Lihakanga
JF-Expert Member
- Dec 17, 2016
- 4,829
- 6,376
Hongereni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa.
Naomba nitoe wito kwenu kutonielewa vibaya kwa uzi huu. Lengo langu ni kupata ukweli ili kwa pamoja kama taifa tuone nini kifanyike ili matokeo ya uchaguzi hasa uchaguzi mkuu yawe ni "real ballot paper outstanding" badala ya figisufigisu na mizengwe.
Natamani mwenye ujuzi hasa na nini hufanya matokeo yasiwe yasiyotarajiwa hasa aseme ni wapi pana tatizo, ni uelewa wa wapiga kura? Ni mawakala hurubuniwa wasaini matokeo yasiyo ya kweli? Au karatasi zina miujiza ya kubadili kura aliyopigiwa mgombea hubadilika kuwa ya mwingine?
Je, ni karatasi za matokeo hubadilishwa na kujazwa matokeo fake? Na kama ndivyo ni wakati gani matokeo hubadilishwa?
Lakini kwa upande wa pili sasa, nini kifanyike kuepuka matokeo fake?
Hatuwezi kuacha kupiga kura kwa kukata tamaa ya kile kinachotajwa kuwa wizi wa kura. Yafaa kutafuta ufumbuzi kwa tafiti za kisayansi juu ya namna ya kupata ufumbuzi wa wizi wa kura usiojulikana na kila mwaka mchawi hapatikani.
Natazamia mjadala wa busara kama wanaJF walivyo.
Asanteni na karibuni.