Naomba sana kuelemishwa juu ya uchaguzi wa Vijana wetu kuingia kidato cha tano. Mimi kijana wangu alipata daraja la kwanza ya pointi 9. Hii ina maana alipata A7, B1 na C1 lakini cha kushangaza amechaguliwa kozi ya Clinical Officer - Kilosa. Nilitegemea achaguliwe kidato cha tano - Shule Maalum. Swali la kuuliza Je huyu kijana ndiyo alichagua hiyo kozi au Serikali ndiyo imemchagulia?. Mimi sioni kama kuna haki hapa. Basi ngoja nimpeleke Feza Boys hata kwa gharama yeyote.