Salim Ahmed Salim

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
SALIM AHMED SALIM; MWANASIASA MWENYE AKILI, MTULIVU, WAZIRI MKUU MSTAAFU, MWANADIPLOMASIA MKONGWE NA CHAGUO LA NYERERE KAMA MRITHI WAKE ILA FITNA ZA WAZANZIBARI NA UNYERERE UKAMPONZA, IKAMFANYA ACHUKIWE NA KUGEUKA LULU ISIYO NA THAMANI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu -CMCA
Sunday- 1/1/2023 (Uzi wa kwanza 2023)
Marangu Kilimanjaro Tanzania.

Salim Ahmed Salim ni mwanadiplomasia mkongwe, mahiri na mwenye ushawishi mkubwa kwenye korido za diplomacy duniani.

Ni lulu ya siasa za mashuri ya kigeni, namanisha kuwa Salim ni mtu muhimu na mahiri kwenye maswala ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa, anaheshimika sana China, Umoja wa Afrika na Marekani.

Ndio mtu pekee Kutoka Afrika ambaye alitikisa dunia kwenye mchuano wa kumpata katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Mwaka 1981, Marekani na China zilivutana mpaka Dunia ikasimama.

Salim ni mwanasiasa mwenye heshima kubwa Tanzania, ni lulu ambayo siasa za fitina na uzanzibari zimemfanya kupotea kisiasa.

Dr Salim Ahmed Salim, alikuwa katibu mkuu wa 7 wa Umoja wa Afrika, akawa Waziri mkuu wa 4 wa Tanzania na akawa Waziri wa 8 wa Mambo ya nje wa Tanzania.

Dr Salim Ahmed Salim alizaliwa tarehe 23 January mwaka 1942, kwa sasa ana miaka 80, alizaliwa huko Zanzibar kwa mama mwenye asili ya kiarabu na kiafrika pamoja na baba mwenye asili ya kiarabu kutoka Oman aliyeitwa Sheikh Ahmed Salim Riyami.

Salim ana Masters ya masuala ya ushirikiano wa kimataifa kutoka chuo kikuu cha Columbia University.

Salim alisoma katika shule ya Lumumba huko Zanzibar na baadaye akaendelea na masomo yake ya shahada ya kwanza katika Chuo cha St. Stephen cha Chuo Kikuu cha Delhi huko India, na akapata shahada yake ya uzamili katika Masuala ya Kimataifa kutoka Shule ya Masuala ya Kimataifa na Umma katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York Marekani.

Salim alikua mwanaharakati wa wanafunzi miaka ya 1950 na kuwa mwanzilishi na Makamu wa kwanza wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Zanzibar wote.

Salim alikuwa na mke mmoja aitwae Amne aliyefariki tarehe 20 October 2020, Salim amebahatika kupata watoto 3 ambao ni Maryam, Ali na
Ahmed, ingawaje husemekana ana mtoto wa nje ambaye ni mwanamama waziri kwa sasa kwenye serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan, hata hivyo taarifa hizi hazijawahi kuthibitishwa popote.

Salim amekuwa Balozi nchini Egypt mwaka 1961 akiwa na miaka 19 tu na hivyo kuweka historia ya kuwa Mtanzania mwenye umri mdogo kuliko wote kuwahi kuwa balozi.

Salim amewahi kuwa pia balozi nchi za China, Cuba, Trinidad, Guyana n.k, alikuwa kijana mchapakazi na mtiifu mno kwa Nyerere.

Salim amewahi kuwa mwakilishi wa kudumu Umoja wa mataifa kuanzia mwaka 1970 Mpaka 1980 ambapo mojawapo ya mafanikio yake ilikuwa kuihakikishia China inapewa kiti cha kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Salim ni rafiki wa China.

Salim amewahi kuwa Waziri wa mambo ya Nje mwaka 1981 Mpaka 1984, alipokea nafasi hiyo kutoka kwa Mkapa, na alipo badilishwa alimuachia Mkapa tena.

Salim amewahi kuwa Waziri Mkuu wa 4 wa Tanzania mwaka 1984 mpaka 1985 na kuwa Waziri Mkuu pekee kutoka Zanzibar lakini pia aliyehudumu kwa muda mfupi kushinda wote, Uteuzi wake ulifuata baada kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu kipenzi cha Watanzania wengi, Edward Sokoine kufuatia ajali ya gari, Morogoro.

Salim aliuachia Uwaziri Mkuu mara moja baada ya aliyekuwa amemteua, Rais Mwalimu Nyerere kustaafu lakini pia kufuatia uchaguzi wa Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mzanzibar mwenzake lakini kutokea Unguja kushika rasmi kiti cha Urais.

Kufuatia uchaguzi wa Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais, Salim aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Salim anadai katika nyadhifa alizowahi kuzifurahia kuzishikilia kushinda zote ilikuwa ni ya uwaziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa kwani alikuwa na jukumu la kuwahudumia wanajeshi na kuhakikisha ulinzi wa nchi na mipaka yake ambayo anadai ilikuwa heshima kubwa sana kwake.

Mwaka 1989 mpaka 2001, Salim alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja Afrika na kuwa Katibu Mkuu aliyehudumu muda mrefu zaidi kushinda wote, Katika kipindi hiki, Salim alisimamia mikakati ya pamoja ya nchi za Afrika kufanikisha ukombozi kwenye nchi za Afrika Kusini na Namibia lakini pia kutatua migogoro mbalimbali ya kisiasa kwenye baadhi ya nchi.

Wakati akiwa mwanafunzi shule ya Sekondari Lumumba, Salim alishaanza harakati za kisiasa na alijiunga na vyama tofauti vya kisiasa vilivyokuwa na lengo la kuwapatia uhuru Wanazanzibar.

Mwaka 1985, wakati Mwalimu Nyerere aliyekuwa Rais kipindi hicho anajindaa kung'atuka, paliibuka mapendekezo ya wanasiasa watatu wa kumrithi ambao walikuwa ni Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Rashid Kawawa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu pamoja na Salim mwenyewe ambaye wakati huo alikuwa Waziri Mkuu.

Mwalimu Nyerere alisemekana kumtaka Salim amrithi huku baadhi ya wahafidhina kutokea Zanzibar na bara wakimpiga vita Salim vikali.

