Uchaguzi Busanda: Majigambo, Uteuzi na Kampeni kuelekea uchaguzi

Mbona picha zinaonekana au nyie msioziona ndo hamjui namna ya kuzifungua.
Mpaka kieleweke. Na sisiemu wameshikwa pabaya mwaka huu?
TINGATINGA NALO LIMEGEUKA KUWA KIBAJAJI!!!!!!!!! kwi kwi kwi kwi!
 
hivi ni kweli hamzioni hizo picha au mmeamua kuanzisha ligi. Mbona ziko picha kama nane hivi tofauti, Au upepo mbaya umepita hapo kwenye Computer zenu
 
Wakuu samahanini sana niliziweka kumbe kutokana na matatizo ya kimtandao huku zikawa hazijatokea nimemtumia invisible na Mwanakijiji ili waziweke na nyingine nitaweka usiku pamoja na maelezo ya kina .

Mkiziona picha ya kwanza ni ya gari la polisi ambalo lilienda kumchukua diwani aliyekamatwa na kikosi cha CHADEMA jana saa saba usiku akiwa ananunua shahada kwenye kata ya busanda, ya pili ni diwani aliyekakamatwa na ya tatu ni balozi mmoja wapo aliyekamatwa akiwa ananunua shahada na alikutwa na shahada 17 za wananchi na alipohojiwa alisema kuwa wameagizwa na ngazi za juu.

Wameshikiliwa na sasa wametolewa kwa dhamana ila watafikishwa mahakamani.

Nyingine ni za mkutano wa Zitto kata ya Katoro juzi .

Mengine baadae kwanni huku umeme shida na jenereta wanawasha usiku tuu hivyo ni hadi usiku tena.



Jamani mbona hao madiwani unasema walikuwa wananunua shahada Wamechoka kiasi hiki!!!!! Hivi wanaelewa kwanza nini wanafanya au ni umasikini ndiyo unawaponza!!!! Au elimu duni inawaponza , maana kama umasikini halafu wangekuwa na elimu kidogo wangegundua kuwa They NEED CHANGES kujaribu na upande wa pili wa shilingi ili waone kama kweli wataendelea kuwa masikini kiasi hicho. Maana inaonesha hata chakula mchana hawajapata si kwa kutaka bali hali ngumu.

Busanda Show the Tanzania that : - Ili kukomesha IFISADI you need CHANGES, na ni sasa.
 
MPYA toka BUSANDA!
DIWANI wa CCM na barozi wawili wa Chama hicho wametiwa mbaroni na Chadema na kukabiudhiwa polisi walikuwa wakiendesha zoezi la kuandikisha watu wenye shahada kwa lengo la kuwatambua ili kisha wakazinunue shahada hizo.
 
Lengo la wapinzani ni kupata fursa ya kuongoza serikali na wakifanya jambo lolote la kufanikisha hili lengo shaka hakuna. tatizo linakuja kama wakifanya mambo ambayo ni kinyume na sheria kama mlivyoiba nyie kuiba fedha za umma ili mchaguliwe.....Laana tupu

Akina nani? Kufanya jambo lolote hata kama ni nkinyume na sheria?
 
Hii debate ya umri wa Malecela haina tija. As long as hakuna limit ya umri kwa mtu kuwa Mbunge na wananchi ( ambao kimsingi ndio waajiri wake) wanamchagua hakuna shida hapo.

After-all Malecela sio the oldest MP kule mjengoni kuna akina Kingunge, Mzee Shelukindo et al
 
Nimerekebisha 1st post na naamini sasa zinaonekana vema.
yes, sasa zinaonekana vizuri. Du kweli Busanda wana hasira, sasa inabidi wakaipigie kura chadema, siyo wafike kwa wingi kwenye mikutano halafu kura waipe CCM. Hapo itakuwa haina maana. Sasa CCM kwisha habari yao. ama kweli ngoma mdundo.
 
Naona picha zimetua sasa. Mr. Dow.. naona anakata ishu..lol

Maskini waTz kweli ni kondoo wasio na mchungaji..Hebu ona hata facial expressions zao zilivyochoka.
 
Malecela ashtakiwe kwa kutoa rushwa ya ahadi ya umeme ikiwa tu wananchi wataichagua CCM.
 
Hii nimeipata hivi punde, mods mkiona yafaa mtaiunganisha na zingine zinazowiana

:eek:

Makada wawili wa CCM, wamakamatwa na polisi katika vijiji viwili huko Busanda wakiwa katika harakati za kununua shahada za kupigia kura kutoka kwa wanachama cha upinzani.

