Uchaguzi mdogo mwingine wanukia...

Hivi katika historia ya Tanzania, kuna Mbunge alishawahi kujiuzulu Ubunge ?
Mkuu uko mbali na historia na hata matukio.Aliyewahi kujiuzulu ni Rostam Aziz aliyekuwa Mbunge wa Igunga.Jihabarishe ndugu..
 
wabunge wengi walifuata pesa kama ajira sio uwakilishi .
kilicho fanywa na utawala wa bunge ni kibaya sana wabunge wote walikopeshwa pesa kuanzia za posho na mikopo ya magari wameshachukuwa kwa sasa wanaenda bungeni kama mnavyoona wanachokifanya hamna ni ndiooo na kulala tu wachache wenye mioyo ya dhati kuwasaidia wa tz utawaona hata hoja zao za msingi lakini ukiangalia wengi wao wanaenda tu kutimiza siku wewe angalia bunge likianza
 
Uchaguzi unaonukia saaaaana na tunausubiria kwa hamu ,ni wa S E G E R E A".
 
Nani alimtuma kugombea. mijitu mingine kama hawakui vile.
 
Tetesi zingine bana mbona ubunge unalipa kuliko hata hizo biashara zake.Halafu ukiwa mbunge na biashara ndo inachochea kwa kulindwa na jina la mbunge sasa wewe na hiyo habari yako imekaa kiuzushi zaidi
 
Nimeshazoea kuitwa mzushi humu JF ndugu.Nilishawahi kutoa habari kuwa madaktari wangegoma tena,nikaitwa mzushi.Wakagoma tena.Tusubiri tuone..
 
Mimi uchaguzi ambao najua unanukia kama pafyumu ya Beyonce ni wa jimbo la Gairo. Mbunge wa jimbo hili anasema biashara zake za mabasi zinadidimia kwasababu ya kutumia muda wake mwingi mjengoni Dodoma.

hahaaa alidhani Ubunge ni sehemu ya kuongeza Income yake?
 
Ndo maana wana shauri wafanya biashara waachane na siasa, nadhani aliiingia katika siasa kwa manufaa ya biashara zake. Let him step down, Lol!
 
kumbe Makinda aliwahesabu hawa mwisho wa siku tutawajua wote
 
Tatizo watanzania hatutofautishi kati ya kuchagua mbunge, kuchagua hela, na kuchagu mfadhili. Ndo maana tajiri akiingia ulingoni anapigiwa kura bila kujali kama ana muda wa kuwatumikia? Wenzangu waluguru wa Moro mjini mbunge wao yuko busy muda wote lakini ametenga basi moja bovu kusaidia kwenda kuzika, ole wao wamuombe asaidie kupeleka mgonjwa hospitali anawatoa baru. Eti kipaumbele ni kuzika na sio kuponya
 
Huenda ni kweli kwa kuwa huyu bwana ana Makampuni kama kumi hivi!

Makampuni kumi????????????????

Ama kweli ufisadi ulishatandaga kitambo!
Mtu mmoja makampuni kumi kweli hii ndiyo Tanzania yetu!
 
Rorya na Shinyanga mjini pia wbunge wanata kujitoa
Mimi uchaguzi ambao najua unanukia kama pafyumu ya Beyonce ni wa jimbo la Gairo. Mbunge wa jimbo hili anasema biashara zake za mabasi zinadidimia kwasababu ya kutumia muda wake mwingi mjengoni Dodoma.
 
JF inanuka umbea umbea tu , nadhani ni wakati sasa wakujiunga na magazeti ya shigongo !

Sidhani kama ataachia ngazi, kwa jinsi alivyotumia gharama kubwa na uchakachuaji alafu leo kirahisi tuu!
 
Mimi uchaguzi ambao najua unanukia kama pafyumu ya Beyonce ni wa jimbo la Gairo. Mbunge wa jimbo hili anasema biashara zake za mabasi zinadidimia kwasababu ya kutumia muda wake mwingi mjengoni Dodoma.

wewe mwanamke unatafutia watu ban hapa wewe ni gamba la mamba au kobe tuu
 
Kwani alipogombea alidhani kuna nini huko?

Haya ndiyo mambo ya kukimbilia Magogoni ukifikiria kuna biashara kumbe kuna matatizo mengi sana kwa mtu mwadilifu na mnyofu. Ni bora awaachie watu waadilifu wafanye kazi.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…