Sababu ya Salim kuanguka ilitokana na kugawanyika kwa wanasiasa huko Zanzibar, Kati ya liberator (walio tetea mapinduzi) na front line (waliotoka hizbur, vijana ambao hawakutoka ASP).

Mgawanyiko huu ulitokana na Siasa za Jumbe, Mwanzoni Jumbe aliutaka uraisi wa Tanzania, alipoona mambo yamekuwa sivyo alivyotegemea akarudisha siasa za fitina ndani ya Zanzibar, wakati anarudi alikuta CCM imeshagawinyika huko Zanzibar, vijana kutoka hizbur kama Maalim Self, Salim Ahmed Salim na kina Izack Sepetu walikuwa Tayari wameshapata nguvu ndani ya Chama.

Ikumbukwe vijana hawa walitoka nationalist (hizbur) yani wale wasio unga mkono mapinduzi, walijiunga na ASP na kuanza kupata nguvu.

Vijana hawa ndio walitumiwa na Nyerere kumuondoa Jumbe Zanzibar, katika Kipindi kile cha kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar, Hivyo wakati Salim anataka uraisi wengi walimtuhumu kuwa ni hizbur, yani wale Waarabu waliopinduliwa enzi za Shamte.

Ilisemekana kuwa Salim alitajwa kuwa mhafidhina wa Siasa za unyerere, pia alituhumiwa kuusika njama ya mauaji ya Karume, njama za kumuondoa Jumbe na kuidhibiti CCM ya wanamapinduzi, yani wale front line kuhodhi visiwa vya Zanzibar dhidi ya wanamapinduzi (liberator).

Hivyo walidai kuwa Salim ana unyerere, Hivyo kwakua walisalitiwa na Nyerere kupitia Jumbe hawakuwa Tayari kumuunga mkono, waliona kuwa Nyerere alitaka kufuta historia ya mapinduzi huko Zanzibar.

Jumbe aliporejea Zanzibar ili kujiongezea nguvu kisiasa baada ya kuona kushindwa huko bara alitaka kuwashughulikia wakina Salim kama alivyokuwa akifanya Karume, lakini asingeweza kwasababu Tayari kambi ya front line ilikuwa imeshahodhi sehemu kubwa ya siasa za Zanzibar.

Zanzibar ikapasuka vipande viwili, yani liberator na front line, front line ilitumiwa vyema na Nyerere kudhoofisha mipango ya Abood Jumbe, Mwaka 1983 Jumbe akangolewa madarakani na kuwekwa kizuizini huko mji mwema.

Chuki ya liberator ikaendela, ikaja kutumiwa vizuri mwaka 1985 kipindi cha uchaguzi wa kumrithi Nyerere, wakati Nyerere akitaka Salim kumrithi aliwashawishi Mwinyi na Kawawa kumuachia Salim, Kawawa alikubali na kutekeleza.

Mwanzo Mwinyi alikubali lakini baadae aligoma baada ya kufuata na kambi ya liberator, wengi waliona kuwa kwakuwa Mwinyi walikuwa wameshaishi nae kama Rais huko Zanzibar kwa mwaka mmoja waliona wangeweza kummudu, pia waliona Mwinyi anaingilika haraka Kuliko Salim hivyo wakampiga vita ili Salim asiwe Rais badala yake Mwinyi ndie ashinde ili wawe na uhuru wa mambo yao.

Inatajwa kuwa Salim alikuwa muumini wa serikali moja ya Muungano, imani ambayo alikuwa nayo Nyerere, wengi humtaja Salim kuwa mfuasi wa Nyerere.

Wengi walimuhofia na kutomuelewa Salim vizuri na kuogopa kuwa anaweza kuwa mwanamisimamo mkali, asingilike kwa uraisi.

Wafuasi wa front line kutoka Zanzibar walikuja bara na kuwashawishi wanaccm kadhaa kumuunga mkono Mwinyi ili kuondoa mfumo wa unyerere Tanzania.

Kwa bara Balozi Getrude Mongela na Paul Bomani waliongoza kambi hii ya wahafidhina wakisaidiwa na wanasiasa wengi Wazanzibar kutoka Unguja kwani Salim alitokea Pemba.

Mama Mongela alisemekana kumfuata Mwalimu na kumuuliza kwa nini alikuwa anatakata kumuaibisha Mwinyi ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wake na badala yake kumpigia upatu Salim ambaye kiprotokali yuko hadhi chini ya Mwinyi.

Nyerere alipanga kuwa katika uchaguzi ule Kawawa ajitoe, na kweli alijitoa, akabaki Mwinyi na Salim, Nyerere alitegemea Mwinyi kujitoa pia ili abakie Salim, tofauti ilivyo tegemewe ngome ya Zanzibar wakasambaza fitina kuwa hawatamuunga mkono Salim kwakua ni hizbur (wafuasi wa Shamte waliopinduliwa na ASP).

Wakatangaza kumuunga mkono Mwinyi, mwinyi hakujutoa, mwishowe Mwinyi alifanikiwa kumrithi Mwalimu, akawa Rais wa pili wa Tanzania.

Wale wafuasi wa mapinduzi humuona Salim kama hizbur, yani mwarabu na mfuasi wa serikali iliyopinduliwa ya Shamte.

Mwaka 1995 tena, wakati Uchaguzi unakaribia kufanyika, Rais Mstaafu Julius Nyerere alimtuma Waziri wa fedha wa wakati huo, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa anakwenda Nairobi kwenye kikao ambapo Salim naye alikuwepo kikazi aende kumbembeleza aje kwa mazungumzo nchini.

Salim alijua anachoitiwa na Mwalimu akamwambia Kikwete amwambie Mwalimu kuwa yuko bize sana na shughuli za Umoja wa Afrika (ni kama Salim alihisi alichokuwa anaitiwa au pengine kulishafanyika mazungumzo kabla baina yao), Rais Mstaafu Mkapa kwenye kitabu chake cha mwisho, amewahi kueleza kuwa Mwalimu aliwahi kumuambia kuwa amewahi kumbembeleza kweli mwanasiasa kijana mmoja agombee lakini akaonekana kuringaringa.

Nyerere alitaka Salim awe Rais mwaka 1995 baada ya Mwinyi kumaliza muda wake, Nyerere aliamini kuwa hicho ndio kilikuwa kipindi kizuri kwa Salim kwakua joto la siasa Zanzibar lilikuwa limeshuka, na hakukuwa na mgombe mwenye nguvu kutokea Zanzibar kuweza kumzuia Salim.

