Uchaguzi 2020 Uchaguzi mwaka huu 2020 waweza kuwa ACT Wazalendo vs CHADEMA

Hakuna mwaka ambao upinzani ni rahisi kuchukua serikali kama mwaka huu. Ni wao kuchanga karata vizuri. Na wakitaka kufanikiwa wote wakubali na kumpitisha Lissu kuwa mgombea wao mwaka huu.

CCM wanajua fika bora wakutane na Kifo ila sio Lissu. Membe ahadi ya kupewa uwaziri mkuu inamtosha, kikubwa wajiandae tu kumtumia kufanya reformation TISS kwa uzoefu wake
Naam
 
zitto hawezi kugombea urahisu kamwe coz anajua hatochaguliwa.na atapotea kisiasa mazima co mkaka. yote hii yee atagombea ubunge tu tuu had atakapohakikisha chama kimekuwa kikubwa ndpo atagombea urahid
 
ACT Wazalendo imedhamiria kuona Membe anagombea upinzani iwe kwa tiketi ya umoja wa upinzani (ACT+CHADEMA) au ACT peke yake.

CHADEMA haina mpango na mgombea kutoka nje ina wagombea wa kutosha mpaka sasa 6 washachukua fomu na matarajio ni wagombea zaidi ya 10 kuchukua fomu.

Katika namna hiyohiyo CHADEMA imeonesha kutokutilia manani sana muungano wa vyama. Hivyo uwezekano wa vyama kuungana ni mdogo mno.

Kwakuwa Membe anapenda kugombea Urais na kwa ushawishi wa Zitto na ACT atajikuta anagombea kupitia ACT Wazalendo na CHADEMA ikamteua Lissu basi uchaguzi utakuwa ni ACT vs CHADEMA
Chadema itakuwa n na nguvu kidogo kuliko ACT; ask me why; Iachane na kupeana viti kienyeji tu bali kila mtia nia agombee kiti anachokitaka, ila baadaye atakayeshinda kiti hicho aungwe mkono na wanachedama wote. Naona kama ACT inakula makombo ya CHADEMA 2015 ambayo CDM haiko tayari kuyarudia.
 
Hakuna mwaka ambao upinzani ni rahisi kuchukua serikali kama mwaka huu. Ni wao kuchanga karata vizuri. Na wakitaka kufanikiwa wote wakubali na kumpitisha Lissu kuwa mgombea wao mwaka huu.

CCM wanajua fika bora wakutane na Kifo ila sio Lissu. Membe ahadi ya kupewa uwaziri mkuu inamtosha, kikubwa wajiandae tu kumtumia kufanya reformation TISS kwa uzoefu wake
Kweli kabisa, membe awe mgombea mwenza
 
Back
Top Bottom