Kang, yameshakuwa hayo ya nina matatizo ya ubongo? Ukijiheshimu tunaweza kujadiliana tukabadilishana uelewa, vinginevyo tutachafua hali ya hewa hapa sasa hivi na patapoteza muelekeo, huwa ninakuchukulia kama muungwana fulani, sasa ukiona hoja zako zinapingwa usihamaki na kupoteza hulka hiyo, wewe si mkufunzi wa teknolojia ya habari wa jamvi ambae akipingwa kidogo ana panic.
Kupoteza passphrase haimanishi mtu ana ubongo mbovu, na unapokariri password risk ya kupoteza huwa ipo. Wewe mwenye ubongo bora unaokumbuka kwa kichwa encryption passphrases zote hebu nikuulize, umesema ukipoteza password ya Ubuntu mafaili yatakuwa bado kwenye computer. Mada yetu hapa ni "ubuntu has now increased its online storage..." Tunaongelea Ubuntu online storage, sio kwenye computer, sasa huo uelewa wako mkubwa sana mbona hapo umeonyesha very faint comprehension of the subject matter?
Ninasema ukipoteza access password au encryption passphrase ya mafaili yaliyoko kwenye servers za Ubuntu (third party, elewa) data zako zinaweza kuwa ndio imetoka. Haziko kwenye computer yako!
Hakuna ku instal kitu unapotumia Dropbox? Huo ni uongo period, lazima u download Dropbox hapa, halafu u install software, soma hapa. Kwa hiyo ukitaka kumtumia mtu file lazima kwanza umuulize anaijua Ubuntu One, sijui ka download, ka install, halafu nenda wwww, nani ana muda wa kufundishana wakati official modality of communication ya "mafaili madogo" ni e-mail ? Besides, how many end users have heard of the word Ubuntu, let alone Ubuntu-One?
Si watumiaji wote 1GHz of microprocessor power inawatosha, laptop yangu ya 2005 ndio ilikuwa ina gigahertz moja ya processor. Kazi zangu haziwezi kufanywa kwenye simu, na kama zikifanywa bandwidth na computing ninayohitaji haitoshelezwi.
"Backup ambayo haifanywi automatic hiyo sio backup..." ludicrous, I'm sorry, but that's plain baloney. Haya ndio matatizo ya kukariri maneno maneno bila kujua concept, kwani backup maana yake nini? Backup ni nakala ya data, simple as that! Sasa ukiniambia mimi nina copy, kumbe backup maana yake nini? Jamani mbona tunakariri vitu bila kuelewa undani? Mimi ninafanya incremental backup ya data zangu zote routinely, natumia EMC Retrospect Professional, sio lazima back up iwe automatic. Nina nearly a terabyte of data ambayo nina nakala yake - kwa lugha nyingine, backup - kwenye HDD nyingine, hard drive moja ikibuma sipotezi data!
"cloud storage ni kuhusu convenience na efficiency sio kuhusu raw storage or processing power." Kwa nini u limit the realm of analysis kwenye convience tu? Tunalinganisha hizi approaches mbili, tunajadili pros and cons zake halafu unasema hayo mengine usiyaongelee, we vipi mazee, ndio drawbacks zake hizo nakupa. Nimeonyesha sababu mbali mbali ni kwa nini sihitaji vi gigabyte space viwili vya Ubuntu One.
Ku "share project folders kwenye team..." Well organizations nyingi zinazofanya team projects zina internal volumes kwenye servers zao ambamo kuna shared access to folders of members or staff etc, team projects zinafanyika within those volumes, organizations nyingi zinataka mambo yake yafanyike within it digital space, sio kusambazwa sambazwa na ku postiwa kwenye ma server ya Ubuntu. Siku nyingine utazikuta Michuzi!
Kwa hiyo mpaka leo hujui jinsi ya ku transmit .exe file on line? I'm not going there, just google it.
"Offline approach ina favor large volumes tu..." Kumbe mi pointi yangu toka mwanzo nini? Nasema vi giga byte viwili vya kutunziwa na Ubuntu servers mimi sihitaji, nina archive mia tano ya hiyo, kumbe tunabishana nini kama unakubaliana kwa ukiwa na data set kubwa hivi vi service havina manufaa, kumbe unakubali, mbona unajichanganya au halafu una imply wenzio ndio tuna "matatizo ya ubongo"?
Mkuu sijasema wewe una matatizo ya ubongo nasema kama unasahau password una matatizo ya ubongo, usinielewe vibaya.
Hizi service zinasync, yaani hauweki mafaili kwenye Ubuntu kisha unayafuta kwenye PC, so risk ya kupoteza password uunapoteza access ya online storage tu haupotezi actual files. Anyway service za online zina password recovey mechanism "reset password" hii ni non issue.
Nakuhakikishia hauitaji account ya Dropbox kushare mafaili ya mtu, ndo maana nakuambia ungejaribu kabla ya kukomment kwa mfano link hii
http://dl.dropbox.com/u/4270110/Penguins.jpg
ni file ambalo nimelidondosha kwenye dropbox folder yangu, nimeliright click na kuchagua Public link, now naweza kushare na mtu yoyote na wewe unaweza kuliona nadhani. Hauna haja ya account.
Kwani wewe kwenye PC unafanya "kazi zako" tu? Hausomi JF? hausomi docs, pdfs, pictures haufanyi kitu chochote kisichohitaji Pentium i7 processor na gigabytes of RAM?
Najua makampuni yana internal services, lakini sio kila kampuni linayo na sio kila mtu anafanya projects kwenye kampuni tu, nimetumia sana hii kitu kwenye school project zangu. Na hizo internal services siku hizi zinarun juu ya hizi hizi tunazotumia sisi kama box.net.
Anyway internal service haizimzuii kupost vitu kwenye michuzi nadhani hiyo ni misconception.
Sio tatizo la kujua jinsi ya kutuma exe/file online, tatizo ni which is the best most convenient and efficient way ya kushare mafaili online. Wote tunajua jinsi ya kutuma traditional mail lakini tunatumia email why? Convenience and efficiency.
Sikatai point yako ya large storage ila kwa point hiyo tu kuikataa service kabisa ni very short sighted, usiwe one dimensional kwenye analysis yako, there is more to file storage than cost.
Hakuna aliyesema "Ubuntu one ni kwa ajili ya kutunzia data sets kubwa tu, na hauna haja ya kuwa na HDs" wewe ndo umeona 5GB ukazarau moja kwa moja service nzima. Ni vizuri uwe na upeo mkubwa kwenye mambo ya tech.
Edit: Nimeshau, backup ya copy/paste ni ya kujidanganya mkuu, fuata ushauri wangu kwenye hilo, kabla hayajakukumba!