William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
QUOTE:
"Kwa haraka haraka,
1. Ridhiwani, aligombea ujumbe wa kuiwakilisha Bagamoyo, kwenye Mkutano Wa Halamashauri Kuu ya CCM, Taifa kwa jina la kizungu NEC."
Mzee Said Yakub,
Nimekusikia mkuu, kwanza ninashukur kwamba hatimaye umeamua kuja mzima mzima, as opposed na zamani ulipokuwa ukitumia yale majina yako kunishambulia na kunitukana, shukrani kwa hilo na ninakukaribisha kwa mikono miwili ili tuendeleze ile mijadala mingi ambayo tuiliachia njiani, I am looking forward to that,
kuhusu huu mjadala, ninaomba unipe muda kidogo, maana kama nilivyosema kwenye kichwa cha hiyo post kuwa niliandika kwa haraka haraka, sasa ninaweka vitu pamoja na ninakuja, na kama ulivyoniomba kwenye pm tuwe na mijadala ya kisomi!
Ahsante Mkuu!
Quote:
"lakini connections have to be worked on and be accurate, remember one rule of reporting is CROSS CHECKING THE INFO,".......As a person with legal bias and a journalist by profession nafahamu umuhimu wa research and rebuttals, hivyo take your time mkuu Komandoo"
Mzee Yakub, ahsante kwa ushauri wako mzuri, lakini una walakini kidogo maana mimi sio a journalist by profession, kwa hiyo sielewi umuhimu wa research na rebuttals, ndio maana huwa si-take my time na sina huo mpango in the furture!
Na pia bado ninakurudia kwenye hoja izngine hapo juu, subira tu mkuu!
Ahsante Mkuu, na heshima mbele!
Quote:
"3. Mheshimiwa hapa kidogo idadi ya wanachama wa Kamati Kuu umeichanganya kidogo, Kamati Kuu ina wajumbe 35 na Halmashauri Kuu ina wajumbe 215 tu. Hii figure ya 100 nadhani ndio zile lapses tulizozungumzia kwenye role ya JF lakini nadhani tuwe makini katika kutoa facts as hizi errors sometimes zinaepukika..."
Ninaomba nianze na hoja yako ya msingi, kuhusu credibility ya tunayoyasema, kwenye post niliyomjibu mjumbe kuhusu kamati na halamashauri za CCM, niliweka bayana mwanzoni mwa post kuwa ninajibu kwa haraka, haraka, meaning kwamba kunaweza kuwa na makosa, kwa mtu yoyote aliyeenda shule, hiyo ndio hasa maana kunadika kwa haraka haraka, na ninaamini kuwa wewe umeenda shule na ulinielewa.
Katika usahihisho wako umesema kuwa, wajumbe wa Kamati Kuu ni 35, ukweli ni kwamba ulikuwa unajaribu kuidanganya hii forum, tena kwa makusudi makubwa, maana wajumbe wa kamati kuu ni 36, kama ninavyoleta uthibiti hapa chini, na hii ni kwa sababu safari hii sikuandika kwa haraka haraka, ila nilikaa chini na kuweka vitu, ukweli ni huu chini:-!
WAJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (2002-2007)
1. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mwenyekiti
2. Ndugu John Samwel Malecela - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Philip Mangula - Katibu Mkuu
5. Brig. Gen. Hasan Ngwilizi - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Frederick Tluway Sumaye - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Ndugu Salome J. Mbatia - Mjumbe
14. Ndugu Jackson W. Msome - Mjumbe
15. Ndugu Omar Ramadhan Mapuri - Mjumbe
16. Ndugu Pius Msekwa - Mjumbe
17. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
18. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
19. Ndugu Amina Salum Ali - Mjumbe
20. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
21. Ndugu Pindi Chana - Mjumbe
22. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
23. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
24. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
25. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
26. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
27. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mjumbe
28. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
29. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
30. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
31. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
32. Ndugu Kingunge Ngombale-Mwiru - Mjumbe
33. Ndugu Juma Suleiman Nhunga - Mjumbe
34. Ndugu Salim Ahmed Salim - Mjumbe
35. Ndugu Abiud Mugini Maregesi - Mjumbe
36. Ndugu Yussuf Mohd Yussuf - Mjumbe
Ahsante Mkuu wangu na tutaendelea, ila in the meantime, talking about credibility, tunashukur sana kwamba umeamua kuingia mzima mzima, kama ulivyo, sisi wananchi wa hii forum, tungependa sana uyaweke sawa yote yaliyojiri kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa wa-Tanzania huko London, uchaguzi ambao wewe ulishiriki kama mgombea wa cheo hicho, baada ya uchaguzi tumesikia mengi sana yanayokuhusisha wewe binafsi na outcome ya uchaguzi huo,
Ndugu yangu do you mind kuligusa hilo, lakini nitaelewa uki-decline, maana tunazo data nyingi sana kuhusiana role yako kwenye outcome ya huo uchaguzi, ni vizuri tukapta nafasi ya kuchanganua na kupambanua, mchele ulipo na pumba ziko wapi?