Nyerere aliamini kuwa iwapo Salim angeshinda basi muungano wa serikali moja ungefanikiwa, hii ndio ilikuwa ndoto ya Nyerere katika muungano, na mtu pekee ambae angeamini kufanya hivyo ni Salim pekee.

Mwaka 1985, wakati Rais Mwinyi anagombea kumrithi Mwalimu kwenye kiti cha Urais dhidi ya Salim, kuliibuka watu kutoka kambi ya mpinzani wake wakidai yeye alikuwa mpinga mapinduzi kwa kuwa alikuwa hamalizi hotuba zake na kauli, ''mapinduzi daima'' hivyo alionwa kama mpinzani wa mapinduzi ya Zanzibar.

Mwaka 2005, Salim alipokuwa amehitimisha utumishi wake Umoja wa Afrika kama Katibu mkuu wa jumuiya husika, aliamua kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wazee Joseph Warioba, Pius Msekwa, Joseph Butiku walisemekana kumuunga mkono kisirisiri, lakini ndani ya chama alibwagwa na Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete aliyefanikiwa kuibuka na kupata uteuzi wa kuwa mgombea Urais na yeye kushikilia nafasi ya pili kwa wingi wa kura huku akifuatiwa na Prof Mark James Mwandosya.

Kipindi hiki ilikuwa ngumu Salim kushinda kwasababu Kikwete alikuwa amejiandaa vya kutosha, Salim akuwa na maandalizi makubwa kwasababu ilikuwa ndio mda mfupi katoka huko Umoja wa Afrika.

Hata hivyo, kwa mara nyingine tena Salim alichafuliwa kweli kweli kwa kuitwa Hizbu, muarabu na mpanga mauaji ya Mzee Sheikh Abeid Karume mwaka 1972 na wanamtandao waliokuwa wanamuunga mkono Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

Wazanzibar wengi kwenye mkutano mkuu wa chama walihamasishwa kutompigia kura na wanamtandao pamoja na kuwa alikuwa Mzanzibar pekee miongoni mwa wagombea watatu, Mwaka 2000, wakati aliyekuwa Waziri wa Ujenzi Zanzibar, Amani Karume anaenda kuchukua fomu ya kugombea Urais, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alionekana akiambatana naye na mwishowe kumfungulia mlango wa gari ili aingie ndani ya ofisi za chama kuchukua fomu.

Ukaribu kati ya mgombea Urais Jakaya Kikwete na Rais Amani Karume ulisemekana kuwa mwiba kwa mgombea Salim Ahmed Salim ambaye alichafuliwa kweli kweli na kuangukia pua.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa miaka 20 kabla (1985), Salim hakuwahi kulalamikia siasa chafu dhidi yake popote pale waziwazi, Salim husemekana kuwa mwanasiasa mwenye akili tulivu lakini mwenye misimamo mikali na asiyeyumbishwa kirahisi.

Salim sio msemaji sana lakini asemapo hutoa sauti yenye uzito na isiyo na mashaka, China imewahi kumtunuku Salim nishani ya heshima mwaka 2019 iliyopokelewa na mwanaye.

Ikumbukwe, Salim alifanikisha jitihada ya China kupewa kiti cha kudumu baraza la Usalama, Umoja wa Mataifa miaka ya 70-80 akiwa mwakilishi wa kudumu Umoja wa Mataifa.

Miaka ya 80 wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kurt Waldheim anahitimisha muhula wake wa pili huku akiingiwa na tamaa kugombea mhula wa tatu tofauti na ilivyozoeleka kwa watangulizi wake, Salim alishawishiwa na China pamoja na nchi za jumuiya ya Umoja wa Afrika na zisizo na mfungamano (non aligned) kuwania kiti hicho na kigogo huyo.

Salim alifanya hivyo na katika raundi ya kwanza alimshinda Waldheim kwa kura moja (10 kwa 11) hata hivyo kura ziliporudiwa kufuatia Marekani kupiga kura ya veto kumpinga Salim kwa kuwa Salim alionekana kufungamana na China na Urusi ambao walionekana kuwa maadui wa Marekani.

China nayo ikapiga kura ya veto dhidi ya Waldheim, Wote wakawa wanapigiwa kura za veto kwa raundi zilizofuatia. Mwishowe, wote walijitoa kwenye kinyang'anyiro.

Javier Perez de Cuellar mwishowe alipitishwa kuwa Katibu mkuu mpya ya Umoja wa Mataifa kumrithi Kurt Waldheim.

Mwaka 1996 wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Boutrous Ghali ambae alikuwa na veto ya Marekani kwenye ugombeaji wake wa awamu ya pili, ilisemekana Marekani kuwa iko tayari kwa Mwafrika yeyote yule mwingine kushika nafasi hiyo hata kama ni Salim kwa kuwa walishamchoka Mmisri huyo.

Mwaka 1994 palitokea mauaji makubwa ya halaiki nchini Rwanda bila kuwepo na majibu yasiyoridhisha kutoka kwa Boutrous Ghali yanayoonyesha hatua ilizochukua Umoja wa Mataifa kukabiliana na hali ile, Pamoja na mkwamo wa Boutrous Ghali, Salim alikataa kugombea tena nafasi hiyo adhimu Umoja wa Mataifa.

Kofi Annan akachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1997.

Salim aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuwa ya Chama cha Mapinduzi kwenye awamu yake ya pili.

Salim kwasasa ni Mkuu wa Chuo cha Herbert Kairuki Memorial, pia Salim amewahi kuwa Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Foundation na pia Mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya uongozi bora Afrika ya Mo Ibrahim.

Salim anafahamika na kukubalika sana nje ya nchi na ni rafiki wa vigogo Thabo Mbeki, Olesegun Obasanjo na kwa ndani ya nchi husemekana kuwa karibu na Prof Mark Mwandosya na marehemu Magufuli na Mpemba mwenzake, Maalim Seif.

Mwaka 2014, Thabo Mbeki aliwahi kumwelezea Salim, Ndipo nilipojua huyu mzee alikuwa ni mpambanaji, mwenye misimamo (pengine kuliko hata Nyerere), na mpigania uhuru haswaa tofauti na haiba yake ya upole aliyo nayo.

