Uchaguzi Daruso

Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,452
Nasikia Uchaguzi wa DARUSO uliokuwa ufanyike leo umeahirishwa, naskia ni sababu za kisiasa, naomba mwenye datails azimwage hapa JF tumkome nyuni kweupeeeeeeeeeee
 
Ni kweli umeahirishwa lakini ulioahirishwa ni uchaguzi wa RAIS tu. Uchaguzi wa makamu wa Rais na wakuu wa mabweni unaendelea. Nafuatilia kujua sababu za kuahirishwa uchaguzi wa rais na nikizipata nitazieleza hapa
 
Nasikia Uchaguzi wa DARUSO uliokuwa ufanyike leo umeahirishwa, naskia ni sababu za kisiasa, naomba mwenye datails azimwage hapa JF tumkome nyuni kweupeeeeeeeeeee
Yah umeahirishwa na hii ni kutokana na wagombea wawili wamelalamika kwenye kamati kwamba mwenzao anapiga kampen za kuwapakazia.. kwa taarifa za wana JF ni kwamba mgombea Odong ambaye ni mganda ndiye anyrlalamikiwa na wenzake Mlowe na Juma..
Upepo wa uraisi inaonyesha unamuelekea Odong kwani wanafunzi wanamzungumzia na naonekana ndiye anyeweza kuwa raisi
Bt kampeni za Mwaka huu zimedorora sana kutokana na kutoruhusiwa kutumia vipaza sauti na k\mikusanyiko wakati wa usiku na hii inafanyta kiongozi kuchaguliwa kutokana na popularity yake ..
 
KAMPENI za kugombea nafasi ya urais katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), sehemu ya Mlimani zimetawaliwa na itikadi za vyama vya siasa pamoja na uzawa.

Hali hiyo ilishuhudiwa na Tanzania Daima jana, ilipotembelea chuoni hapo katika siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi huo unaofanyika leo, na kuelezwa kuwa baadhi ya wagombea wamegeuka kuwa kama mawakala wa vyama vya siasa.

Hali hiyo inatokana na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo, kutumia nafasi zao kuwanadi wagombea hao, huku wakiwapigia kampeni kwa kutumia madaraka yao.

Akizungumza na Tanzania Daima, mwanafunzi wa mwaka wa pili anayechukua masomo ya Biashara na Uongozi, Owawa Steven, alisema kuwa, anapinga kampeni za kuwania uongozi katika serikali ya wanafunzi kuchukua sura ya kampeni ya vyama vya siasa.

Alisema mmoja wa wagombea watatu wa nafasi ya urais (jina tunalo), anahusishwa kusaidiwa na moja ya vyama vya siasa nchini katika kampeni zake.

“Ninasema hivyo kwa sababu kuna wenye viti waliitwa Millennium Tower kupewa pesa ili wampitishe mgombea huyo. Pia mgombea huyo ametumia zaidi ya sh milioni sita kwenye kutengenezea mabango, kuchapishia makala na kukodishia ma-Fuso ambayo yamewekwa muziki mkubwa kwa ajili ya kampeni,” alisema Steven.

Wakati hilo likitokea, baadhi ya wanafunzi waliokerwa na hatua hiyo ya chama hicho cha siasa, wameazimia kumpa kura zao mgombea mmoja wa urais anayetoka nje ya nchi, ili kuepusha kuingia kwa masuala ya itikadi za vyama katika uongozi wa chuo kikuu hicho kikongwe kuliko vyote nchini, jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za chuo.

“Tumeamua kumpa mgeni kura zetu, kwa sababu anatetea haki ya wanafunzi. Aliteuliwa na uongozi kwa kuwa walifikiri kuwa hatapigiwa kura kwa sababu si raia, huku wakijua watu wao watachaguliwa,” alisema Steven.

Hata hivyo, mgombea anayetuhumiwa kuungwa mkono na chama hicho cha siasa, alipohojiwa kuhusu hilo, alikanusha akieleza kuwa hizo ni kashfa kutoka kwa wapinzani wake, ambazo anasema amejizatiti kukabiliana nazo.

“Nagombea hii nafasi nikitokea katika hali ya kawaida. Pia tuhuma kuwa mimi naungwa mkono na chama cha siasa, hilo mimi silijui na sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote. Kampeni zangu nazifanya na wanafunzi wenzangu ambao tunachangishana pesa kidogo kidogo kwa ajili ya kusukuma kampeni hii. Kumbuka ukiingia sehemu kwa kununuliwa hutafanya chochote,” alisema mgombea huyo.

Kwa upande wake, mgombea mwingine kutoka nje ya nchi alilieleza Tanzania Daima kuwa, kampeni zinaendelea vizuri kwa kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanamuunga mkono. Hata hivyo, mgombea huyo alilalamika akisema amekuwa akipata vitisho kutoka kwa watu asiowajua.

