bush kwani alileta msaada wa dawa za ukimwi na vyandarua... Hivi Bush hagombei tena kama yule Komandoo wa Russia..?🙂
 
Nilidhani waTanzania wanamuunga mkono Bush kwani alileta msaada wa dawa za ukimwi na vyandarua... Hivi Bush hagombei tena kama yule Komandoo wa Russia..?🙂

Bush aliishia kuingiza nchi vitani, hivyo hawezi gombea akashinda. "Komandoo" amesaidia sana Urusi, hivyo ni wazi atashinda despite the western propaganda.
 
Hapa swala sio kumtetea Obama coz ni mweusi mwenzangu. But kwa mtu anayejua kufatilia mambo na mwenye upeo, hili swala liko wazi. Obama amechemsha sana. Hata sisi tuishio uku USA tunaliona hilo. Uongozi wake umekuwa kama sharobaro wetu Jk. Na pia naweza Sema, marekani ikiendelea hivi, next few years haitakuwa leading economy country anymore
 
Obama anapita kiulaini tu...Obama will create more jobs ....Labda hujafatiliia news tu mana juzi saud arabia ka sign na mmarekani auziwe ndege F15 hapo ni 29Billion.

Yani watu 5000 wanapata kazi hapo.

Na klla Iran akitingisha kibiriti ndo Obama anafurahia mana USA ataingia kwenye vita.

Na katika Hiistory za kimarecan nchi ikiwa kwenye vita Presdent Obama will probably get reeleted.
 
Jaman tuwe tuna2nza kumbkumb,wakat obama anaapa maneno aliyoyasema,ataisimamia,kuilnda na kuitetea katiba ya malekan na si vinginevyo.Najua mlikua mnadhan atapingana kabsa na bush,mmalekan yeyote lazma afuate katba,sio km viongoz wa tz.ukikiuka katiba lazma upindulwe.
 
Namuunga Mkono Mitt Romney kwenye primary. I want him to meet Obama in General
 
Subirini kampeni za kitaifa zitakapoanza ndio mtakapoona watu watakavyokuwa "Fired Up" na Jaluo!.
 
Back
Top Bottom