Chicho_
Member
- May 15, 2024
- 7
- 4
Utupaji hovyo wa taka kando ya Mto Matarawe umekuwa tatizo kubwa linalozidi kushamiri kila siku. Wananchi wanaoishi karibu na mto huo wamegeuza kingo za mto kuwa sehemu ya kutupia taka ngumu, taka za nyumbani, plastiki, mabaki ya chakula na hata vinyesi.
Tabia hii si tu inaharibu mandhari ya mto, bali pia inaleta athari kubwa kwa afya ya binadamu na uhai wa mazingira.
Mto Matarawe umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Songea na maeneo ya jirani kwa miaka mingi, hasa wakati wa uhaba wa maji.
Mto huu umetegemewa kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kuoga, kufua, kunyweshea mifugo, kilimo, na hata matumizi ya nyumbani kwa baadhi ya familia. Lakini kutokana na utupaji wa taka holela unaoendelea bila kudhibitiwa, mto huu upo katika hatari ya kupoteza thamani yake na kugeuka chanzo cha majanga ya kiafya.
Taka zinazotupwa huingia moja kwa moja ndani ya mto au kukusanyika kando, zikisukumwa ndani kwa mvua au upepo. Uchafu huu huleta mazalia ya mbu, husababisha harufu mbaya, na kubadilisha rangi na hali ya maji.
Maji ya mto yanapochafuka kwa taka hizi, huweza kuzalisha vimelea vya magonjwa kama kipindupindu, typhoid, kuhara, amoeba na hata magonjwa ya ngozi na macho. Zaidi ya hayo, mbu wanaozaliana kwenye maji yaliyotuama pembeni ya mto huzidisha maambukizi ya malaria.
Endapo hali hii haitadhibitiwa, mto Matarawe unaweza kukauka kwa sababu ya uchafu mkubwa unaoziba njia ya maji na kuathiri uhai wa viumbe hai waliomo ndani yake. Aidha, familia nyingi zinazotegemea maji ya mto huu zitakosa huduma hiyo muhimu, na hali ya maisha itazidi kuwa ngumu zaidi.
Ni jukumu la kila mmoja kutambua kuwa uchafuzi wa mazingira ni uchafuzi wa maisha yetu wenyewe. Wananchi wanapaswa kuacha kabisa tabia ya kutupa taka hovyo na badala yake kutumia mifumo rasmi ya ukusanyaji taka inayowekwa na halmashauri.
Elimu ya mazingira inapaswa kutolewa kwa jamii nzima, kuanzia mashuleni hadi katika nyumba za ibada ili kuhimiza utunzaji wa mazingira kwa vitendo.
Viongozi wa mitaa, wenyeviti wa serikali za mitaa, watendaji na wakuu wa idara za usafi wa mazingira wanapaswa kusimama imara na kuchukua hatua madhubuti. Hii ni pamoja na kuweka alama za onyo, kupanga siku maalum za usafi wa jamii, kutoa elimu ya madhara ya uchafuzi wa vyanzo vya maji, na kuwatoza faini kali wale wote wanaobainika kutupa taka kando ya mto.
Ninaiomba kwa dhati Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Mkoa wa Ruvuma, pamoja na Manispaa ya Songea, kushughulikia kwa haraka hali ya mto Matarawe kabla athari hazijafika pabaya. Hatua zikiwemo kuanzisha kampeni za kusafisha mto, kuweka vifaa vya kutupia taka karibu na makazi ya watu, na kushirikiana na jamii katika kutunza mazingira ni muhimu na za haraka kuchukuliwa na ikibidi kutoza faini kwa wale watakaobainika kutupa takatka ndani na pembezoni mwa mto huo wenye manufaa makubwa kwa watu na wanyama.
Mazingira ni uhai. Hatuwezi kuendelea kukaa kimya huku tukishuhudia uharibifu mkubwa ukifanyika mbele ya macho yetu. Tunapolinda mto Matarawe, tunalinda afya zetu, watoto wetu, na kizazi kijacho.
Mazingira ni zawadi – tuyatunze.
Maji ni uhai – tusiyachafue.