Uchaguzi 2020 Uchaguzi 2020 Zanzibar: Prof. Mbarawa vs Dr. Mwinyi, nani namba zinambeba?

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,660
15,744
Kama tunavyojua kuwa 2020 Dr Shein atakuwa anafikia muhula wake wa mwisho wa uongozi visiwani Zbar, kinyang'anyiro cha kumpata mrithi wake kinaweza kikatawaliwa na 'wababe' hawa wawili yani Dr Mwinyi na Prof Mbarawa.

Sasa nimekuja kwenu wachambuzi wa maswala ya siasa mtoe uchambuzi wenu kuwa nani namba zinambeba na nani kati ya hawa wawili anaweza kuibuka kidedea?

Karibuni.
 
Umetumwa? Mitihani ya chuo umemaliza? Acha upuuzi dogo. Pigania maisha yako.
 
Atawika mwenye sauti ya mwisho nae ni...... .....ndo atakae amua nani awe mgombea uraisi wa chama chetu.
.
 
Mkulu anamkubali sana Mbarawa, na atakuwa kwenye akili yake kuhusu huko visiwani. Lakini Wazee ndani ya Chama mda mrefu sasa wanamuandaa Hussein.

Lakini ni jambo sensitive sana kuwalazimishia wavisiwani kiongozi. Unaweza ukatumia ushawishi wako kama unao mkubwa tena na akili nyingi maana mara nyingi wao huwa tayari wanakuwa na watu wao wanapendekeza au kuwakubali.

JK aliweza kuwatuliza akamuacha Gharib na kumpa Shein. Lakini ilibidi Gharib apozwe kwa umakamu wa Jamhuri ya Muungano.

Wangazija wananguvu sana, kuruhusu mpemba haikuwa kazi rahisi. JK gwiji wa siasa. Shikamoo huko uliko
 
Back
Top Bottom