Wana-JF: Leo pia (Jumamosi tarehe 28 August) katika kipindi chake cha mapitio ya magazeti saa moja kasoro dak kumi, msomaji Isaack Gamba wa kituo hicho cha ITV alisoma magazeti yafuatayo tu: Nipashe, Uhuru, Habari Leo na Guardian. haya yote yalikuwa na vichwa vya habari chanya kwa kampeni za CCM.
Magazeti mengine, baadhi yao yametokea kujizolea usomaji mkubwa hivi karibuni kama vile Mwananchi, T. Daima, Majira, Jambo Leo, The Citizen hayakuwapo kabisa. Na kwa ITV sasa hii ndiyo imekuwa trend katika kipindi hiki cha uchaguzi inajitambulisha moja kwa moja inasimamia upande wa CCM. TCRA -- haya siyo matumizi mabaya ya matumizi ya TV uliyoipa liseni kwa ajili ya kuhudumia wananchi wote?
WanaJF kuna thread zinaendelea zikionesha jinsi wafanyakzi wa ITV na TBC wanavyoujumu Habari, lakini kwa mtazamo wangu hawa tutakuwa tunawaonea bure wana wanapokea maelekezo kutoka kwa maboss wao
R Mengi na TIDO kama majasusi ndo wanawalazimisha vyombo vyao viwe na mlengo wa kiCCM
nkubaliana na wewe kwa asilimia zote mkuu.TBC hawana haki kufanya hivyo ni chombo cha umma ITV wapo huru kama lilivyo Tanzania Daima na Mwanahilisi !
Ni kweli ITV ni chombo huru, ila tatizo liko kwa Mmiliki wake maana siku zote anataka kutuaminisha kuwa ni mtetezi wa wanyonge,mpiga vita rushwa na ufisadi hasa ufisadi papa, na muumini mzuri wa haki za binadamu pia mcha Mungu. Sasa iweje aviamrishe (kama ni hivyo) vyombo vyake vya habari viwatete na kuwanadi kwa nguvu zote wale waendao kinyume na hayo anayotuaminisha kuwa ndiyo anayofuata? Na wale waletao njia mbadala za kumkomboa Mtanzania kama asemavyo yeye hawapi nafasi ya kutosha? Imani yangu kwake inaanza kutoweka. Na ninadhani siko peke yangu.TBC hawana haki kufanya hivyo ni chombo cha umma ITV wapo huru kama lilivyo Tanzania Daima na Mwanahilisi !
Mkuu naona huwa huangalii Chanel 10 mara kwa mara.Leo asubuhi nimeshtushwa na kituo cha ITV kinachimilikiwa na IPP media pale msomaji wa mapitio ya magazeti aliposoma magazeti kama manne tu -- Nipashe, Uhuru, Habari Leo na Guardian, mengineyo kama vilw Mwananchi, Majira, Tanzania Daima na Mtanmzania hayakusomwa kabisa.
Kwa upande wake, kituo cha Channel 10 katika kipindi kama hicho cha saa moja na robo, msomaji Hamis Mkotya alisoma magazeti yote na nikagundua kwamba yale ambayo ITV iliyaacha kusoma kama vile Mwananchi, Tanzania Daima na jambo Leo yalikuwa na habari kubwa kubwa za uzinduzi wa kampeni za Chadema Leo na pia kuhusu pingamizi la Chama hichi dhidi ya mgombea urais wa CCM, JK.
Yaani ghafla ITV imekuwa mpiga debe mkubwa wa kampeni za CCM? Si vyema wajitangaze hivyo tujue? Mimi nilifikiri ITV ni kituo huru cha ITV kumbe ni cha chama tawala? Aibu kubwa hii!!
Nawapa Hongera sana Channel 10, endeleeni na msimamo wenu mliojitambulisha kwamba mko huru.