Mbeki aliwahi kueleza kuwa miaka ya 1980, kuwa ANC walifikia hitimisho kwamba waache mapambano ya mtutu, warudi kwenye meza ya mazungumzo Wakamtuma Thabo aje kumwambia Mwalimu.

Kabla hajamwona Mwalimu, Thabo alikutana na Salim, akamweleza azma yao, Salim akanonekana kushtuka na kumuliza kwa mstuko, "You want to negotiate with Boers?".

Ilikuwa ni kauli iliyoonesha kudharau maamuzi yao na kutamani wasauzi waendelee na mapambano dhidi ya makaburu.

Thabo Mbeki alielezea kwa undani kwamba ile hali, pengine iliyomwogopesha, ilimwanadaa vizuri kuukabili upinzani wa Mwalimu juu ya hoja yao ya kuweka silaha chini.

Salim Ahmed Salim ni hazina ya bara la Afrika, ana tuzo kadhaa za heshima kama Order of the Star of Africa aliyopewa na Liberia mwaka 1980, tuzo ya heshima ya Order of the United Republic of Tanzania - ribbon bar aliyopewa na Tanzania mwaka 1985.

Pia ana tuzo ya heshima ya National Order of the Thousand Hills, aliyopewa na Rwanda Mwaka 1993. Pia tuzo ya heshima ya Order of Congolese Devotion aliyopewa na Congo.

Nyingi ni ile aliyopewa na China mwaka 2019.

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526/0765026057 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057(Whatsapp).
Email-mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.
Salim-cover.jpg
Screenshot_20230101-163712.jpg
Screenshot_20230101-164518.jpg
Screenshot_20230101-163732.jpg
Screenshot_20230101-164438.jpg
Screenshot_20230101-163812.jpg
Screenshot_20230101-163515.jpg
Screenshot_20230101-163537.jpg
Screenshot_20230101-163444.jpg
Screenshot_20230101-163432.jpg
Screenshot_20230101-163140.jpg
Screenshot_20230101-163122.jpg
Screenshot_20230101-163049.jpg
sep-09-1979-new-president-of-the-general-assembly-salin-ahmed-salim-E11R1G.jpg
Screenshot_20230101-163031.jpg
Screenshot_20230101-163040.jpg
Screenshot_20230101-162904.jpg
Screenshot_20230101-162918.jpg
IMG-20221231-WA0085.jpg
IMG-20221231-WA0091.jpg
IMG-20221231-WA0090.jpg
IMG-20221231-WA0093.jpg
IMG-20221231-WA0089.jpg
IMG-20221231-WA0087.jpg
IMG-20221231-WA0092.jpg
 
Maktaba Kuu.View attachment 2465775View attachment 2465776View attachment 2465777View attachment 2465778View attachment 2465779View attachment 2465780View attachment 2465781View attachment 2465782View attachment 2465783View attachment 2465784View attachment 2465786View attachment 2465787View attachment 2465788View attachment 2465793View attachment 2465789View attachment 2465790View attachment 2465791View attachment 2465792View attachment 2465794View attachment 2465801View attachment 2465803View attachment 2465802View attachment 2465799View attachment 2465800View attachment 2465804
Nilibahatika kumtembelea Dr. Salim Ahmed Salim nyumbani kwake.
Nilichozungumzanae ilikuwa yeye kuandika kumbukumbu zake.

Kuanzia hapo miaka michache iliyopita ikawa sura yangu kaitambua na kila nilipokutananae nilimuomba kumpiga picha.

Bahati ni kuwa wasaidizi wake tunafahamiana na wakati mwingine wakimsimamisha khasa ili nipate picha yake kwa utulivu:

05J2J6mv1ARGLxWQ5sbgY0qbABUe1ZoNhL-GLB92fSVp5D6UGKjQrrXnfk98tMqX5JroLlIWQBQGMTAqx7nf9mCdgsPySpuEtjnG264oGzryYpJYlAYmT2UIsFVY-gYdfb8VFL5jTq9o9FKVJD-K3ZaqattK4Ughhjv6DLEThS2TcMzuQ0-ne_3mmEGb_WXcLlNiUlsbSQ6yWTcDNL_tG4RjOa186XBxhuXULEiPb2D9HhNi_d3tqnBjOEEnQaufHyYme5jtLOaLV2ctYDdz0bz8Yeuq8DKhqTWWTblKf_bET5WsYLIf_WRtbWmcriLXncSvYHSXBlMangniScQevKT4B0B_eCV-XWmCw9NaOjpEukoPYY2CMxvI1e1v8hfJNVR2clJcUNV_6VZSCJKCUq0QlEbb_gh46JtmxYi3H-JT0n-moBL-LgRIYnTcBvKZ9MAPy8pWBKN379opcRUtD-YZ5msyoQ2_4yLp8e5B11NN8M_2XIwMaISIUBYH0C38klqtPKysu_nSZgoyhkwqqELWtOXI0Vsv_CmQTe1LOKEs9kSDgEs_JJnzVmyy-1ezjKhIL39fJcceTMlVqic7noEszhpucu3IEacWn02H7ZDkLg-F_LZZEId_UESOWzK7sM8h066s-zNw97bnRcucbHvcVv52m8y0v6opZQpKyip--KKuIAdMFIomvisaFuFq7giYtmFu_tz961Tpy33IgWYsUZFSyoCDHL_STaVad8uUTBfRntq7oLxt_f5ZMby4Oqdg29mYlfNHONo_LziMZu4iVFitU0bLc0_2KFFHpm7IXN51CyGMcu8GHkrxQPZ0qSGYPNKELFVzs0WnGAbzhImDECgvvK6ju7ggKtpTEnvRmVXcK0bh_ErIbDSxobxhJq7dCM0R--JWv3rMU1FFSzSErunbVfA7K4xfzuCslaWxn6eQ4-RBJ6dRfU3synggovYzOUefxcHWUdVLW34=w867-h650-no
 
Daaah miaka 19 wa sasa ni mbeba vyuma au panya rodi
Kwa wakati huo ilikua inawezekana kwasababu ya uhaba wa watu wenye Elimu walau.

Kwasasa hata uwe na uwezo wa kumzidi SAS kwa mbali hauwezi kupewa uongozi kwa umri huo kwasababu watu wasomi ni wengi Sana.

Hata SAS arudi umri huo aliokua nao kwa sasa hapati uongozi aliopata miaka hiyo.
 
