Uchaguzi mdogo majimbo ya Ukonga na Monduli: CCM yashinda majimbo yote!

Ni kama wananchi wepoteza ari ya kupiga kura kuchagua viongozi wao!!

Katika maeneo mengi niliyobahatika kufika leo hali ni mbaya sana namna muitikio wa wananchi ulivyo chini mno.

Watumishi wa tume ya uchaguzi na wanausalama (Polisi) ndio wanaoonekana zaidi vituoni kuliko walengwa ambao ni wananchi wa Ukonga!

Kinachoendelea tangu asubuhi ni watendaji hawa kujipigisha stori wenyewe kwa wenyewe bila kuwa na kazi yoyote ya kufanya!

Kwangu naona kwa namna siasa za nchi hii zinavyoendelea kuna hatari huko mbele (2020) chaguzi zikawa na wapiga kura 0 kabisa vituoni.

Kwa maono yangu huu ni upotevu mkubwa wa rasilimali muda na fedha na niiombe serikali iliangalie hili kwa jicho sahihi ili kama hakuna ulazima basi tusipoteze fedha na huo muda kufanya chaguzi zisizo na ulazima.
IMG_20180916_131913.jpg
 
Chadema imegeuka chuo cha kutengeneza uzushi ,uongo na uzandiki.

Wamepoteza mvuto kwa wananchi sasa wanajaribu kuzusha kila aina ya uongo kutafuta huruma ya wananchi.

Hovyo kabisa
 
Chadema imegeuka chuo cha kutengeneza uzushi ,uongo na uzandiki.

Wamepoteza mvuto kwa wananchi sasa wanajaribu kuzusha kila aina ya uongo kutafuta huruma ya wananchi.

Hovyo kabisa
Nahatimae ccm imeshinda sasa,tumekuelewa
 
Wakuu heshima yenu,

Leo ni siku ya uchaguzi katika Majimbo ya Ukonga na Monduli pamoja na kata 9 za Tanzania bara,

Naomba tupeane updates hapa ili dunia ijue kinachojiri.

Kama wewe ulipo panafanyika uchaguzi nenda kupiga kura ili kutumia haki yako. Kesho usijesema hutendewi haki.

Kumbuka watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Jimbo au Kata husika na wana kadi ya mpiga kura na wale walio wamepoteza kadi zao za kupigia kura au zimeharibika au zimechakaa watatumia Pasi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

====

UPDATES

DAR: Wasimamizi wa uchaguzi kituo cha Pugu Mnadani kata ya Pugu wamewaondoa vituoni mawakala saba wa Chadema, NLD na NCCR Mageuzi kwa maelezo kuwa hawana barua za utambulisho wa mtendaji wa kata.

Mgombea ubunge wa Ukonga kupitia CCM, Mwita Waitara amesema anashukuru amepiga kura ya ushindi.

Mgombea Ubunge wa CHADEMA Jimbo la Ukonga, Asia Daudi Msangi atapiga kura yake Kituo cha Kitunda Relini, Shule ya St. Lawrence, baadae majira ya mchana.

Waitara amesema hayo mara baada ya kupiga kura kwenye kituo cha Kerezange kilichopo Kivule asubuhi ya leo Septemba 16, 2018.

Mwitikio mdogo wa wapiga kura asubuhi hii, Waitara amesema ni kwa sababu jumapili ni siku ya ibada hivyo watu bado wapo makanisani.

Wanajua kuwa mwisho wa kupiga kura ni saa 10 jioni na sasa ni saa 4 asubuhi) bado wana saa sita za kupiga kura," amesema Waitara.

=>GARI LA MBUNGE WA CHADEMA LASHAMBULIWA KWA RISASI

Ni la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Anna Gidarya na limeshambuliwa akiwa katika kata ya Majengo

Waliofanya shambulio hilo hawajatambulika bado

Soma Monduli: Matairi ya gari ya mbunge wa Viti maalum Anna Giderya(CHADEMA) yamepigwa risasi - JamiiForums

=>MWENYEKITI NEC AKANA MAWAKALA WA CHADEMA KUZUILIWA

Baada ya CHADEMA kulalamika kuwa mawakala wake wamezuiliwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura Monduli, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage amekanusha na kusema mawakala wa nne wamekataliwa kwasababu wamekwenda tofauti na walioapishwa.
Yap,hata mwwnyekit wa tume amekili kua idadi ya watu nindogo haijapata kutokea
 
Na; Thadei Ole Mushi

Ni matarajio yangu kwa sasa wananchi wa Jimbo la Siha, Kinondoni na mengineyo ambayo wabunge wake walijiuzulu na kuhamia CCM pamoja na madiwani waliohama na kuhamia Ccm kwa asilimia mia moja wanakunywa maziwa na asali kwa sasa.

Ni matarajio yangu kuwa maisha yenu yamebadilika na mpo tofauti kabisa na majimbo ambayo wapinzani wanayoongoza kama vile Ubungo, Kibamba na Mengi mengineyo yanayoongozwa na UPINZANI.
Natarajia baada ya Mbunge wenu kuhamia CCM na kuchaguliwa tena anakimbizana na Shida zenu na mmeletewa maendeleo ambayo majimbo ya upinzania hawana.
Natarajia shida za maji mlizokuwa nazo awali zimeisha, Elimu ipo juu, Huduma za Mahospitalini zimebadilika, Barabara zimetandazwa lami au zimerekebishwa, Mna fedha kuliko wengine nk.
Kama bado haya hamjayapata na hali yenu bado ipo kama ilivyokuwa awali basi naweza kusema ninyi ni wajinga kuliko wsjinga wenyewe.
Na leo mnaweza kupata wajinga wengine waliojifunika na gunia la Demokrasia. Na jua Lote hili la Dar ulipanga Foleni 2015 kumchagua mtu huyu huyu na leo anakupangisha tena mstari na jua huku ukisubiri asali na maziwa Ukonga.
Nani ametuloga sisi watanzania? Nilichoshuhudia kwenye kampeni ni Sarakasi za hali ya juu toka kwa Mbunge wa Mbulu ndio kitu pekee nachoweza kusema nimefaidi.
Sijadikia watu wakiadress matatizo ya wananchi na kutafuta "How".
Tuanze kuwapima ambao walihama na kucjaguliwa tena je wamebadilisha nn? Mambo yako vile vile? Kama ndivyo huu si ujinga ni nn?
Pamoja na kupoteza kodi za wananchi waoneeni huruma hawa walalahoi mnaowatembeza na jua lote hili.
Wananchi wajingeze katika elimu ya uraia.....
Kuna wajanja wapo kivulini wanawacheka tu hihiii hiiiiii hahahahahah. Bado sana aisee waitara hanipangishi foleni acha uccm wangu muutilie tu shaka ila nitaendelea kupinga hii dhana ya Hama na Gombea tena.....
Ifike mahali sisi Vijana wa ccm tuliotumia Kodi za nchi kusomea tuwasaidie wannchi katika baadhi ya Mambo.
Ole Mushi.
0712702602
 
Inasikitisha sana!! nchi yetu imefikia hapa kwasababu ya kikundi fulani cha chama cha siasa kinataka kutawala milele...
 
Binafsi nachukia sana maamuzi ya ndiyooooooooo! hata kwenye mambo hatari
 
Watu wanasubiri matokeo, foleni zimeisha muda mrefu
 
Back
Top Bottom