Leo nilifanya matembezi nikitokea Kigamboni kuelekea Tabata Segerea kwa kutumia usafiri wa umma, daladala. Pamoja na malengo ya safari yangu, nilitamani kuona ni jinsi gani jiji limepiga hatua katika kujitofautisha kwa kuwa safi kama miji mingine kama Moshi kule KLM na Mwanza.
Sikushangaa kuona biashara kama kawaida na uchafu wa kutosha pamoja na harufu mchanganyiko toka mwanzo wa safari mpaka mwisho.
Sema na Mnazi mmoja, Kariakoo, Amana, Malapa, na kiboko yao Buguruni sokoni, kisha dampo na kuendelea.
Bila shaka uchafu unapendwa na wanajiji wengi na kwa maana hiyo wamechagua kuendelea kuishi nao bila kujali madhara ya magonjwa ya mlipuko yanayoibuka kila mara.
Buguruni sokoni, bado bidhaa za mashambani zinawekwa sakafuni jirani kabisa na urojorojo mzito wa uchafu, na wananchi hawaulizi, ila wanpata huduma tu, ukijali wewe shauri yako. Lakini wakianza kuugua na pengine kupoteza maisha, basi hutafuta serikali ipo wapi ili iwasaidie.
Hii si tabia ya kibinadamu katika enzi hizi za maendeleo, kila mmoja ajione analo la kuchanigia ili kufany jiji liwe safi.
Tutimize majukumu yetu.