Viongozi wa Chadema walipata taarifa za kufanyika kwa vikao vilivyoongozwa na madiwani katika kata na kuhudhuriwa na mabalozi wa nyumba kumi na kuitaarifu poklisi kuhusiana na njama hizo.

Polisi waliwasili katika maeneo kadhaa na kufanikiwa kuwatia nguvuni makada hao wa CCM wakiwa na orodha ya majina ya wafuasi wa upinzani waliokuwa wanataka kununua shahada zao za kupigia kura.

OCD wa Geita amethibitisha kuwakamata makada hao na kukionya CCM kuwa wanafuatilia kwa karibu mbinu zao zote chafu zinazolenga kuvuruga uchaguzi huo.

Mmoja wa makada waliokamatwa alikiri mbele ya polisi na viongozi wa chadema kuwa walikuwa wanatekeleza maagizo kutoka kwa mabosi wao, kama mkakati wa kupunguza kura za wapinzani ili CCM ishinde.

Makada wengine wa CCM walifanikiwa kukimbia.
 
Hii nimeipata hivi pode, mods mkiona yafaa mwaweza kuiunganisha na zinazoshabihiana...


Makada wawili wa CCM, wamekamatwa na polisi leo asubuhi katika vijiji viwili huko Busanda wakiwa katika harakati za kununua shahada za kupigia kura kutoka kwa wanachama cha upinzani.

Viongozi wa Chadema walipata taarifa za kufanyika kwa vikao vilivyoongozwa na madiwani katika kata na kuhudhuriwa na mabalozi wa nyumba kumi na kuitaarifu poklisi kuhusiana na njama hizo.

Polisi waliwasili katika maeneo kadhaa na kufanikiwa kuwatia bguvuni makada hao wa CCM wakiwa na orodha ya majina ya wafuasi wa upinzani waliokuwa wanataka kununua shahada zao za kupigia kura.

OCD wa Geita amethibitisha kuwakamata makada hao na kukionya CCM kuwa wanafuatilia kwa karibu mbinu zao zote chafu zinazolenga kuvuruga uchaguzi huo.

Mmoja wa makada waliokamatwa alikiri mbele ya polisi na viongozi wa chadema kuwa walikuwa wanatekeleza maagizo kutoka kwa mabosi wao, kama mkakati wa kupunguza kura za wapinzani ili CCM ishinde.

Makada wengine wa CCM walifanikiwa kukimbia.
 
Wanaina, Wanainuka, Wanaona haya hao!!!!!

Kweli SISIEM maji yamewafika shingoni, can imagine 2010!!!!!!
 
Hii ndio kampeni ya nyumba kwa nyumba aliyobuni mzee Tingatinga. hataki majukwaa tena bali ananegotiate na mpiga kura nyumbani kwake. Shahada inathaminishwa mwanangu. Kama we ni wa upinzani na hutaki kupiga kura, unachukua chako mapema na kujikausha. Kwenye mikutano unaongeza idadi ya watu wakati wakaati wa kupiga kura we unaendelea kula vijisent vyoko kutoka kwa mafisadi.
 
Hii ndio kampeni ya nyumba kwa nyumba aliyobuni mzee Tingatinga. hataki majukwaa tena bali ananegotiate na mpiga kura nyumbani kwake. Shahada inathaminishwa mwanangu. Kama we ni wa upinzani na hutaki kupiga kura, unachukua chako mapema na kujikausha. Kwenye mikutano unaongeza idadi ya watu wakati wakaati wa kupiga kura we unaendelea kula vijisent vyoko kutoka kwa mafisadi.

mhhhhh.. ama kweli mfa maji haachi kutapa tapa! lakini wangewahoji vyem ili wawaseme hao bosi zao walio watuma. huu nao ni ufisadi wa aina yake, yaani unamdhulumu mtu haki yake ya kupiga kura, kwa sababu tu ya umasikini wake damn!
 
Jamani kama kweli hao watapiga kura basi nahesabu CCM chaliiiiiiiiiiiii dah CHADEMA wamekula vichwa balaaa kitu nyomi kha!

Watoto wa uswahili ndo hapo huwa wakishangilia na kusema watu weweeeeeeeeeeeeee!!!!

Kwakweli inatia matumaini, na hasa mkakati wa kukamata hao mafisadi wa kununua shahada za watu waliochoka mbaya kwa ajili ya CCM hiyo hiyo ambayo tena watu wana tamani eti ishinde! Hai ingii akilini kwakeli
 
Back
Top Bottom