NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,840
- 5,096
Uchaguzi mkuu ulifanyika nchini Liberia mwaka 1927.Katika matokeo mshindi alikuwa bwana Charles D.B King wa chama cha True Whig, alichaguliwa kwa kipindi cha tatu baada ya kumshinda mpinzani wake bwana Thomas J.R.Faulkner wa chama cha watu yaani People's Party.Kabla ya hapo Faulkener alikuwa ni meya wa jiji la Monrovia na alifanya kampeni maalum kwa ahadi kuwa atarekebisha sheria za kazi Labor law.
Uchaguzi huo ulionekana ni uchaguzi ambao ulionekana kama uchaguzi ambao haujawahi kutokea duniani kwa wakati huo na hadi sasa bado rekodi haijavunjwa ulikuwa na ukiukwaji mkubwa.Ulivunja rekodi ya Guinnes wakati huo hadi sasa.
Ilikuwaje basi
Wapiga kura waliojiandikisha walikuwa 19,000 tu nchi nzima wakati huo Liberia ilikuwa na watu wachache sana lakini ajabu sasa bwana King alishinda kwa idadi ya kura za wapiga kura za 248,000 na mwenzake Faulkner alipata kura 9000.
Kwa hesabu ya kawaida maana yake Faulkner alipata kura asilimia 47% kama utachukua 9000 ugawe kwa 19,000 uzidishe kwa 100.Ila mwenzake mshindi bwana King alipata asilimia 1,305% endapo utachukua 248,000 ugawe kwa 19,000 uzidishe kwa 100.
Je kulitokea nini?
Yaliyojiri baada ya uchaguzi, Faulkner alitupia lawama wanachama wa chama cha The True Whig Party na serikali yake kwa kutumia watumwa na kuuza watumwa Kwenda kisiwa koloni la Hispania visiwa vya Fernando po Pamoja na kuhusisha jeshi katika kadhia hiyo, Pamoja na serikali kukataa na kugoma kutoa ushirikiano,umoja wa mataifa wakati huo iliitwa League of Nation walianzisha kamati ya uchunguzi kama kuna utumwa unaendelea Liberia na watu kufanyishwa kazi kwa nguvu huko Liberia chini ya uenyekiti wa mwanasheria mwingereza Chuthbert Christy kuangalia ukubwa wa tatizo.Raisi wa Marekani wakati huo Herbert Hoover alisimamisha uhusiano kwa muda na Liberia ajili ya kadhia hiyo.
Mwaka 1930 repoti ya kamati ilitolewa japo haikutoa Ushahidi wa chaji ya biashara ya utumwa na watu kulazimishwa kufanya kazi iliiweka maofisa wa serikali kitimoto,kwa kuwatia hatiani raisi bwana King na makamu wake wa raisi bwana Allen Yancy kwa kujipatia faida kutokana na utumwa .Pia kulikuwa na pendekezo Liberia kuweka chini ya baraza la udhamini.Matokeo yake baraza la wawakilishi walianza kumshughulikia King,ambapo kwa haraka sana alijiuzulu nafasi yake ya uraisi Nafasi yake ilichukuliwa na bwana Edwin Barclay. Faulkner Faulkner aligombea tena uchaguzi wa 1931 lakini hakushinda kiti chake tena.
Picha chini ni picha ya mwamba bwana Charles D.B King.Raisi wa 17 wa Liberia toka mwaka 1920
Alizaliwa tarehe 12 March 1875 na kufariki tarehe 4 September 1961.
Rais
wa kwanza mweusi Liberia alikuwa ni bwana Joseph Jenkins Robert alizaliwa mwaka 1809 na kufariki 1876