Ahsante Mkuu na tutaendelea!
Quote:
Next time usisome udaku no body will care as of now, Just CRYING BABIES!, hakuna maziwa hapa kuna mawe tu Take it or leave it, next time nenda Uhuru na Mzalendo, upate za uhakika zaidi!
Kwa haraka haraka,
1. Ridhiwani, aligombea ujumbe wa kuiwakilisha Bagamoyo, kwenye Mkutano Wa Halamashauri Kuu ya CCM, Taifa kwa jina la kizungu NEC.
2. NEC = National Executive Commitee, yaani Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ambayo kazi yake ni pamoja na kuishauri kamati kuuu ya CCM, na pia kushughulikia na kuzichambua ishus inazopewa na Kamati kuu ya CCM.
3. Kamati Kuu ya CCM, au Executive Committee pia huitwa Central Committee, ni kikao chenye kauli ya mwisho kuhusu maamuzi mengi ya CCM, lakini pia mwenyekiti wa CCM, anayo power ya kui-overrule kamati hiii na pia Halmashauri kuu, kitu ambacho Mkapa alikuwa akikifanya mara nyingi na kwa makusudi, akitumia ubabe na hii power!
kamati hii ina wajumbe 100!
Mimi naona huu mjadala umeenda beyond putting the record straight. Now, let me try kwenye hizi points tatu za Mzee wetu ES:
1. Mzee ES anasema "Ridhiwani, aligombea ujumbe wa kuiwakilisha Bagamoyo, kwenye Mkutano Wa Halamashauri Kuu ya CCM, Taifa kwa jina la kizungu NEC"
Well, (a) Ridhiwan Kikwete hakugombea kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC); (b) Wilaya (kwa hapa inaongelewa Bagamoyo) huwa hazina wawakilishi kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa kwahiyo hata kama Ridhiwani angekuwa anagombea ujumbe huo wa NEC, asingegombea "kuiwakilisha" Bagamoyo. Taarifa sahihi ni kwamba: Ridhiwani anaomba kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM, ambao hufanyika mara mbili katika miaka mitano. Katika Mkutano huu Wilaya zote nchini huwakilishwa na wajumbe tisa. Kati ya hao, wengine wanaingia automatically kwa vyeo vyao (kama vile Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya na Katibu wa CCM wa Wilaya) na wengine inabidi ugombee. Sasa Ridhiwani ndio anagombea moja ya nafasi hizo. Na wachaguaji ni Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya.
2. ES amesema kwamba "NEC = National Executive Commitee, yaani Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ambayo kazi yake ni pamoja na kuishauri kamati kuuu ya CCM, na pia kushughulikia na kuzichambua ishus inazopewa na Kamati kuu ya CCM"
Ni kweli Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM huitwa NEC. Lakini kazi yake sio kuishauri "Kamati Kuu ya CCM" kama anavyosema ES (actually, hii inaitwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa"). In fact, it is the other way round. NEC ndio hu-endorse au kukataa maamuzi ya Kamati Kuu. In fact, Kataraiya hakufukuzwa na Kamati Kuu. Halmashauri Kuu ilikubali mapendekezo ya Kamati Kuu ya kumfukuza. At the same time, Halmashauri Kuu inaweza kukasimu madaraka kwa Kamati Kuu ili i-act haraka kwa baadhi ya mambo kwa kuwa yenyewe hukutana kila mwezi wakati Halmashauri Kuu hukutana kila baada ya miezi mitatu.
