Uchaguzi Senegal unatufundisha muunganiko wa Mahakama na nguvu ya umma

Haikuwa rahisi kwa mgombea wa upinzani Bw. Bassirou Diomayo Faye kushinda Urais nchini Senegal. Nasema haikuwa rahisi kutokana na hali ya kisiasa iliyokuwepo nchini humo hasa Rais anayemaliza muda wake Bw. Macky Sally alipotaka kubadili Katiba ili aendelee kuongoza muhura wa tatu.

Mwaka 2021 Rais Macky Sally alijaribu kutaka kubadilisha Katiba ili angombee muhura wa tatu katika uchaguzi mkuu wa 2024. Upinzani uliitisha maandamano ya kupinga mchakato huo ambao wengi waliutafsiri ni wa kibinafsi na tamaa ya madaraka ya Rais Macky Sally.

Wapinzani walianza kukutana na mkono wa vyombo vya dola mamia yao wakakamatwa na kufungwa jela ili angarau kupunguza joto la upinzani, lakini bado joto lilikuwa kubwa. Kiongozi mkuu wa upinzani Bw. Ousmane Sonko na mshirika wake Bw. Bassirou Diomayo Faye na wafuasi wengine 300 walikamatwa na kufungwa jela huku internet ikiwa imezimwa nchini kote na chama chao cha siasa kikafutwa. Kitendo hicho kiliamsha zaidi hisia za wananchi wa Senegal maandamano yakawa makubwa zaidi kiasi kwamba zoezi la Rais kubadili katiba likakwama.

Baadaye Rais Macky Sally akasogeza uchaguzi mkuu mbele kwamba ufanyike December 2024 badala ya March 2024. Mahakama ya juu nchini Senegal Supreme Court ikatupilia mbali takwa hilo la Rais kusogeza uchaguzi mbele kwamba linakiuka Katiba na ni batili. Pamoja na mahakama kutupilia mbali takwa hilo wananchi waliendelea kuandamana wakitaka tarehe ya uchaguzi kutangazwa huku wakitaka wapinzani waliopo jela waachiliwe.

Rais Macky Sally hakuwa na chaguo akatangaza tarehe ya uchaguzi ambao ulifanyika juzi Jumapili 24 March 2024 na pia ndani ya saa 48 akawaachia wafungwa wote wa kisiasa akiwemo mpinzani mkuu Bw. Ousmane Sonko na mshirika wake wa karibu Bw. Bassirou Diomayo Faye.

Pamoja na kuachiliwa huru kwa wafungwa hao wa kisiasa lakini figisu ilifanyika kumzuia mpinzani mkuu mwenye ushawishi Bw. Ousmane Sonko kugombea uRais nchini Senegal. Lengo lilikuwa upinzani ukipata mgombea asiye na ushawishi basi chama tawala kitashinda kirahisi katika uchaguzi huo ambao tayari Rais Macky Sally alikuwa amemuandaa mrithi wake. Sonko aliliona hilo akaona isiwe tabu akamuunga mkono mshirika wake Bw. Bassirou Diomayo Faye kama mgombea wa uRais wa upinzani nchini humo. Sonko alizunguka na Faye katika maeneo yote ya Senegal akimuombea kura huku akiwaambia wananchi ukimchagua Faye umenichagua mimi. Kwa umoja wao wameshinda na Bassirou Diomayo Faye ndiye Rais mteule anayesubiri kuapishwa muda wowote kuanzia sasa.

Kwa hiyo Bassirou Diomayo Faye ameshinda uRais kwa sababu kuu mbili.

1. Mahakama ya juu Supreme Court ambayo ilitupilia mbali takwa la Rais kutaka kusogeza uchaguzi mbele kwamba ni batili na linakiuka katiba.

2. Nguvu ya Umma. Wananchi waliandamana kutaka uchaguzi ufanyike na wapinzani waliopo jela waachiliwe haraka kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza ili nao washiriki uchaguzi.

Kwetu mahakama imewekwa mfukoni na dola na kwamba hata jaji mkuu mwenyewe hana sifa za kikatiba yuko katika nafasi hiyo kwa fadhila za dola. Chombo pekee kilichobakia na matumaini ya kusimamia Katiba ni Jeshi la wananchi. Kwamba hata leo ikitokea nguvu ya Umma ikiamua basi pengine jeshi la wananchi ndio linaweza kusimama na wananchi lakini sio bunge wala mahakama.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Wanaojifanya ni wapinzani mnakuwa na wasemaji wapuuzi kama Lema na Mdude unategemea nini?
 
