Uchaguzi mdogo majimbo ya Ukonga na Monduli: CCM yashinda majimbo yote!

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Wakuu heshima yenu,

Leo ni siku ya uchaguzi katika Majimbo ya Ukonga na Monduli pamoja na kata 9 za Tanzania bara,

Naomba tupeane updates hapa ili dunia ijue kinachojiri.

Kama wewe ulipo panafanyika uchaguzi nenda kupiga kura ili kutumia haki yako. Kesho usijesema hutendewi haki.

Kumbuka watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye Jimbo au Kata husika na wana kadi ya mpiga kura na wale walio wamepoteza kadi zao za kupigia kura au zimeharibika au zimechakaa watatumia Pasi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

====

UPDATES

DAR: Wasimamizi wa uchaguzi kituo cha Pugu Mnadani kata ya Pugu wamewaondoa vituoni mawakala saba wa Chadema, NLD na NCCR Mageuzi kwa maelezo kuwa hawana barua za utambulisho wa mtendaji wa kata.

Mgombea ubunge wa Ukonga kupitia CCM, Mwita Waitara amesema anashukuru amepiga kura ya ushindi.

Mgombea Ubunge wa CHADEMA Jimbo la Ukonga, Asia Daudi Msangi atapiga kura yake Kituo cha Kitunda Relini, Shule ya St. Lawrence, baadae majira ya mchana.

Waitara amesema hayo mara baada ya kupiga kura kwenye kituo cha Kerezange kilichopo Kivule asubuhi ya leo Septemba 16, 2018.

Mwitikio mdogo wa wapiga kura asubuhi hii, Waitara amesema ni kwa sababu jumapili ni siku ya ibada hivyo watu bado wapo makanisani.

Wanajua kuwa mwisho wa kupiga kura ni saa 10 jioni na sasa ni saa 4 asubuhi) bado wana saa sita za kupiga kura," amesema Waitara.

UPDATES

Dar es Salaam. Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na silaha kwenye vituo vya kupigia kura.

Wakati mtuhumiwa mmoja akikutwa na bastola aina ya glog yenye risasi 14, mwingine anasema amekamatwa akiwa na panga.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumapili Septemba 16, Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa hao waliingia vituoni kama mawakala. Hata hivyo alikataa kuwataja majina kwa madai kuwa bado wanachunguza tukio hilo.

“Huyu mwenye bastola alikuja na barua ambayo haina picha, lakini alipokuwa amekaa alishtukiwa na alipopekuliwa alikutwa na bastola hiyo,” amesema Mambosasa.

Akizungumzia hali ya uchaguzi, amesema ni shwari na hakuna vurugu zilizojitokeza tangu asubuhi. “Niwaambie Watanzania kwamba, uchaguzi huu utakuwa huru na wa haki na utamalizika salama. Niwasisitize waendelee kutii sheria za uchaguzi bila shuruti,” amesema Mambosasa.



=>GARI LA MBUNGE WA CHADEMA LASHAMBULIWA KWA RISASI

Ni la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Anna Gidarya na limeshambuliwa akiwa katika kata ya Majengo

Waliofanya shambulio hilo hawajatambulika bado

Soma Monduli: Matairi ya gari ya mbunge wa Viti maalum Anna Giderya(CHADEMA) yamepigwa risasi - JamiiForums

=>MWENYEKITI NEC AKANA MAWAKALA WA CHADEMA KUZUILIWA

Baada ya CHADEMA kulalamika kuwa mawakala wake wamezuiliwa katika baadhi ya vituo vya kupigia kura Monduli, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage amekanusha na kusema mawakala wa nne wamekataliwa kwasababu wamekwenda tofauti na walioapishwa.


===> MATOKEO UCHAGUZI MDOGO: CCM YAONGOZA, YASHINDA KATA TATU

Robson Kimarowa wa CCM atangwaza Diwani wa Kata ya Machame Uroki, mkoani Kilimanjaro kwa kupata kura 2,174 dhidi ya Kombe(CHADEMA) aliyepata kura 704

Aidha, Newton Mwajutobe wa CCM ashinda udiwani Kata ya Maanga, Mbeya kwa kupata kura 1897 dhidi ya Mwashilindi wa CHADEMA aliyepata kura 1,703

Katika matokeo mengine, Yohana Laizer wa CCM atangazwa mshindi wa udiwani Kata ya Kia, mkoani Kilimanjaro kwa kupata kura 1,367 dhidi ya Ibua wa CHADEMA aliyepata kura 230

UBUNGE:

Ukonga:
CCM: Kura 76,292
CHADEMA: Kura 8,072

Monduli:
CCM: Kura 65,714
CHADEMA: Kura 3,187

2985FC32-1A45-45DF-96C1-99716C878278.jpeg

MATOKEO YA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA MONDULI.

Julius Kalanga (Pichani) ametangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Monduli mkoani Arusha kwa tiketi ya CCM, baada ya kupata kura 65, 714 dhidi ya kura 3,187 alizopata mshindani wake Yonas Leiser wa CHADEMA.

Msimamizi wa Uchaguzi katika jimbo hilo Steven Ulaya ametaja matokeo ya wagombea wengine katika jimbo hilo kama ifuatavyo;-

Elizabeth Michael wa Chama cha Wakulima – Kura 16,

Wilfred Mlay wa ACT Wazalendo – Kura 144,

Francis Ringo wa ADA-TADEA – Kura 21,

Omary Kaigo wa DP – Kura 34,

Simon Ngirisho wa Demokrasia Makini – Kura 35,

Feruzy Juma wa NRA - Kura 45.

e7fba4ba-2d2a-4d71-8848-72b5aca48e0e.jpg
 
Leo ni leo.....lile zoezi muhumu linaloenda kuamua nani ni nani ukonga na monduli limeshaanza. vituo viko wazi tangu saa moja asbh na wananchi wamejitokeza kwa wingi vituoni kutekeleza haki yao ya msingi ya kupiga kura. Kuwa beneti na uzi huu kwa habari mubashara kutoka vituoni hadi matokeo
Hakuna leo ni leo, ni mavi tu hakuna kupiga kura bali KUIBA KURA. Mmeshaiba tayari kura. Msimami wa uchaguzi amekimbia bila kuwaapisha makada wa CDM
 
Tukae mkao wa kula, kushuhudia mabox ya kura yakiibiwa vituoni, tena "under escort" ya hawa "manjago" wetu??

Kwa kweli ubaya unaofanywa na serikali hii ya CCM hata shetani ambaye ndiye chimbuko wa mabaya yote duniani, anawashangaaa kwa kuwa mshamu-overtake!
 
Amkeni watanzania kuichagua ccm ni sawa na kunichagua mimi niwe mjumbe wa nyumba kumi ili hali nina akili timamu kuliko zile za amphd kumi wa ccm
 
Leo ni leo.....lile zoezi muhumu linaloenda kuamua nani ni nani ukonga na monduli limeshaanza. vituo viko wazi tangu saa moja asbh na wananchi wamejitokeza kwa wingi vituoni kutekeleza haki yao ya msingi ya kupiga kura. Kuwa beneti na uzi huu kwa habari mubashara kutoka vituoni hadi matokeo
Mnaoanzisha nyuzi muwe Mna uwezo wa kutoa updates kama huwezi Bora updates aunganishe na nyuzi nyingine ambazo waanzishaji wapo field
 
Back
Top Bottom