Ubunifu waibeba Arumeru ujenzi wa madarasa

MMASSY

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
290
193
Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe David Lusinde (Mb) amesema kitendo cha ubunifu wa ujenzi wa shule tatu za mchepuo wa kingereza ambazo zitakuwa zinamilikiwa na Serikali kupitia Halmashauri ya Arusha Dc zitasaidia kuchochea kasi ya Ujenzi wa madarasa kutokana na mapato ya shule hizo kila mwaka kwenda katika kampeni ya ujenzi wa Madarasa hatua itakayopunguza mzigo kwa wananchi katika kusaidia ujenzi wa madarasa

Mhe Silinde ameyasema hayo baada ya ukaguzi wa majengo ya shule ya kwanza ya mchepuo wa kingereza ya Mringa English Medium School inayojengwa kutokana na fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri itasaidia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa lakini pia itakuwa ni moja ya chanzo endelevu cha mapato kwa Halmashauri ambayo yatakwenda kuongeza nguvu katika kampeni ya kila mwaka ya ujenzi wa madarasa

Kwa Upande wake Mkuu wa wilaya ya Arumeru na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Dc Saad Mtambule wamesema shule hiyo itakuwa na uwezo wa kuingiza zaidi ya milioni 500 kwa mwaka itakapokamilika na wanatarajia kujenga shule kama hizo tatu ili kuweza kupata mapato ya bilioni moja na nusu 1.5 Bilion fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zitatumika katika ujenzi wa madarasa kwenye shule na maeneo mengine yenye uhitaji
 
1611348068117.png
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom