Uchaguzi 2020 Uchaguzi mkuu: Nini hutokea na matokeo?

Lihakanga

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
4,829
6,376
Hongereni kwa majukumu ya ujenzi wa Taifa.

Naomba nitoe wito kwenu kutonielewa vibaya kwa uzi huu. Lengo langu ni kupata ukweli ili kwa pamoja kama taifa tuone nini kifanyike ili matokeo ya uchaguzi hasa uchaguzi mkuu yawe ni "real ballot paper outstanding" badala ya figisufigisu na mizengwe.

Natamani mwenye ujuzi hasa na nini hufanya matokeo yasiwe yasiyotarajiwa hasa aseme ni wapi pana tatizo, ni uelewa wa wapiga kura? Ni mawakala hurubuniwa wasaini matokeo yasiyo ya kweli? Au karatasi zina miujiza ya kubadili kura aliyopigiwa mgombea hubadilika kuwa ya mwingine?

Je, ni karatasi za matokeo hubadilishwa na kujazwa matokeo fake? Na kama ndivyo ni wakati gani matokeo hubadilishwa?

Lakini kwa upande wa pili sasa, nini kifanyike kuepuka matokeo fake?
Hatuwezi kuacha kupiga kura kwa kukata tamaa ya kile kinachotajwa kuwa wizi wa kura. Yafaa kutafuta ufumbuzi kwa tafiti za kisayansi juu ya namna ya kupata ufumbuzi wa wizi wa kura usiojulikana na kila mwaka mchawi hapatikani.

Natazamia mjadala wa busara kama wanaJF walivyo.

Asanteni na karibuni.
 
Mpaka umeandika andiko hili una uelewa kuhusu hicho ulichokiandika, tuambie kwanza kwa uelewa wako wewe unaona nini badala ya kutusukumia sisi, what is your position?
 
Mpaka umeandika andiko hili una uelewa kuhusu hicho ulichokiandika, tuambie kwanza kwa uelewa wako wewe unaona nini badala ya kutusukumia sisi, what is your position?
Ninafikiri ili kupata matokeo sahihi ya uchaguzi yenye kumchagua tumpendae tufanye haya:

Kwanza kujiandikisha kupiga kura na kuwa na shahada zetu muda wote na kupiga kura kwa dhati siku ya tukio.

Kujua tunachokihitaji yaani kumchagua uliyemsikiliza na kuelewa sera zake badala ya kutumia uzoefu au kufuata mkumbo.

Wale wanaopewa dhamana ya uwakilishi kwenye kuhesabu kura wawe na uelewa wa jukumu hilo na kuwa na msimamo thabiti katika kusimamia uhesabiaji kura.

Kwa upande mwingine, wasimamizi wa uchaguzi wasiwe na msimamo wa kichama. Tume ya uchaguzi ichuje na kujidhirisha na wasimamizi. Tena wasiwe watumishi wa umma kwani ni rahisi kuegemea kwa mwajiri wao (serikali inayokuwa madarakani).

Naomba na wewe uongeze mawazo yako hapa.
 
Back
Top Bottom