Mimi napenda ya kibongo kwa sababu yametengenezwa kwa kuzingatia mazingira ya Kibongo.
Yanahimili mikiki mikiki na bara bara zetu mbovu kuliko mengine..
Hata ikitokea ukaligongesha kwenye gari nyingine haliharibiki sana kiasi cha kukuacha kwenye mataa.
Ya Ulaya hayako stable sana hasa kwa tabia yetu ya uendeshaji, yanachemsha haraka.
Ukiyagongesha na mengine hesabu umeumia, hayana uvumilivu kabisa, very delecate.
Ya Kijapani hali kadhlika, kwanza ni malaini kuliko hata ya Ulaya, na hayana kabisa uvumilivu wa mazingira yetu..
Hayana uwezo wa kubeba mizigo mikubwa, vinginevyo utaliua kabla ya siku zake..
Naungana na mkuu Kiduku kuwa kama huna uwezo wa kumiliki gari bora kuendelea na Taksi, ikiwezekana kuomba lift kwa wengine.
Ingawa lift za mara kwa mara siyo nzuri sana, kama una haraka bora ukamate Taksi na lift iwe option ya pili kama ikijitokeza bila wewe kulazimisha.
Ingawa Taksi siku hizi zinonekana kuwa hatari kwa usalama, hivyo tuzipande at awa ouni riski...