TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uanze miezi kadhaa iliyopita, tumeshuhudia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ikijitahidi kufanya kazi zake kwa kiwango cha kuridhisha, kinyume na ilivyokuwa huko nyuma. Tume hiyo mara hii imejitahidi kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni husika, kiasi cha watu wengi kujiuliza kama kweli hii ndiyo Tume waliyoijua miaka ya nyuma.
Katika chaguzi nyingi ambazo tume hiyo ilizisimamia miaka ya nyuma, wananchi walishuhudia vituko, mizengwe na kasoro nyingi zilizotokana na udhaifu wa tume hiyo ambayo, kwa kiasi kikubwa, ilionekana kuegemea upande mmoja tu wa chama tawala. Kutokana na tume hiyo kuonekana kama imejisalimisha kwa dola na chama tawala kwa kupokea amri na maelekezo kuhusu uendeshaji na utoaji wa maamuzi mbalimbali, wananchi walikosa imani siyo tu na tume hiyo, bali pia na mchakato mzima wa chaguzi hizo.
Tumefuatilia kwa makini tangu matayarisho ya uchaguzi huo mkuu wa mwaka huu yalipoanza hadi hivi sasa na kugundua kuwepo kwa ufanisi mkubwa kwa upande wa tume hiyo katika nyanja kadhaa muhimu. Kwanza, uandikishaji wa wapiga kura ulifanyika kwa uwazi, pasipo ubaguzi na katika mazingira yaliyowezesha zoezi hilo kuweka rekodi ya kuandikisha idadi kubwa zaidi ya wapiga kura kuliko wakati mwingine wowote. Tume ilihakikisha vifaa vinavyohitajika vinapatikana na vituo vya kujiandikisha vinaongezwa na vinapatiwa wafanyakazi wa kutosha.
Pili, tume hiyo ilifanya uteuzi wa wagombea kwa kufuata haki na matakwa ya vyama vilivyo katika kinyanganyiro cha kugombea urais, ubunge na udiwani. Na pale ambapo baadhi ya wagombea walioteuliwa na vyama walishindwa kurejesha fomu au kupata wadhamini, tume hiyo haikusita kuwaengua kama taratibu na kanuni zinavyotaka.
Tatu, tume hiyo pia ilizishughulikia kwa haki na umakini mkubwa pingamizi dhidi ya wagombea kwa kuhakikisha kwamba inazitupilia mbali zile zisizokuwa na msingi. Hii ilisaidia kuwarejesha ulingoni wagombea wote waliokuwa wamewekewa pingamizi kwa sababu za kisiasa, fitna au majungu.
Tungependa kuipongeza tume hiyo ya uchaguzi kwa kazi yake nzuri mpaka sasa, kwani kazi iliyo mbele yake ni kubwa mno. Kwa kuvitendea haki vyama vyote pasipo ubaguzi, tume inaweka misingi na mfumo endelevu utakaoendesha shughuli zake na siyo tu kuzifanya chaguzi zote zitakazofanyika kuwa huru na haki, bali pia kuwafanya wagombea wakubali matokeo. Hii inawezekana kwa sababu tume hiyo imeona umuhimu wa kuondokana na utamaduni wa kukipendelea chama tawala na sasa imeacha demokrasia ichukue mkondo wake.
Lakini pamoja na kutoa pongezi hizo, ingefaa tume hiyo ifahamu kwamba mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu bado unaendelea, hivyo isibweteke. Tunaishauri sasa isimame kidete na ihakikishe kwamba wagombea katika ngazi zote wanapewa fursa ya kufanya kampeni pasipo bughudha au vikwazo ilimradi wanafuata sheria na kanuni zilizokubaliwa baina ya vyama vyao na tume yenyewe. Tungependa kuona kwamba vyama au wagombea wanaokiuka sheria, taratibu na kanuni hizo wanachukuliwa hatua bila woga wala upendeleo.
Ni wajibu wa Tume pia kuhakikisha kwamba kampeni hizo zinafikia kilele katika hali ya amani na salama, kwa maana ya wananchi kupiga kura katika mazingira huru. Wagombea na mawakala wao washilikishwe katika zoezi la kuhesabu kura na wapiga kura waachwe washuhudie zoezi hilo huku wakifuata sheria na taratibu zilizowekwa.
Uwepo wa utitiri wa askari wenye silaha katika vituo vya kupigia kura utaleta hofu, na tunalipongeza Jeshi la Polisi nchini kwa kuahidi kwamba kamwe askari wao hawatakaribia vituo hivyo wala kubeba silaha za kivita eneo hilo siku hiyo ya kupiga kura. Sisi tunaiombea Tume kheri na fanaka katika kazi yake hiyo