Alisema endapo atachaguliwa, moja ya mambo atakayofuatilia ni mradi wa Mlimani City, ili kujua unawanufaishaje wanafunzi wa UDSM, kwa sababu upo katika ardhi yao, lakini hawaoni faida yake.

“Ninasimama kwenye ukweli, ndiyo maana napata ushirikiano mzuri kutoka kwa wenzangu. Japo kampeni zinazoendeshwa zinanichafua na kusema kuwa nduli amerudi tena, lakini nashukuru kuwa nakubalika,” alisema.

Mgombea wa tatu aliyezungumzia suala hilo yeye alisema mazingira ya kufanya kampeni kwa mwaka huu chuoni hapo yamekuwa magumu tofauti na miaka iliyopita.

“Uchaguzi utakuwa mzuri kwa kuwa kampeni zimekuwa na ushindani. Hii ni changamoto kwetu sisi wagombea,” alisema mgombea huyo asiyehusishwa na kundi lolote.

Uchaguzi huo umekuwa ukilalamikiwa na wanafunzi mbalimbali kwa kuwa umekuwa na itikadi za kisiasa zaidi, kwani baadhi ya wanasiasa na watoto wao wameonekana wakimpigia kampeni au kuwa karibu na mgombea wa kwanza.

“Mtoto wa kigogo mmoja mkubwa serikalini, alionekana mara mbili chuoni hapa akiwa na mgombea huyo. Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni ya mchujo, alionekana chumba namba 1515, Hall 6,” alisema mmoja wa wanafunzi ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Wakati huo huo, Rais wa Daruso anayemaliza muda wake, Deo Daud alisema kuwa taratibu za uchaguzi chuoni hapo zinakwenda sawasawa, ila kampeni za mwaka huu zimekuwa na upungufu tofauti na miaka mingine, kwa kuwa hakukuwa na muda mrefu wa kufanya kampeni.

Leo wanafunzi wa UDSM wanamchagua rais wa serikali ya wanafunzi ambaye atakuwa madarakani kwa kipindi cha mwaka mzima. Kampeni hizo za rais zilianza Aprili 7, mwaka huu.

Wagombea wanaochuana katika kinyang’anyiro hicho ni, Odong’ Odwar, Juma Faustine na Mlowe Pesience.

Source: Tanzania Daima
 
Mliopo hapo Mlimani endeleeni kutupasha kwani hili suala la Vyama vya Siasa hususani CCM huwa wanapenda kuweka influence zake hapo chuo kwenye kipindi hiki cha Uchaguzi sasa inaoneka mwaka huu Mtu wao upepo unamwelekea Vibaya
 
mlioko hapo UDSM ongeeni kwa uwazi, nani antuhumiwa kufadhiliwa na chama gani?
 
mlioko hapo UDSM ongeeni kwa uwazi, nani antuhumiwa kufadhiliwa na chama gani?


Unafikiri ni chama gani chenye tabia ya kufadhili chaguzi, na kununua kura!? Hili si swali ndani ya TZ!! Muulize Mh. Juma Ngasongwa atakufahamisha.
 
Unafikiri ni chama gani chenye tabia ya kufadhili chaguzi, na kununua kura!? Hili si swali ndani ya TZ!! Muulize Mh. Juma Ngasongwa atakufahamisha.

Think Big unapenyeza ujumbe mzito sana .Mie nakusoma kwa mbali Mheshimiwa.Ngasongwa kachoka hata Ujumbe wa nyumba kumi sina hakika kama ataupata.Lakini anaweza maana Tanganyika ina maajabu .
 
hawa ndio mafisadi tunaowandaa kuiongoza tz ya kesho.
hivi hii tz yetu itapona kweli??
 
hawa ndio mafisadi tunaowandaa kuiongoza tz ya kesho.
hivi hii tz yetu itapona kweli??

Jamaa ananieleza kwamba Mkandara na CCM wanamtaka kijana apite na wameleta ubaguzi wa kumwiya Mganda badala ya kumuona kama ni mwanafunzi wa UDSM.Ndiyo shida hii wanalia hakuna ubaguzi lakini hapa wanaonyesha wazi wazi .
 
Yule waziri wa elimu ya juu alisema mahali kuwa viongozi wa wanafunzi ndio wanaleta vurugu vyuoni (soma kwamba serikali haitaki viongozi wa wanafunzi ambao ni safi na ambao wako active kutetea masilahi ya wanafunzi).

Katika hili sishangai kabisa kuwa Mkandara na wenzake watataka kuwa na kiongozi kama Maina Owino (just to get him on the spot light again) .... ambaye wanamtumia wanavyotaka na kuhakikisha kuwa analinda masilahi ya wakubwa na mafisadi na sio masilahi ya wanafunzi.
 
Back
Top Bottom