2. ES anasema "Kamati Kuu ya CCM, au Executive Committee pia huitwa Central Committee, ni kikao chenye kauli ya mwisho kuhusu maamuzi mengi ya CCM, lakini pia mwenyekiti wa CCM, anayo power ya kui-overrule kamati hiii na pia Halmashauri kuu, kitu ambacho Mkapa alikuwa akikifanya mara nyingi na kwa makusudi, akitumia ubabe na hii power! kamati hii ina wajumbe 100!"
Inawezekana kweli Kamati Kuu iitwe Executive Commitee halafu tena iitwe Central Committee wakati tumekwisha-establish kwamba Halmashauri Kuu ndio Executive Commitee?
Kusema Kamati Kuu ndio kikao chenye kauli ya mwisho, sio sahihi. Kikao chenye kauli ya mwisho ni Mkutano Mkuu wa Taifa. Hata hivyo, kwa kuwa Mkutano Mkuu wa Taifa hufanyika mara mbili kila baada ya miaka mitano, kikao cha maamuzi makubwa ni Halmashauri Kuu ya Taifa. Kinachowatisha watu tu ni kwamba Kamati Kuu ina-comprise the most powerful people lakini ultimately lazima Kamati Kuu ipeleke mapendekezo NEC, hapo ndipo maamuzi mengi hujadiliwa na kufanyika. Kwenye huu mchakato wa uchaguzi, kuna watu walipitishwa na Kamati Kuu lakini Halmashauri Kuu ikawakataa na kuwa watu walikataliwa na Kamati Kuu lakini wakatetewa na Halmashauri Kuu na wakapita.
Hii habari ya kwamba Kamati Kuu ina wajumbe 100 nadhani mtoa hoja amesahihisha na kusema kuwa ina wajumbe 36, ingawa kuna mjumbe mwingine anasema ina wajumbe 35. Mimi sijui. Lakini inawezekana mjadala hapa ni je, mwenyekiti yumo kwenye hiyo hesabu?
Nadhani huu ufafanuzi utakuwa umetoa mwanga. Heshima ya Forum mbele!
Mzee Mugongox2, heshima mbele mkuu ila sina sbabu ya kuwapa watu faida kwa kulumbana na wewe, kwa hiyo ninakupa ushindi!
Mzee Said Yakub,
Nilifikiri kuwa baada ya kuja mzima mzima, utakuwa umebadilika tabia, lakini ninaona spirit ni ile ile kama ulipokuwa TTJ, una lako jambo, karibu mkuu, ila kwenye hii ishu nimeamua kumsikiliza Mzee Bob. Mkandara, kwa hiyo sitawajibu tena, unless ikibidi tu!, so far sioni sababu!
Isipokuwa get ready na uchaguzi wa uliopita wa London, maana nina data zako wewe mwenye na u-candidate wako fake! nakula pumzi kwanza!
Heshima mbele wakuu!
Evidence based arguments- Ila real life arguments are a function of values and facts or values only!Kwa watakaosoma maelezo yako kuhusu Ridhiwani Kugombea ndani ya CCM na ufafanuzi wako wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu watapata picha mchele upi na usio mchele ni upi....
At least a third party amefafanua vizuri na kuweka wazi.
Mimi ndio nimeweka hapa kwamba Kamati Kuu ina wajumbe 35 na sikukurupuka nimetoa hapa:
http://www.ccmtz.org/0kamatikuu.htm na katika kuangalia jina la Mwenyekiti wa chama Jakaya Mrisho Kikwete lipo.
Hii ya wajumbe 36 hata wengine wamenitumia kwenye PM wakisema hivyo lakini sijui kwanini official website ya chama ionyeshe wajumbe 35!
Hawa 36 sina hakika Komandoo ES amewatoa wapi....ingawa kama nilivyosema majina ni yale yale more or less na yale ya wajumbe 36 ila Mzee ndio hivyo tena kaghafilika kutoa source!