Ugunduzi mwingi dunini umefaywa na Retired professors supervising doctorate/post-doc students......(kama ni msomi google ujielimishe)
iyo ni mada ingine
mbona huu upinzani wetu haungundui chochote after kuwa retired
 
Hata aliyeondoka alikuwa ni mpinzani aliyeshinda uchaguzi wa 2019.
Hata hawa wa sasa watakengeuka tu!
 
iyo ni mada ingine
mbona huu upinzani wetu haungundui chochote after kuwa retired
1. Upinzani siyo retird, ni very active
2. Upinzani wamegundua/wamebuni mengi sana eg how to fight for their rights, ndiyo maana ccm inatumia dola kuwa madarakani knowing nguvu ya upinzani ni kubwa through chadema.
3. Kitendo cha CCM kukataa Tume huru ya uchaguzi tells a lot for thinking people with regard to upinzani in Tanzania

have a nice day
 
Hili ndio jambo linalofanya nizidi kuamini, wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu mustakabali wa mataifa yao, viongozi wa vyama vya siasa hasa wapinzani ni wasimamizi tu wa kuwezesha mabadiliko hayo.

Hapo bila wananchi kusimama kwa pamoja, inawezekana leo hii Faye pamoja na chama chake wote wangekuwa gerezani, lakini kwa maamuzi ya wananchi wa Senegal, wamemtoa Faye kifungoni wakampeleka mpinzani ikulu.

Hapa lazima tukubaliane, kususia kushiriki uchaguzi mkuu ndio njia ya kwanza kujimaliza kisiasa, na kuzidi kujichelewesha kuyafikia malengo yetu ya kujikwamua na tawala dhalimu. Hapa niwapongeze Chadema waliona mbali.

Kinachotakiwa kufanyika, kwanza chaguzi lazima zifanyike na wapinzani wenye malengo washiriki, baada ya hapo haki ya wananchi kumchagua wamtakaye lazima itekelezwe, hili lazima lifanyike kwa gharama yoyote, bila kujali wala kuogopa vitisho vya polisi au chama dola, hiki ndio kitovu cha mabadiliko, na wananchi wakisimamie.

Mbinu za kuanzia msituni au mapinduzi ya kijeshi ni mbinu zilizopitwa na wakati, wananchi ndio wenye nchi na maamuzi ya mwisho juu ya hatma zao na vizazi vyao. Kulisubiri jeshi kuamua hatma yetu, ni uzembe wetu, lazima tuijue starting point yetu, nayo ni kushiriki uchaguzi zote za kisiasa, na sio kuzisusia.

Tunajifunza hapo kwa Faye, bila nguvu ya umma inawezekana hata mahakama ya juu ya Senegal ingekubaliana na uamuzi wa Sall kuongeza muda wa kufanyika uchaguzi, lakini baada ya majaji wa Supreme Court kuiona nguvu ya umma, hawakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na kile wananchi wa Senegal wanachotaka, kumbe majaji hupindisha sheria kwa kuwaogopa watawala bila nguvu ya umma.

Kumbe basi, hata hizi mahakama zetu tunazoziona kila siku hazifai, zimetekwa na watawala bado sisi wananchi tunaweza kuzikomboa kama tukiamua kwa dhati kufanya hivyo, kumbe wale majaji wanajipendekeza kwa watawala kwasababu wanaiona kula yao mikononi mwa CCM, lakini tukiwaonesha kula yao ipo mikononi mwa kusimamia haki, wataachana na CCM dakika hiyo hiyo, waongozane na umma.

โ€ข Nguvu ya mageuzi yoyote kisiasa, inaanzia na kuishia mikononi mwa wananchi, viongozi wa vyama vya siasa ni wasimamizi tu wa kuwezesha kuyafikia mageuzi hayo, tusipobadilika tutaendelea kuwalalamikia CCM miaka yote na brazaj alishawahi kusema CCM sio chama cha kutangaza injili.
 
Sio kwa tanzania hii, werevu wachache ni keyboard warriors, majuha mengi ni majitu ya kuunga juhudi, hata juhudi hakuna wao ni vipofu wanaenda waliposhikwa mkono.