Nilibahatika kumtembelea Dr. Salim Ahmed Salim nyumbani kwake.
Nilichozungumzanae ilikuwa yeye kuandika kumbukumbu zake.

Kuanzia hapo miaka michache iliyopita ikawa sura yangu kaitambua na kila nilipokutananae nilimuomba kumpiga picha.

Bahati ni kuwa wasaidizi wake tunafahamiana na wakati mwingine wakimsimamisha khasa ili nipate picha yake kwa utulivu:

05J2J6mv1ARGLxWQ5sbgY0qbABUe1ZoNhL-GLB92fSVp5D6UGKjQrrXnfk98tMqX5JroLlIWQBQGMTAqx7nf9mCdgsPySpuEtjnG264oGzryYpJYlAYmT2UIsFVY-gYdfb8VFL5jTq9o9FKVJD-K3ZaqattK4Ughhjv6DLEThS2TcMzuQ0-ne_3mmEGb_WXcLlNiUlsbSQ6yWTcDNL_tG4RjOa186XBxhuXULEiPb2D9HhNi_d3tqnBjOEEnQaufHyYme5jtLOaLV2ctYDdz0bz8Yeuq8DKhqTWWTblKf_bET5WsYLIf_WRtbWmcriLXncSvYHSXBlMangniScQevKT4B0B_eCV-XWmCw9NaOjpEukoPYY2CMxvI1e1v8hfJNVR2clJcUNV_6VZSCJKCUq0QlEbb_gh46JtmxYi3H-JT0n-moBL-LgRIYnTcBvKZ9MAPy8pWBKN379opcRUtD-YZ5msyoQ2_4yLp8e5B11NN8M_2XIwMaISIUBYH0C38klqtPKysu_nSZgoyhkwqqELWtOXI0Vsv_CmQTe1LOKEs9kSDgEs_JJnzVmyy-1ezjKhIL39fJcceTMlVqic7noEszhpucu3IEacWn02H7ZDkLg-F_LZZEId_UESOWzK7sM8h066s-zNw97bnRcucbHvcVv52m8y0v6opZQpKyip--KKuIAdMFIomvisaFuFq7giYtmFu_tz961Tpy33IgWYsUZFSyoCDHL_STaVad8uUTBfRntq7oLxt_f5ZMby4Oqdg29mYlfNHONo_LziMZu4iVFitU0bLc0_2KFFHpm7IXN51CyGMcu8GHkrxQPZ0qSGYPNKELFVzs0WnGAbzhImDECgvvK6ju7ggKtpTEnvRmVXcK0bh_ErIbDSxobxhJq7dCM0R--JWv3rMU1FFSzSErunbVfA7K4xfzuCslaWxn6eQ4-RBJ6dRfU3synggovYzOUefxcHWUdVLW34=w867-h650-no
Yupo wapi kwa sasa na hali yake ya afya ikoje?
 
Mmoja wa Viongozi wangu bora wa Nchi hii baada ya Mwalimu.

Nilitamani sana Huyu Bwana angepata nafasi ya kuwa President of United republic of Tanzania wakati ule.
 
SALIM AHMED SALIM; MWANASIASA MWENYE AKILI, MTULIVU, WAZIRI MKUU MSTAAFU, MWANADIPLOMASIA MKONGWE NA CHAGUO LA NYERERE KAMA MRITHI WAKE ILA FITNA ZA WAZANZIBARI NA UNYERERE UKAMPONZA, IKAMFANYA ACHUKIWE NA KUGEUKA LULU ISIYO NA THAMANI.

Na. Comred Mbwana Allyamtu -CMCA
Sunday- 1/1/2023 (Uzi wa kwanza 2023)
Marangu Kilimanjaro Tanzania.

Salim Ahmed Salim ni mwanadiplomasia mkongwe, mahiri na mwenye ushawishi mkubwa kwenye korido za diplomacy duniani.

Ni lulu ya siasa za mashuri ya kigeni, namanisha kuwa Salim ni mtu muhimu na mahiri kwenye maswala ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa, anaheshimika sana China, Umoja wa Afrika na Marekani.

Ndio mtu pekee Kutoka Afrika ambaye alitikisa dunia kwenye mchuano wa kumpata katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Mwaka 1981, Marekani na China zilivutana mpaka Dunia ikasimama.

Salim ni mwanasiasa mwenye heshima kubwa Tanzania, ni lulu ambayo siasa za fitina na uzanzibari zimemfanya kupotea kisiasa.

Dr Salim Ahmed Salim, alikuwa katibu mkuu wa 7 wa Umoja wa Afrika, akawa Waziri mkuu wa 4 wa Tanzania na akawa Waziri wa 8 wa Mambo ya nje wa Tanzania.

Dr Salim Ahmed Salim alizaliwa tarehe 23 January mwaka 1942, kwa sasa ana miaka 80, alizaliwa huko Zanzibar kwa mama mwenye asili ya kiarabu na kiafrika pamoja na baba mwenye asili ya kiarabu kutoka Oman aliyeitwa Sheikh Ahmed Salim Riyami.

Salim ana Masters ya masuala ya ushirikiano wa kimataifa kutoka chuo kikuu cha Columbia University.

Salim alisoma katika shule ya Lumumba huko Zanzibar na baadaye akaendelea na masomo yake ya shahada ya kwanza katika Chuo cha St. Stephen cha Chuo Kikuu cha Delhi huko India, na akapata shahada yake ya uzamili katika Masuala ya Kimataifa kutoka Shule ya Masuala ya Kimataifa na Umma katika Chuo Kikuu cha Columbia huko New York Marekani.

Salim alikua mwanaharakati wa wanafunzi miaka ya 1950 na kuwa mwanzilishi na Makamu wa kwanza wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Zanzibar wote.

Salim alikuwa na mke mmoja aitwae Amne aliyefariki tarehe 20 October 2020, Salim amebahatika kupata watoto 3 ambao ni Maryam, Ali na
Ahmed, ingawaje husemekana ana mtoto wa nje ambaye ni mwanamama waziri kwa sasa kwenye serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan, hata hivyo taarifa hizi hazijawahi kuthibitishwa popote.

Salim amekuwa Balozi nchini Egypt mwaka 1961 akiwa na miaka 19 tu na hivyo kuweka historia ya kuwa Mtanzania mwenye umri mdogo kuliko wote kuwahi kuwa balozi.

Salim amewahi kuwa pia balozi nchi za China, Cuba, Trinidad, Guyana n.k, alikuwa kijana mchapakazi na mtiifu mno kwa Nyerere.

Salim amewahi kuwa mwakilishi wa kudumu Umoja wa mataifa kuanzia mwaka 1970 Mpaka 1980 ambapo mojawapo ya mafanikio yake ilikuwa kuihakikishia China inapewa kiti cha kudumu kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, Salim ni rafiki wa China.

Salim amewahi kuwa Waziri wa mambo ya Nje mwaka 1981 Mpaka 1984, alipokea nafasi hiyo kutoka kwa Mkapa, na alipo badilishwa alimuachia Mkapa tena.

Salim amewahi kuwa Waziri Mkuu wa 4 wa Tanzania mwaka 1984 mpaka 1985 na kuwa Waziri Mkuu pekee kutoka Zanzibar lakini pia aliyehudumu kwa muda mfupi kushinda wote, Uteuzi wake ulifuata baada kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu kipenzi cha Watanzania wengi, Edward Sokoine kufuatia ajali ya gari, Morogoro.

Salim aliuachia Uwaziri Mkuu mara moja baada ya aliyekuwa amemteua, Rais Mwalimu Nyerere kustaafu lakini pia kufuatia uchaguzi wa Ndugu Ali Hassan Mwinyi, Mzanzibar mwenzake lakini kutokea Unguja kushika rasmi kiti cha Urais.

Kufuatia uchaguzi wa Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais, Salim aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga taifa, Salim anadai katika nyadhifa alizowahi kuzifurahia kuzishikilia kushinda zote ilikuwa ni ya uwaziri wa ulinzi na Jeshi la kujenga taifa kwani alikuwa na jukumu la kuwahudumia wanajeshi na kuhakikisha ulinzi wa nchi na mipaka yake ambayo anadai ilikuwa heshima kubwa sana kwake.

Mwaka 1989 mpaka 2001, Salim alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja Afrika na kuwa Katibu Mkuu aliyehudumu muda mrefu zaidi kushinda wote, Katika kipindi hiki, Salim alisimamia mikakati ya pamoja ya nchi za Afrika kufanikisha ukombozi kwenye nchi za Afrika Kusini na Namibia lakini pia kutatua migogoro mbalimbali ya kisiasa kwenye baadhi ya nchi.

Wakati akiwa mwanafunzi shule ya Sekondari Lumumba, Salim alishaanza harakati za kisiasa na alijiunga na vyama tofauti vya kisiasa vilivyokuwa na lengo la kuwapatia uhuru Wanazanzibar.

Mwaka 1985, wakati Mwalimu Nyerere aliyekuwa Rais kipindi hicho anajindaa kung'atuka, paliibuka mapendekezo ya wanasiasa watatu wa kumrithi ambao walikuwa ni Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Rashid Kawawa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu pamoja na Salim mwenyewe ambaye wakati huo alikuwa Waziri Mkuu.

Mwalimu Nyerere alisemekana kumtaka Salim amrithi huku baadhi ya wahafidhina kutokea Zanzibar na bara wakimpiga vita Salim vikali.

Sababu ya Salim kuanguka ilitokana na kugawanyika kwa wanasiasa huko Zanzibar, Kati ya liberator (walio tetea mapinduzi) na front line (waliotoka hizbur, vijana ambao hawakutoka ASP).

Mgawanyiko huu ulitokana na Siasa za Jumbe, Mwanzoni Jumbe aliutaka uraisi wa Tanzania, alipoona mambo yamekuwa sivyo alivyotegemea akarudisha siasa za fitina ndani ya Zanzibar, wakati anarudi alikuta CCM imeshagawinyika huko Zanzibar, vijana kutoka hizbur kama Maalim Self, Salim Ahmed Salim na kina Izack Sepetu walikuwa Tayari wameshapata nguvu ndani ya Chama.

Ikumbukwe vijana hawa walitoka nationalist (hizbur) yani wale wasio unga mkono mapinduzi, walijiunga na ASP na kuanza kupata nguvu.

Vijana hawa ndio walitumiwa na Nyerere kumuondoa Jumbe Zanzibar, katika Kipindi kile cha kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar, Hivyo wakati Salim anataka uraisi wengi walimtuhumu kuwa ni hizbur, yani wale Waarabu waliopinduliwa enzi za Shamte.

Ilisemekana kuwa Salim alitajwa kuwa mhafidhina wa Siasa za unyerere, pia alituhumiwa kuusika njama ya mauaji ya Karume, njama za kumuondoa Jumbe na kuidhibiti CCM ya wanamapinduzi, yani wale front line kuhodhi visiwa vya Zanzibar dhidi ya wanamapinduzi (liberator).

Hivyo walidai kuwa Salim ana unyerere, Hivyo kwakua walisalitiwa na Nyerere kupitia Jumbe hawakuwa Tayari kumuunga mkono, waliona kuwa Nyerere alitaka kufuta historia ya mapinduzi huko Zanzibar.

Jumbe aliporejea Zanzibar ili kujiongezea nguvu kisiasa baada ya kuona kushindwa huko bara alitaka kuwashughulikia wakina Salim kama alivyokuwa akifanya Karume, lakini asingeweza kwasababu Tayari kambi ya front line ilikuwa imeshahodhi sehemu kubwa ya siasa za Zanzibar.

Zanzibar ikapasuka vipande viwili, yani liberator na front line, front line ilitumiwa vyema na Nyerere kudhoofisha mipango ya Abood Jumbe, Mwaka 1983 Jumbe akangolewa madarakani na kuwekwa kizuizini huko mji mwema.

Chuki ya liberator ikaendela, ikaja kutumiwa vizuri mwaka 1985 kipindi cha uchaguzi wa kumrithi Nyerere, wakati Nyerere akitaka Salim kumrithi aliwashawishi Mwinyi na Kawawa kumuachia Salim, Kawawa alikubali na kutekeleza.

Mwanzo Mwinyi alikubali lakini baadae aligoma baada ya kufuata na kambi ya liberator, wengi waliona kuwa kwakuwa Mwinyi walikuwa wameshaishi nae kama Rais huko Zanzibar kwa mwaka mmoja waliona wangeweza kummudu, pia waliona Mwinyi anaingilika haraka Kuliko Salim hivyo wakampiga vita ili Salim asiwe Rais badala yake Mwinyi ndie ashinde ili wawe na uhuru wa mambo yao.

Inatajwa kuwa Salim alikuwa muumini wa serikali moja ya Muungano, imani ambayo alikuwa nayo Nyerere, wengi humtaja Salim kuwa mfuasi wa Nyerere.

Wengi walimuhofia na kutomuelewa Salim vizuri na kuogopa kuwa anaweza kuwa mwanamisimamo mkali, asingilike kwa uraisi.

Wafuasi wa front line kutoka Zanzibar walikuja bara na kuwashawishi wanaccm kadhaa kumuunga mkono Mwinyi ili kuondoa mfumo wa unyerere Tanzania.

Kwa bara Balozi Getrude Mongela na Paul Bomani waliongoza kambi hii ya wahafidhina wakisaidiwa na wanasiasa wengi Wazanzibar kutoka Unguja kwani Salim alitokea Pemba.

Mama Mongela alisemekana kumfuata Mwalimu na kumuuliza kwa nini alikuwa anatakata kumuaibisha Mwinyi ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wake na badala yake kumpigia upatu Salim ambaye kiprotokali yuko hadhi chini ya Mwinyi.

Nyerere alipanga kuwa katika uchaguzi ule Kawawa ajitoe, na kweli alijitoa, akabaki Mwinyi na Salim, Nyerere alitegemea Mwinyi kujitoa pia ili abakie Salim, tofauti ilivyo tegemewe ngome ya Zanzibar wakasambaza fitina kuwa hawatamuunga mkono Salim kwakua ni hizbur (wafuasi wa Shamte waliopinduliwa na ASP).

Wakatangaza kumuunga mkono Mwinyi, mwinyi hakujutoa, mwishowe Mwinyi alifanikiwa kumrithi Mwalimu, akawa Rais wa pili wa Tanzania.

Wale wafuasi wa mapinduzi humuona Salim kama hizbur, yani mwarabu na mfuasi wa serikali iliyopinduliwa ya Shamte.

Mwaka 1995 tena, wakati Uchaguzi unakaribia kufanyika, Rais Mstaafu Julius Nyerere alimtuma Waziri wa fedha wa wakati huo, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa anakwenda Nairobi kwenye kikao ambapo Salim naye alikuwepo kikazi aende kumbembeleza aje kwa mazungumzo nchini.

Salim alijua anachoitiwa na Mwalimu akamwambia Kikwete amwambie Mwalimu kuwa yuko bize sana na shughuli za Umoja wa Afrika (ni kama Salim alihisi alichokuwa anaitiwa au pengine kulishafanyika mazungumzo kabla baina yao), Rais Mstaafu Mkapa kwenye kitabu chake cha mwisho, amewahi kueleza kuwa Mwalimu aliwahi kumuambia kuwa amewahi kumbembeleza kweli mwanasiasa kijana mmoja agombee lakini akaonekana kuringaringa.

Nyerere alitaka Salim awe Rais mwaka 1995 baada ya Mwinyi kumaliza muda wake, Nyerere aliamini kuwa hicho ndio kilikuwa kipindi kizuri kwa Salim kwakua joto la siasa Zanzibar lilikuwa limeshuka, na hakukuwa na mgombe mwenye nguvu kutokea Zanzibar kuweza kumzuia Salim.

Nyerere aliamini kuwa iwapo Salim angeshinda basi muungano wa serikali moja ungefanikiwa, hii ndio ilikuwa ndoto ya Nyerere katika muungano, na mtu pekee ambae angeamini kufanya hivyo ni Salim pekee.

Mwaka 1985, wakati Rais Mwinyi anagombea kumrithi Mwalimu kwenye kiti cha Urais dhidi ya Salim, kuliibuka watu kutoka kambi ya mpinzani wake wakidai yeye alikuwa mpinga mapinduzi kwa kuwa alikuwa hamalizi hotuba zake na kauli, ''mapinduzi daima'' hivyo alionwa kama mpinzani wa mapinduzi ya Zanzibar.

Mwaka 2005, Salim alipokuwa amehitimisha utumishi wake Umoja wa Afrika kama Katibu mkuu wa jumuiya husika, aliamua kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wazee Joseph Warioba, Pius Msekwa, Joseph Butiku walisemekana kumuunga mkono kisirisiri, lakini ndani ya chama alibwagwa na Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete aliyefanikiwa kuibuka na kupata uteuzi wa kuwa mgombea Urais na yeye kushikilia nafasi ya pili kwa wingi wa kura huku akifuatiwa na Prof Mark James Mwandosya.

Kipindi hiki ilikuwa ngumu Salim kushinda kwasababu Kikwete alikuwa amejiandaa vya kutosha, Salim akuwa na maandalizi makubwa kwasababu ilikuwa ndio mda mfupi katoka huko Umoja wa Afrika.

Hata hivyo, kwa mara nyingine tena Salim alichafuliwa kweli kweli kwa kuitwa Hizbu, muarabu na mpanga mauaji ya Mzee Sheikh Abeid Karume mwaka 1972 na wanamtandao waliokuwa wanamuunga mkono Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.

Wazanzibar wengi kwenye mkutano mkuu wa chama walihamasishwa kutompigia kura na wanamtandao pamoja na kuwa alikuwa Mzanzibar pekee miongoni mwa wagombea watatu, Mwaka 2000, wakati aliyekuwa Waziri wa Ujenzi Zanzibar, Amani Karume anaenda kuchukua fomu ya kugombea Urais, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alionekana akiambatana naye na mwishowe kumfungulia mlango wa gari ili aingie ndani ya ofisi za chama kuchukua fomu.

Ukaribu kati ya mgombea Urais Jakaya Kikwete na Rais Amani Karume ulisemekana kuwa mwiba kwa mgombea Salim Ahmed Salim ambaye alichafuliwa kweli kweli na kuangukia pua.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa miaka 20 kabla (1985), Salim hakuwahi kulalamikia siasa chafu dhidi yake popote pale waziwazi, Salim husemekana kuwa mwanasiasa mwenye akili tulivu lakini mwenye misimamo mikali na asiyeyumbishwa kirahisi.

Salim sio msemaji sana lakini asemapo hutoa sauti yenye uzito na isiyo na mashaka, China imewahi kumtunuku Salim nishani ya heshima mwaka 2019 iliyopokelewa na mwanaye.

Ikumbukwe, Salim alifanikisha jitihada ya China kupewa kiti cha kudumu baraza la Usalama, Umoja wa Mataifa miaka ya 70-80 akiwa mwakilishi wa kudumu Umoja wa Mataifa.

Miaka ya 80 wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kurt Waldheim anahitimisha muhula wake wa pili huku akiingiwa na tamaa kugombea mhula wa tatu tofauti na ilivyozoeleka kwa watangulizi wake, Salim alishawishiwa na China pamoja na nchi za jumuiya ya Umoja wa Afrika na zisizo na mfungamano (non aligned) kuwania kiti hicho na kigogo huyo.

Salim alifanya hivyo na katika raundi ya kwanza alimshinda Waldheim kwa kura moja (10 kwa 11) hata hivyo kura ziliporudiwa kufuatia Marekani kupiga kura ya veto kumpinga Salim kwa kuwa Salim alionekana kufungamana na China na Urusi ambao walionekana kuwa maadui wa Marekani.

China nayo ikapiga kura ya veto dhidi ya Waldheim, Wote wakawa wanapigiwa kura za veto kwa raundi zilizofuatia. Mwishowe, wote walijitoa kwenye kinyang'anyiro.

Javier Perez de Cuellar mwishowe alipitishwa kuwa Katibu mkuu mpya ya Umoja wa Mataifa kumrithi Kurt Waldheim.

Mwaka 1996 wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Boutrous Ghali ambae alikuwa na veto ya Marekani kwenye ugombeaji wake wa awamu ya pili, ilisemekana Marekani kuwa iko tayari kwa Mwafrika yeyote yule mwingine kushika nafasi hiyo hata kama ni Salim kwa kuwa walishamchoka Mmisri huyo.

Mwaka 1994 palitokea mauaji makubwa ya halaiki nchini Rwanda bila kuwepo na majibu yasiyoridhisha kutoka kwa Boutrous Ghali yanayoonyesha hatua ilizochukua Umoja wa Mataifa kukabiliana na hali ile, Pamoja na mkwamo wa Boutrous Ghali, Salim alikataa kugombea tena nafasi hiyo adhimu Umoja wa Mataifa.

Kofi Annan akachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1997.

Salim aliteuliwa na Rais Kikwete kuwa mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuwa ya Chama cha Mapinduzi kwenye awamu yake ya pili.

Salim kwasasa ni Mkuu wa Chuo cha Herbert Kairuki Memorial, pia Salim amewahi kuwa Mwenyekiti wa Mwalimu Nyerere Foundation na pia Mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya uongozi bora Afrika ya Mo Ibrahim.

Salim anafahamika na kukubalika sana nje ya nchi na ni rafiki wa vigogo Thabo Mbeki, Olesegun Obasanjo na kwa ndani ya nchi husemekana kuwa karibu na Prof Mark Mwandosya na marehemu Magufuli na Mpemba mwenzake, Maalim Seif.

Mwaka 2014, Thabo Mbeki aliwahi kumwelezea Salim, Ndipo nilipojua huyu mzee alikuwa ni mpambanaji, mwenye misimamo (pengine kuliko hata Nyerere), na mpigania uhuru haswaa tofauti na haiba yake ya upole aliyo nayo.

Mbeki aliwahi kueleza kuwa miaka ya 1980, kuwa ANC walifikia hitimisho kwamba waache mapambano ya mtutu, warudi kwenye meza ya mazungumzo Wakamtuma Thabo aje kumwambia Mwalimu.

Kabla hajamwona Mwalimu, Thabo alikutana na Salim, akamweleza azma yao, Salim akanonekana kushtuka na kumuliza kwa mstuko, "You want to negotiate with Boers?".

Ilikuwa ni kauli iliyoonesha kudharau maamuzi yao na kutamani wasauzi waendelee na mapambano dhidi ya makaburu.

Thabo Mbeki alielezea kwa undani kwamba ile hali, pengine iliyomwogopesha, ilimwanadaa vizuri kuukabili upinzani wa Mwalimu juu ya hoja yao ya kuweka silaha chini.

Salim Ahmed Salim ni hazina ya bara la Afrika, ana tuzo kadhaa za heshima kama Order of the Star of Africa aliyopewa na Liberia mwaka 1980, tuzo ya heshima ya Order of the United Republic of Tanzania - ribbon bar aliyopewa na Tanzania mwaka 1985.

Pia ana tuzo ya heshima ya National Order of the Thousand Hills, aliyopewa na Rwanda Mwaka 1993. Pia tuzo ya heshima ya Order of Congolese Devotion aliyopewa na Congo.

Nyingi ni ile aliyopewa na China mwaka 2019.

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526/0765026057 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057(Whatsapp).
Email-mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 2465775View attachment 2465776View attachment 2465777View attachment 2465778View attachment 2465779View attachment 2465780View attachment 2465781View attachment 2465782View attachment 2465783View attachment 2465784View attachment 2465786View attachment 2465787View attachment 2465788View attachment 2465793View attachment 2465789View attachment 2465790View attachment 2465791View attachment 2465792View attachment 2465794View attachment 2465801View attachment 2465803View attachment 2465802View attachment 2465799View attachment 2465800View attachment 2465804
ASANTE SANA KWA HISTORIA
MH.SALIM AHMED SALIM ATABAKI KUWA KIONGOZI BORA KUTOKEA TANZANIA ZAIDI YA HAO WALIOMPIGA FITINA na MAJUNGU MUNGU AZIDI KUMPA MAISHA MAREFU Mh.SALIM AHMED SALIM
 
Wapemba na wazanzibar ni watu wa chuki, umbea umbea na fitna sana! Hata kwenye maisha ya kawaida tu... wachunguzeni 😊

Mleta mada inaonekana una mapenzi sana na Mzee Salim Ahmed Salim... binafsi nilitamani kuona ameshika kiti cha Urais wa Tanzania siku moja, ni mwanasiasa makini sana! Aliyependwa na wengi nafkiri kurudi tena kugombea 2005 ilikuwa too late kwake maana mtetezi wake alikuwa ameshatangulia mbele ya haki (Mzee Nyerere).... ingawa bandiko au chapisho hili umeanza nalo mapema kabisa ya mwaka, kwangu ni moja ya bandiko/chapisho bora kabisa kwa mwaka 2023. Leta mengine mkuu

#KeepItUp 👊🏾💪🏾👍🏾
 
Back
Top Bottom