Nishaikatia tamaa tanzania yetu.
 
upinzani wenyewe wa kuaminika Tanzania uko wapi

huu wa siku mbili una omba maridhiano

huu wa kelele hata kuendesha vyao vyao tu hawawezi

kabla ya kuilaumu mahakama tujiangalie na wapinzani kweli tuko vzr ama porojo mingi
Upinzani imara Tz upo ila sheria na Katiba zimekipa Chama tawala haki zote za kufanya siasa wanavyotaka !
Ila wapinzani wanadhibitiwa katika nyanja nyingi !
Hiyo iko wazi na kila mwenye akili anajua hivyo. !
Hata haki ya kufanya maandamano imekuwa ni kama imetolewa kwa hisani ya Mheshimiwa Rais !
Tuwe wakweli tu maana Ukweli utatuacha huru !
Hii ni Nchi yetu sote !
Na siasa sio uadui !
Tafakari ! ๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Hili ndio jambo linalofanya nizidi kuamini, wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho kuhusu mustakabali wa mataifa yao, viongozi wa vyama vya siasa hasa wapinzani ni wasimamizi tu wa kuwezesha mabadiliko hayo.

Hapo bila wananchi kusimama kwa pamoja, inawezekana leo hii Faye pamoja na chama chake wote wangekuwa gerezani, lakini kwa maamuzi ya wananchi wa Senegal, wamemtoa Faye kifungoni wakampeleka mpinzani ikulu.

Hapa lazima tukubaliane, kususia kushiriki uchaguzi mkuu ndio njia ya kwanza kujimaliza kisiasa, na kuzidi kujichelewesha kuyafikia malengo yetu ya kujikwamua na tawala dhalimu. Hapa niwapongeze Chadema waliona mbali.

Kinachotakiwa kufanyika, kwanza chaguzi lazima zifanyike na wapinzani wenye malengo washiriki, baada ya hapo haki ya wananchi kumchagua wamtakaye lazima itekelezwe, hili lazima lifanyike kwa gharama yoyote, bila kujali wala kuogopa vitisho vya polisi au chama dola, hiki ndio kitovu cha mabadiliko, na wananchi wakisimamie.

โ€ข Mbinu za kuanzia msituni au mapinduzi ya kijeshi ni mbinu zilizopitwa na wakati, wananchi ndio wenye nchi na maamuzi ya mwisho juu ya hatma zao na vizazi vyao. Kulisubiri jeshi kuamua hatma yetu, ni uzembe wetu, lazima tuijue starting point yetu, nayo ni kushiriki uchaguzi zote za kisiasa, na sio kuzisusia.

Tunajifunza hapo kwa Faye, bila nguvu ya umma inawezekana hata mahakama ya juu ya Senegal ingekubaliana na uamuzi wa Sall kuongeza muda wa kufanyika uchaguzi, lakini baada ya majaji wa Supreme Court kuiona nguvu ya umma, hawakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na kile wananchi wa Senegal wanachotaka, kumbe majaji hupindisha sheria kwa kuwaogopa watawala bila nguvu ya umma.

Kumbe basi, hata hizi mahakama zetu tunazoziona kila siku hazifai, zimetekwa na watawala bado sisi wananchi tunaweza kuzikomboa kama tukiamua kwa dhati kufanya hivyo, kumbe wale majaji wanajipendekeza kwa watawala kwasababu wanaiona kula yao mikononi mwa CCM, lakini tukiwaonesha kula yao ipo mikononi mwa kusimamia haki, wataachana na CCM dakika hiyo hiyo, waongozane na umma.

โ€ข Nguvu ya mageuzi yoyote kisiasa, inaanzia na kuishia mikononi mwa wananchi, viongozi wa vyama vya siasa ni wasimamizi tu wa kuwezesha kuyafikia mageuzi hayo.
Kumbe ulikuwa hujui hivyo ??!!
 
Kumbe ulikuwa hujui hivyo ??!!
Kuna wakati huwa mawazo yanabadilika hasa nikifikiria wao wana risasi sisi hatuna, wao wana mabomu ya machozi sisi hatuna, basi ndio nikawa naiona safari ya mabadiliko yetu kisiasa bado iko mbali sana, kumbe risasi na mabomu ya machozi haviwezi kuishinda nguvu ya umma.
 
Upinzani imara Tz upo ila sheria na Katiba zimekipa Chama tawala haki zote za kufanya siasa wanavyotaka !
Ila wapinzani wanadhibitiwa katika nyanja nyingi !
Hiyo iko wazi na kila mwenye akili anajua hivyo. !
Hata haki ya kufanya maandamano imekuwa ni kama imetolewa kwa hisani ya Mheshimiwa Rais !
Tuwe wakweli tu maana Ukweli utatuacha huru !
Hii ni Nchi yetu sote !
Na siasa sio uadui !
Tafakari !
Usivilaumu sheria na katiba kukibeba chama tawala, maamuzi ya wananchi hasa kwenye sanduku la kura yatakayoambatana na nguvu ya kuyalinda yapo juu ya sheria na katiba.
 
๐—จ๐—ฐ๐—ต๐—ฎ๐—ด๐˜‚๐˜‡๐—ถ ๐—ฆ๐—ฒ๐—ป๐—ฒ๐—ด๐—ฎ๐—น ๐˜‚๐—บ๐—ฒ๐˜๐˜‚๐—ณ๐˜‚๐—ป๐—ฑ๐—ถ๐˜€๐—ต๐—ฎ ๐—บ๐˜‚๐˜‚๐—ป๐—ด๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ธ๐—ผ ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐—ฎ๐—ต๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ๐—บ๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ป๐—ด๐˜‚๐˜ƒ๐˜‚ ๐˜†๐—ฎ ๐—จ๐—บ๐—บ๐—ฎ

Bassirou Diomayo Faye ameshinda uRais kwa sababu kuu mbili.
Kwamba mahakama imeungana na Umma kuleta mabadiliko ya Siasa? enhe

Nguvu ya Umma. Wananchi waliandamana kutaka uchaguzi ufanyike

na wapinzani waliopo jela waachiliwe haraka kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza ili nao washiriki uchaguzi.
Mdude alisha achiwa bana Mdude, na itoshe mzee wetu Kinana alishatolea ufafanuzi suala hili la 'Wafungwa wa Kisiasa' kupitia "maridhiano" tena baada ya kuingilia michakato ya Kimahakama, ikiwa ina maana wameingilia uhuru wa mahakama-mtindo huo sio endelevu. Itoshe hamuwezi nyie CHADEMA kutoa lawama kwa CCM ikiwa wote mmehusika kuingilia mhimili wa Serikali.
 
Upinzani imara Tz upo ila sheria na Katiba zimekipa Chama tawala haki zote za kufanya siasa wanavyotaka !
Ila wapinzani wanadhibitiwa katika nyanja nyingi !
Hiyo iko wazi na kila mwenye akili anajua hivyo. !
Hata haki ya kufanya maandamano imekuwa ni kama imetolewa kwa hisani ya Mheshimiwa Rais !
Tuwe wakweli tu maana Ukweli utatuacha huru !
Hii ni Nchi yetu sote !
Na siasa sio uadui !
Tafakari ! ๐Ÿ™๐Ÿ™
hizo nchi nyingine sheria zao zikoje

kenya tumeona hadi kubadili katiba kupata sheria nzuri ilikuwaje

ukikaa usubiri serikali ikupe sheria nzuri za kuitoa madarakani utasubiri sana na haiwezekani
 
Mdude anakuzidi ana akili kichwani. He can fight for his right, He can resist uonevu and the like!!
Mwambie kabisa kuwa Mdude ni kijana anayejitambua na hawezi kulamba makalio ya wakubwa.
Wengi wanaobeza hapa ni watu wakujipendekeza kama ilivyo kanuni ya CCM kuwa kujipendekeza na kuabudu kwa viongozi ni wajibu.
Hawa wako radhi kuwatoa hata wake zao ili kiongozi wa ccm aburudike na wakajisikia fahari

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
nguvu ya umma unaitoa wapi bila kua na hoja ๐Ÿ’
Mahakama ifanyaje sasa, na huweza thibitisha malalamiko yako ๐Ÿ’
Halafu imagine mvuta bangi, mtu wa mitusi kama huyu Mdude_Nyagali yuko kwenye cream ya vijana wenye akili (thinktank) ya CHADEMA!!

Hawa eti ndiyo wanahubiri "nguvu ya umma"
 
Back
Top Bottom